Wahitimu wa Jeshi wa Zimamoto na Uokoaji wa kozi ya kuzima moto wa ndege
wakizima moto kwenye ndege bandia kabla ya mafunzo yao kufungwa na Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Maofisa na Askari 21 wa jeshi hilo
walihitimu mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti katika hafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na
wahitimu na wageni waalikwa kabla ya kufunga mafunzo ya kozi ya uzimaji moto wa
ndege. Maofisa na Askari 21 walihitimu kozi hiyo na kutunukiwa vyeti katika
sherehe fupi ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius Nyambacha.
Kulia ni Meja Generali Kapwani, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi
zawadi ya cheti mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo darasani, Mohammed
Shomari (kulia). Akizungumza baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu 21 wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji waliomaliza mafunzo ya kozi ya kuzima moto wa ndege, Waziri
Nchimbi aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao wakiiheshimu
kazi. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius
Nyambacha. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kikosi cha gwaride la wahitimu kikitoa heshima mbele ya mgeni rasmi
(hayupo pichani) wakati wa sherehe yao ya kumaliza mafunzo ya kozi ya kuzima
moto wa ndege kwa maofisa na askari 21 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
waliohitimu kozi hiyo jijini Dar es Salaam leo. Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye aliyafunga mafunzo ya kozi hiyo aliwataka
wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao wakiiheshimu kazi.
Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius Nyambacha, akimshukuru Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) kwa kukubali wito wao
wa kuja kuyafunga mafunzo ya Maofisa na Askari 21 wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji waliohitimu mafunzo ya kozi ya kuzima moto wa ndege. Waziri Nchimbi
katika hotuba yake aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao
wakiiheshimu kazi.
Picha zote na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
maafisa hao wanaozima moto hawajavaa cha helmet (hard hat) wala gloves. moto gani huo watazima.
ReplyDeletehata kama ni demo, bado kuna umuhimu wa kuvaa hizo protection kujenga mazoea.