Qunu ni kijiji kidogo katika jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini, kilomita 32 Kusini-Magharibi ya mji wa Mthatha, katika barabara ya Butterworth na Mthata.
Kijiji cha Mvezo, pembezoni mwa mto Mbashe, ni jirani ya mahali ambapo Mzee Nelson Mandela alizaliwa.
Hapo Qunu ndipo alipokulia na aliweka nadhiri ya kurejea.
Kijiji cha Qunu ndipo baba yake Mandela alipohamia baada ya kuvuliwa Uchifu wa Mvezo.
Katika kitabu chake cha ‘Long Walk to Freedom’ Mzee Mandela amekitaja kijiji hicho kuwa ndipo alipoishi maisha ya furaha wakati wa utotoni.
Jumapili ya Desemba 15, 2013 Mzee Mandela alizikwa kijijini Qunu katika mazishi ya Kitaifa yaliyoshuhudiwa dunia nzima.
Alizikwa kwa heshima zote za kiongozi wa Taifa na Chifu wa kimila katika sehemu aliyochagua mwenyewe kuwa nyumba yake ya milele.
yani hapo ni kijijini kila mwanakijiji anausafiri mweh
ReplyDeleteInapendeza. NI kijijini lakini hakuna nyumba za udongo na nyasi.
ReplyDeleteCha zaidi ya maendeleo ya kawaida, Kijiji kipo Kijaniii!
ReplyDeleteNi jambo zuri saaana!
Mbona mnasifia majani kijiji hakina hata mti wa asili huku. Sio kimeathiriwa na kukata miti.
ReplyDeleteNyumba zinaeleweka zinapendeza, tujifunze kuwa nanyumba bora vijijini.
ReplyDelete