Qunu ni kijiji kidogo katika jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini, kilomita 32 Kusini-Magharibi ya mji wa Mthatha, katika barabara ya Butterworth na Mthata. Kijiji cha Mvezo, pembezoni mwa mto Mbashe, ni jirani ya mahali ambapo Mzee Nelson Mandela alizaliwa. 
Hapo Qunu ndipo alipokulia na aliweka nadhiri ya kurejea. Kijiji cha Qunu ndipo baba yake Mandela alipohamia baada ya kuvuliwa Uchifu wa Mvezo. 
Katika kitabu chake cha ‘Long Walk to Freedom’ Mzee Mandela amekitaja kijiji hicho kuwa ndipo alipoishi maisha ya furaha wakati wa utotoni. Jumapili ya Desemba 15, 2013 Mzee Mandela alizikwa kijijini Qunu katika mazishi ya Kitaifa yaliyoshuhudiwa dunia nzima. 
Alizikwa kwa heshima zote za kiongozi wa Taifa na Chifu wa kimila katika sehemu aliyochagua mwenyewe kuwa nyumba yake ya milele.
Mandhari ya kijiji cha Qunu.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. yani hapo ni kijijini kila mwanakijiji anausafiri mweh

    ReplyDelete
  2. Inapendeza. NI kijijini lakini hakuna nyumba za udongo na nyasi.

    ReplyDelete
  3. Cha zaidi ya maendeleo ya kawaida, Kijiji kipo Kijaniii!

    Ni jambo zuri saaana!

    ReplyDelete
  4. Mbona mnasifia majani kijiji hakina hata mti wa asili huku. Sio kimeathiriwa na kukata miti.

    ReplyDelete
  5. Nyumba zinaeleweka zinapendeza, tujifunze kuwa nanyumba bora vijijini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...