Namuonea huruma huyo kocha mpya wa Manchester United.
Leo najidai kuwa Sheikh Yahya mpya, natabiri jamaa atapigwa teke karibuni. Recodi yake yatisha.
Man U wamefungwa na Everton timu ambayo haijaifunga Manu tangu 1992, na Moyes alipokuwa kocha wa Everton hakuwahi kuifunga Man U..Juzi Manu tena wamefungwa na Newcastle timu ambayo haijaifunga Man U tangu 1972. Na vipigo vyote vimetokea nyumbani kwenye uwanja wao.
Audhubillah
Mdau Ibrahim



Wadau wa soka wanaamini kuwa ManU walikuwa wakibebwa wakati wa enzi za Sir Alex Ferguson.
ReplyDeleteMdau, kocha hapaswi kulaumiwa hata kidogo kwa timu kufanya vibaya, kumbuka amechukua mikoba timu ikiwa na wachezaji karibia wote ni walemavu kwa maana wamekamuliwa kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo na serious SAF. kwa hiyo hata ukiangalia kwa makini utagundua ile kasi ya mchezaji mmoja mmoja imepungua sana. Apewe fursa aunde kikosi kingine na mambo yatanyooka, kumbuka hata SAF alitaka kufukuzwa mwanzoni.
ReplyDeleteKuna Mkenya kajiuwa baada ya matokeo ya Jumamosi.
ReplyDeletehttp://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2520757/Kenyan-football-fan-commits-suicide-Manchester-United-lose-Newcastle-United-Old-Trafford.html
kila lenye mwanzo huwa na mwisho , na aliye juu msubiri chini, na aliye chini msubiri juu , ukitafakari maneno haya utaelewa maisha na mizunguko yake , hakuna cha milele ktk maisha ya kibinadamu , lazima ukubali kuna kushinda na kushindwa falsafa hii huwa inakubalika katika michezo , lakini wanasiasa ni wagumu kuelewa wanataka kila siku iwe chama fulani tu kinatawala hata wakishindwa basi hughushi kura mradi washinde , ni vyema kwa wanasiasa wakachukua mifano hii inayotokea ktk michezo na kuiga uzalendo wa wanamichezo
ReplyDelete