Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar  kupitia Chama cha CHADEMA Bwa. Hashim Juma Issa
Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akitowa maelezo kwa Mgombea wa CHADEMA Bwa Hashim, alipofika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya MjiniMagharibi Maisara kuchukua fomu ya kugombea Uwakilishi wa Jimbo hilo lillilokuwa Wazi baada ya Mwakilishi wake kuvuliwa Uwanachama na Chama chake Mhe, Mansoor Yussuf Himid, mwaka jana 
 Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akimkabidhi Fomu Mgombea wa Uwakilishi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
 Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Hashim Juma Issa akisaini baada ya kupokea fomu hizo kutoka kwa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. samahani kama itachukuliwa tofauti..nataka tu kujua hivi zanzibari hakuna wakritu maana sijawahi kusoma mtu wa nyadhifa yoyote kutoka huko akiwa mkristu ,unless nimesahau

    ReplyDelete
  2. jaji agostino ramadhani naye ni mkristo. hafu ujue kuwa zanzibar asilimia 99 ni waislamu; kwa hiyo usitegemee kuona wakristo wengi. kwa tanganyika waislamu nao wako wengi lakini maofisini na kwingineko idadi yao iko kidogo sana, jaribu kufanya tafiti halafu ulete jibu.

    ReplyDelete
  3. Jaji Augostino Ramadhan, Balozi Isack Sepetu, ...

    ReplyDelete
  4. Sylvester Mabuma ni mbunge mojawapo wa kuchaguliwa moja kwa moja kwa kura za wananchi wenzake wa Zanzibar.

    ReplyDelete
  5. wenyeji wa znz asilimia kubwa ni waislam na wapo kama wawili nafkiri wawakilishi au mbunge ni mkristo

    ReplyDelete
  6. Vile vile Marehemu Adam Mwakanjuki alikuwa waziri Zanzibar kwa miaka mingi tu.

    Wako akina Raphael Banzi alikuwa katibu mkuu,Joseph Meza na akina Kisasi wamewahi kuwa kwenye system kwa miaka mingi tu.

    ReplyDelete
  7. Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko CHADEMA kupata ushindi ktk jimbo lolote Zanzibar. Hivyo, ni bora kutosimamisha mgombea. Maana mtaambulia asilimia < 5%.

    ReplyDelete
  8. Mhe Hashim Juma issa anatambulikana kua mzee mwenye busara na uchungu kwenye mamuzi ya kitaifa hususan ZANZIBAR. wa busara hii nina amini kua anaweza leta faida na maendeleo, tuombe mungu. maana amejitahidi sana kuleta haki na tamaduni ya uhuru kwa wazanzibari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...