Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akitowa maelezo kwa Mgombea wa CHADEMA Bwa Hashim, alipofika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya MjiniMagharibi Maisara kuchukua fomu ya kugombea Uwakilishi wa Jimbo hilo lillilokuwa Wazi baada ya Mwakilishi wake kuvuliwa Uwanachama na Chama chake Mhe, Mansoor Yussuf Himid, mwaka jana
Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Suluhu Ali Rashid, akimkabidhi Fomu Mgombea wa Uwakilishi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Hashim Juma Issa akisaini baada ya kupokea fomu hizo kutoka kwa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki
samahani kama itachukuliwa tofauti..nataka tu kujua hivi zanzibari hakuna wakritu maana sijawahi kusoma mtu wa nyadhifa yoyote kutoka huko akiwa mkristu ,unless nimesahau
ReplyDeletejaji agostino ramadhani naye ni mkristo. hafu ujue kuwa zanzibar asilimia 99 ni waislamu; kwa hiyo usitegemee kuona wakristo wengi. kwa tanganyika waislamu nao wako wengi lakini maofisini na kwingineko idadi yao iko kidogo sana, jaribu kufanya tafiti halafu ulete jibu.
ReplyDeleteJaji Augostino Ramadhan, Balozi Isack Sepetu, ...
ReplyDeleteSylvester Mabuma ni mbunge mojawapo wa kuchaguliwa moja kwa moja kwa kura za wananchi wenzake wa Zanzibar.
ReplyDeletewenyeji wa znz asilimia kubwa ni waislam na wapo kama wawili nafkiri wawakilishi au mbunge ni mkristo
ReplyDeleteVile vile Marehemu Adam Mwakanjuki alikuwa waziri Zanzibar kwa miaka mingi tu.
ReplyDeleteWako akina Raphael Banzi alikuwa katibu mkuu,Joseph Meza na akina Kisasi wamewahi kuwa kwenye system kwa miaka mingi tu.
Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko CHADEMA kupata ushindi ktk jimbo lolote Zanzibar. Hivyo, ni bora kutosimamisha mgombea. Maana mtaambulia asilimia < 5%.
ReplyDeleteMhe Hashim Juma issa anatambulikana kua mzee mwenye busara na uchungu kwenye mamuzi ya kitaifa hususan ZANZIBAR. wa busara hii nina amini kua anaweza leta faida na maendeleo, tuombe mungu. maana amejitahidi sana kuleta haki na tamaduni ya uhuru kwa wazanzibari
ReplyDelete