Marehemu Felician B. Lutazengelera
25 Novemba 1949 – Desemba, 2013
Kwa masikitiko makubwa, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italia anasikitika kutangaza kifo cha raia wa Tanzania, MAREHEU FELICIAN B. LUTAZENGELERA, ambaye picha yake imeonyeshwa hapo juu.
Taarifa za kifo hicho zimepokelewa Ubalozini tarehe 14/01/2014 kutoka kwa Mamlaka ya Jiji la Milani, Italia, ambako mwili wa marehemu uliokotwa mtaani hapo tarehe 21/12/2013. 
Kwa wiki mbili sasa Ubalozi haujafanikiwa kuwapata ndugu wa marehemu, na sasa Ubalozi unatoa tangazo hili leo 29/01/2014 ukiomba msaada ili kuwapata ndugu wa marehemu.
Ubalozi utashukuru kupokea taarifa kuhusu anuani, na simu, za ndugu wa marehemu kupitia anuani ya baruapepe: info@embassyoftanzaniarome.info  
Asanteni kwa ushirikiano

Tangazo limetolewa na Balozi James Alex Msekela, 
Roma, Italia.
Simu: +39 0633 4858 20 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mungu amlaze mahala pema peponi Marehemu. Ila anaonekana kama Msomali vile?

    ReplyDelete
  2. mnyarwanda...RIP

    ReplyDelete

  3. RIP Felician. Kwa wanaoishi nje ya Tanzania au waliowaishi nje ya Tanzania huko ugenini, hili ni jambo ambalo uwa tunaomba lisitukute....kuangukia ugenini...
    Wote tumetoka home TZ kwenda nje kutafuta na wote twataka turudi salama nyumbani kwa ndugu na jamaa zetu salama usalmini. lakini yote ni ya mungu...
    Poleni kwa wafiwa....na upumzike salama Felician....ingawa sikukufahamu....

    ReplyDelete
  4. RIP ndugu. Nafahamu libeneke lina wafuasi lukuki, ila mpaka sasa hakuna hata fununu za anayemfahamu marehemu. Jina kama sio la Kihaya ni la Kiganda au Kinyarwanda, ila wajihi na sura yake kama vile Msomali au Mhabeshi.

    ReplyDelete
  5. Wadau wa 1 wa 2 na wa 4 tuache Ukabila na Ubaguzi tuangalie Msiba kwanza!!!

    ReplyDelete
  6. Ohooo, amekutana na Ma-Mafia wa Kiitaliana!

    ReplyDelete
  7. Biteya Charles lutatazaFebruary 02, 2014

    Ni msiba mkubw a huyu ni kaka yangu nikopamoja na wanablog katika maombolezo. Mipango ya Mazishi inaf anyika tuweze kumuweka katika nyumba yake ya ku dumu

    Mungu amulaze mahali pema peponi

    Biteya charles lutataza
    0713455737

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...