Marehemu Felician B. Lutazengelera
25 Novemba 1949 – Desemba, 2013
25 Novemba 1949 – Desemba, 2013
Kwa masikitiko makubwa, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Italia anasikitika kutangaza kifo cha raia wa Tanzania, MAREHEU FELICIAN B. LUTAZENGELERA, ambaye
picha yake imeonyeshwa hapo juu.
Taarifa za kifo hicho zimepokelewa Ubalozini tarehe
14/01/2014 kutoka kwa Mamlaka ya Jiji la Milani, Italia, ambako mwili wa
marehemu uliokotwa mtaani hapo tarehe 21/12/2013.
Kwa wiki mbili sasa Ubalozi
haujafanikiwa kuwapata ndugu wa marehemu, na sasa Ubalozi unatoa tangazo hili
leo 29/01/2014 ukiomba msaada ili kuwapata ndugu wa marehemu.
Ubalozi utashukuru kupokea taarifa kuhusu anuani, na
simu, za ndugu wa marehemu kupitia anuani ya baruapepe: info@embassyoftanzaniarome.info
Asanteni kwa ushirikiano
Tangazo
limetolewa na Balozi James Alex Msekela,
Roma, Italia.
Simu: +39 0633 4858 20
Simu: +39 0633 4858 20
Mungu amlaze mahala pema peponi Marehemu. Ila anaonekana kama Msomali vile?
ReplyDeletemnyarwanda...RIP
ReplyDelete
ReplyDeleteRIP Felician. Kwa wanaoishi nje ya Tanzania au waliowaishi nje ya Tanzania huko ugenini, hili ni jambo ambalo uwa tunaomba lisitukute....kuangukia ugenini...
Wote tumetoka home TZ kwenda nje kutafuta na wote twataka turudi salama nyumbani kwa ndugu na jamaa zetu salama usalmini. lakini yote ni ya mungu...
Poleni kwa wafiwa....na upumzike salama Felician....ingawa sikukufahamu....
Mgogo?
ReplyDeleteRIP ndugu. Nafahamu libeneke lina wafuasi lukuki, ila mpaka sasa hakuna hata fununu za anayemfahamu marehemu. Jina kama sio la Kihaya ni la Kiganda au Kinyarwanda, ila wajihi na sura yake kama vile Msomali au Mhabeshi.
ReplyDeleteWadau wa 1 wa 2 na wa 4 tuache Ukabila na Ubaguzi tuangalie Msiba kwanza!!!
ReplyDeleteOhooo, amekutana na Ma-Mafia wa Kiitaliana!
ReplyDeleteNi msiba mkubw a huyu ni kaka yangu nikopamoja na wanablog katika maombolezo. Mipango ya Mazishi inaf anyika tuweze kumuweka katika nyumba yake ya ku dumu
ReplyDeleteMungu amulaze mahali pema peponi
Biteya charles lutataza
0713455737