Na John Gagarini, Kibaha 

 KIJANA Victor Wilfred (29) mkazi wa Keko jijini Dar es Salaam amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kanga aliyoifunga kwenye dirisha la chumba cha rafiki yake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Ulrich Matei alisema kuwa marehemu alifika kwa rafiki yake hapa Kibaha kwa lengo la kutafutiwa kazi.

Kamanda Matei amesema kuwa tukio hilo lilitokea leo Aprili 30 mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi eneo la Maili Moja Shuleni wilayani Kibaha mkoani Pwani ambapo umati wa watu ulikuwa umejazana kushuhudia tukio hilo la kusikitisha.

Alisema kuwa tukio hilo ambalo lilitokea kwenye sebule ya chumba cha Emanuel Lawrance mkazi wa Keko Jijini Dar es Salaam ambaye amepangisha nyumba kwa Emanuel Msengi ambapo marehemu alikuwa mgeni kwenye nyumba hiyo na alifika kwa lengo la kutafuta kazi.

"Marehemu aliachwa na rafiki yake ambaye alikuwa amekwenda kazini na kwa kuwa rafiki yake alimuahidi kumtafutia kazi na aliporudi alikuta marehemu kajinyonga kwa kutumia kanga kwenye dirisha la chumba hicho," alisema Kamanda Matei.

Hata hivyo marehemu aliacha ujumbe kwenye karatasi lililokutwa pembeni ya mwili wake kuwa kutokanana na kifo chake anaomba samahani na asisumbuliwe mtu yoyote kwani kaamua kujiua yeye mwenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. TANZANIA JAMANI....!kwakweli inasikitisha na inauma sana....R.I.P

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2014

    Tuwatafutie ajira vijana wetu. Wanakosa matumaini. RIP

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2014

    Mtu anayejinyonga anakuwa amesumbuliwa na mawazo mengine bila kutafuta ufumbuzi kwa kuongea na wengine au kutafuta counselling/ushauri nasaa kutoka kwa waliosomea counselling au madaktari wa akili. Wakati huu ambapo kulipa bili kuingia mpaka vijijini na matatizo mengine ya mahusiano na watu kwenye biashara na ndoa tunahitaji huduma hizi ziongezeke kusaidia wale wanaopata msongo wa mawazo. Huduma hizi ulaya hutolewa pia kwa simu kumruhusu mtu kutoa yaliyo moyoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...