Na John Gagarini, Kibaha
KIJANA Victor Wilfred (29) mkazi wa Keko jijini Dar es Salaam amekufa
kwa kujinyonga kwa kutumia kanga aliyoifunga kwenye dirisha la chumba
cha rafiki yake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Ulrich Matei alisema kuwa
marehemu alifika kwa rafiki yake hapa Kibaha kwa lengo la kutafutiwa
kazi.
Kamanda Matei amesema kuwa tukio hilo lilitokea leo Aprili 30 mwaka huu
majira ya saa 5 asubuhi eneo la Maili Moja Shuleni wilayani Kibaha
mkoani Pwani ambapo umati wa watu ulikuwa umejazana kushuhudia tukio
hilo la kusikitisha.
Alisema kuwa tukio hilo ambalo lilitokea kwenye sebule ya chumba cha
Emanuel Lawrance mkazi wa Keko Jijini Dar es Salaam ambaye amepangisha
nyumba kwa Emanuel Msengi ambapo marehemu alikuwa mgeni kwenye nyumba
hiyo na alifika kwa lengo la kutafuta kazi.
"Marehemu aliachwa na rafiki yake ambaye alikuwa amekwenda kazini na
kwa kuwa rafiki yake alimuahidi kumtafutia kazi na aliporudi alikuta
marehemu kajinyonga kwa kutumia kanga kwenye dirisha la chumba hicho,"
alisema Kamanda Matei.
Hata hivyo marehemu aliacha ujumbe kwenye karatasi lililokutwa pembeni
ya mwili wake kuwa kutokanana na kifo chake anaomba samahani na
asisumbuliwe mtu yoyote kwani kaamua kujiua yeye mwenyewe.
TANZANIA JAMANI....!kwakweli inasikitisha na inauma sana....R.I.P
ReplyDeleteTuwatafutie ajira vijana wetu. Wanakosa matumaini. RIP
ReplyDeleteMtu anayejinyonga anakuwa amesumbuliwa na mawazo mengine bila kutafuta ufumbuzi kwa kuongea na wengine au kutafuta counselling/ushauri nasaa kutoka kwa waliosomea counselling au madaktari wa akili. Wakati huu ambapo kulipa bili kuingia mpaka vijijini na matatizo mengine ya mahusiano na watu kwenye biashara na ndoa tunahitaji huduma hizi ziongezeke kusaidia wale wanaopata msongo wa mawazo. Huduma hizi ulaya hutolewa pia kwa simu kumruhusu mtu kutoa yaliyo moyoni.
ReplyDelete