Mlipuko unaosadikiwa ni bomu umelipuka usiku wa kuamkia leo jijini Arusha  katika mgahawa wa  Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa hotel ya Gymkana jijini hapa na kujeruhi watu nane.

Akithibitisha kupokea wagonjwa walioadhiriwa na bomu hilo  Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo Kisanga  alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:30 usiku katika eneo kwani walianza kupokea wagonjwa hao kuanzia majira ya saa tano kasoro na saatano .

Alisema kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.

"kati yawagonjwa hao nane mmoja alitwa akiwa mahututi sana kwani mguu wake ulikuwa umeadhiriwa sana na bomu hiloivyo ikatulazimu  kumkata mguu mmoja wa kushoto ,kwakweli mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa  Deepak Gupta (25) mwanaume na sasa ivi anaendelea vyema kidogo na yupo katika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani"alisema Kisanga

Alisema kuwa  katika majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya uangalizi wa madaktari

Aidha aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na  Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25)  wote wakiwa na asili ya kiasia
Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio  waliofika hapo hospitali walidai kuwa   bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.
  Pichani ni Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ kitengo cha Mabomu wakiwa  katika eneo la tukio ambapo bomu lilirushwa ndani ya Mgahawa ujulikanao  kwa jina la Traditional Indian Cusine uliopo pembeni ya hotel ya Gymkana jijini Arusha,aidha taarifa za awali zinaeleza kuwa watu nane wamejeruhiwa vibaya na mlipuko huo
 Picha ni majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25),akiwa amelazwa katika hospitali ya Selian,katika chumba cha watu mahututi (ICU),mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto kutokana na mhuu huo kujeruhiwa vibaya na bomu.
 Sehemu ya baadhi ya watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea jana usiku katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Selian,jijini Arusha kwa matibabu.
Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo akiongea na waandishi wa habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2014

    Duh! Yaani haya mambo tulikua tunasikia tu kwenye taarifa za habari, sasa yamefika kwetu! Ee Mola turehemu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2014

    Jamani, tusishangae tu kwa nini Kenya mabomu kila kukicha sasa ni zamu yetu Tanzania. Kwa nini Arusha mabomu hayaishi? serikali inajipangaje jamani na suala hili? mbona kimya sana kwani hawaoni hilo? Ee Mungu utusamehe waja wako hatujui mambo ya vita. Mama Maria mama wa Mungu utuombee tuepukane na janga hili Amina. Mungu ibariki Afrika na Tanzania.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2014

    Uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu kiini cha vurugu hizi, je zinahusiana na zile zilizopita au ni watu wana maswala mengine na maadui zao?.

    Ni wiki iliyopita ambapo mtu mmoja alilipuliwa bomu miguuni, pamoja na sheria kuchukua mkondo wake waliohusika wajibu.
    Kama inawezekana wazee wa dini watafutwe hata kama siyo wa mkoa huo kama kuna maswala au magomvi ya kutatuliwa pia yashughulikiwe ili watu wasiishi kwa woga. Hii hali si nzuri kwa nchi na katika msimu wa utalii kama huu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2014

    Poleni wahanga wa mkasa huu, nawatakia hafueni ya haraka.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2014

    Ndugu zanguni Watanznaia mmeshalitafakari kwa makini haya matatizo ya mabomu Arusha?
    Kweli inasikitisha sana,hao watu wanao amua kufanya hivyo wanataka nini??
    -Je ni mambo ya Siasa/?
    -Ukabila??
    -Udini??
    -ni nini hasa??

    -Arusha walishapiga bomu kwenye mkusanyiko wakisiasa..
    -Arusha walishapiga Bomu Kanisani..
    -Arusha washapiga Bomu Nyumbani kwa Sheihk Imamu.
    -Sasa wamepiga Bomu kwa Wahindi.

    Nini kinaendelea Arusha watanzania wenzangu.
    Na ni nani anafanya haya maovu.

    EEH MUNGU IBARIKI NCHI YANGU NA KUIPA AMANI KWANI HATUJUI TUENDAKO.

    Mdau.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2014

    Hii lazima ni hujuma....

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 12, 2014

      Katika wote ww umehisi sawa.
      Hii ni ishu ya kibiashara , hakuna ugaidi hapo
      Mdau USA

      Delete
  7. AnonymousJuly 08, 2014

    mungu tusaidie na tunaomba uwape majeruhi wote uponyaji

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2014

    Matatizo ya mabomu Arusha yalianza kama mchezo,kuanzia kwenye mikutano ya kisiasa,mikusanyiko ya kidini na sasa maeneo ya starehe ni wazi tatizo hili lina endelea kukuwa na kama lisipothibitiwa haraka litakuwa janga la Taifa kumbuka "Hata mbuyu ulianza kama mchicha"- Somalia nayo ilianza taratibu namna hii.Ni wakati wa Serikali kuwa serious na kuhakikisha inawakamata wahusika na kuwafanya mfano ili wengine wasiige.Waslwahili wanasema "Ukicheza na moto wa mjinga,utakuchomea nguo"...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2014

    mbona mlango wa hiyo nyumba una alama ya 'Hitler?'

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2014

    Wewe mdau no 1 acha unafiki sio vitu vigeni kwetu kumbuka mwembe chai zanzibar pemba hadi tanzania ikatoa wakimbizi kule shimoni mombasa kunya anye kuku bata kaharisha

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2014

    Jamani Watanzania tunakwenda wapi, na tatizo ni nini hasa? Hivi kudhuru watu ndio suluhisho la tunayoyalalamikia, iwe ni yoyote yale.

    ReplyDelete
  12. Alama uliotaja inafanana na alama waliotumia Wajerumani wakati utawala wa Nazi lakini ukiangalia vizuri alama huu ina "dots" nne. Swastika kama alama kinatumika kwenye dini ya Hinduism, Jainism na Buddhism.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...