Mlipuko unaosadikiwa ni bomu umelipuka usiku wa kuamkia leo jijini Arusha katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa hotel ya Gymkana jijini hapa na kujeruhi watu nane.
Akithibitisha kupokea wagonjwa walioadhiriwa na bomu hilo Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo Kisanga alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:30 usiku katika eneo kwani walianza kupokea wagonjwa hao kuanzia majira ya saa tano kasoro na saatano .
Alisema kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.
"kati yawagonjwa hao nane mmoja alitwa akiwa mahututi sana kwani mguu wake ulikuwa umeadhiriwa sana na bomu hiloivyo ikatulazimu kumkata mguu mmoja wa kushoto ,kwakweli mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa Deepak Gupta (25) mwanaume na sasa ivi anaendelea vyema kidogo na yupo katika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani"alisema Kisanga
Alisema kuwa katika majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya uangalizi wa madaktari
Aidha aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25) wote wakiwa na asili ya kiasia
Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio waliofika hapo hospitali walidai kuwa bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.
Pichani ni Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ kitengo cha Mabomu wakiwa katika eneo la tukio ambapo bomu lilirushwa ndani ya Mgahawa ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine uliopo pembeni ya hotel ya Gymkana jijini Arusha,aidha taarifa za awali zinaeleza kuwa watu nane wamejeruhiwa vibaya na mlipuko huo
Picha ni majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25),akiwa amelazwa katika hospitali ya Selian,katika chumba cha watu mahututi (ICU),mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto kutokana na mhuu huo kujeruhiwa vibaya na bomu.
Sehemu ya baadhi ya watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea jana usiku katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Selian,jijini Arusha kwa matibabu.
Duh! Yaani haya mambo tulikua tunasikia tu kwenye taarifa za habari, sasa yamefika kwetu! Ee Mola turehemu.
ReplyDeleteJamani, tusishangae tu kwa nini Kenya mabomu kila kukicha sasa ni zamu yetu Tanzania. Kwa nini Arusha mabomu hayaishi? serikali inajipangaje jamani na suala hili? mbona kimya sana kwani hawaoni hilo? Ee Mungu utusamehe waja wako hatujui mambo ya vita. Mama Maria mama wa Mungu utuombee tuepukane na janga hili Amina. Mungu ibariki Afrika na Tanzania.
ReplyDeleteUchunguzi wa kina ufanyike kuhusu kiini cha vurugu hizi, je zinahusiana na zile zilizopita au ni watu wana maswala mengine na maadui zao?.
ReplyDeleteNi wiki iliyopita ambapo mtu mmoja alilipuliwa bomu miguuni, pamoja na sheria kuchukua mkondo wake waliohusika wajibu.
Kama inawezekana wazee wa dini watafutwe hata kama siyo wa mkoa huo kama kuna maswala au magomvi ya kutatuliwa pia yashughulikiwe ili watu wasiishi kwa woga. Hii hali si nzuri kwa nchi na katika msimu wa utalii kama huu.
Poleni wahanga wa mkasa huu, nawatakia hafueni ya haraka.
ReplyDeleteNdugu zanguni Watanznaia mmeshalitafakari kwa makini haya matatizo ya mabomu Arusha?
ReplyDeleteKweli inasikitisha sana,hao watu wanao amua kufanya hivyo wanataka nini??
-Je ni mambo ya Siasa/?
-Ukabila??
-Udini??
-ni nini hasa??
-Arusha walishapiga bomu kwenye mkusanyiko wakisiasa..
-Arusha walishapiga Bomu Kanisani..
-Arusha washapiga Bomu Nyumbani kwa Sheihk Imamu.
-Sasa wamepiga Bomu kwa Wahindi.
Nini kinaendelea Arusha watanzania wenzangu.
Na ni nani anafanya haya maovu.
EEH MUNGU IBARIKI NCHI YANGU NA KUIPA AMANI KWANI HATUJUI TUENDAKO.
Mdau.
Hii lazima ni hujuma....
ReplyDeleteKatika wote ww umehisi sawa.
DeleteHii ni ishu ya kibiashara , hakuna ugaidi hapo
Mdau USA
mungu tusaidie na tunaomba uwape majeruhi wote uponyaji
ReplyDeleteMatatizo ya mabomu Arusha yalianza kama mchezo,kuanzia kwenye mikutano ya kisiasa,mikusanyiko ya kidini na sasa maeneo ya starehe ni wazi tatizo hili lina endelea kukuwa na kama lisipothibitiwa haraka litakuwa janga la Taifa kumbuka "Hata mbuyu ulianza kama mchicha"- Somalia nayo ilianza taratibu namna hii.Ni wakati wa Serikali kuwa serious na kuhakikisha inawakamata wahusika na kuwafanya mfano ili wengine wasiige.Waslwahili wanasema "Ukicheza na moto wa mjinga,utakuchomea nguo"...
ReplyDeletembona mlango wa hiyo nyumba una alama ya 'Hitler?'
ReplyDeleteWewe mdau no 1 acha unafiki sio vitu vigeni kwetu kumbuka mwembe chai zanzibar pemba hadi tanzania ikatoa wakimbizi kule shimoni mombasa kunya anye kuku bata kaharisha
ReplyDeleteJamani Watanzania tunakwenda wapi, na tatizo ni nini hasa? Hivi kudhuru watu ndio suluhisho la tunayoyalalamikia, iwe ni yoyote yale.
ReplyDeleteAlama uliotaja inafanana na alama waliotumia Wajerumani wakati utawala wa Nazi lakini ukiangalia vizuri alama huu ina "dots" nne. Swastika kama alama kinatumika kwenye dini ya Hinduism, Jainism na Buddhism.
ReplyDelete