Nani kasema Old School ni kwa muziki peke yake? Mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii Nathan Chiume na mai waifu wake wanakupa jibu la swali hilo wakiwa katika mfano wa studio za mpiga picha maarufu wa miaka ya sitini wa jijini Bamako, nchini Mali, Malick Sidibe, iliyo katika kituo kipya cha utamaduni wa Afrika (The Africa Centre: BOFYA HAPA) katika barabara ya tano na ya 110 (Fifth Avenue and 110th street) kitongoji cha Manhattan  hapo jijini New York kilichoanzishwa na bilionea Mo Ibrahim
 Hapo Nathan na Mai Waifu wake wanaonesha mapozi ya wapendanao walipokwenda studio hiyo. Yaani bila kuwa na redio, baiskeli ama pikipiki studio kulikuwa hakunogi.   Hehehe...si mchezo enzi hizo. Namna ya kuliingiza na kulitoa hilo bodaboda humo studio ni hadithi ingine. Kwa leo furahia taswira hizo huku ukijiuliza kuna ubaya wa kurudia huko?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Safi saaana. Nathan pinch imetoka ka vile enzi zile.

    ReplyDelete
  2. Me Love this!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...