Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akinzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulishwa kwake kujiunga na Chama cha ACT-Tanzania, katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe Lugano Mwaikenda.Picha zote na Othman Michuzi.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akionyesha kadi ya Chama chake kipya yenye namba 007194 mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano wa Chama cha ACT-Tanzania,uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena,jijini Dar es salaam leo. Kluia kwake ni Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe. Lugano Mwaikenda
![]() |
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe na Msanii Afande Sele wakionesha kadi zao za wanachama wa ACT-Tanzania.Wengine ni Dickson Ng'ili pamoja na Adam Shanzy. |
![]() |
Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe Lugano Mwaikenda akionesha vipeperushi vya chama chao wakati wa mkutano huo |
Sehemu ya Wanachama wa Chama ACT-Tanzania wakionyesha mabango ya kumkaribisha Mwanachama mwenzao Mhe. Zitto Kabwe.
Haaaa!Tunakutakia heri ingawa wahenga walisema mchagua jembe si mkulima,ajitengae na wenzake hujitafutia mambo yake mwenyewe na mvumilivu hula mbifu!natumie salama mamilioni ulopewa
ReplyDeleteCDM mmemfukuza ww ulitaka afanyaje?? halafu acha hayo ma methali ya kizamani eti mvumilivu hula mbivu, wakati mwingine mvumilivu hula zilizooza bwashee.. ZZK twanga twende tupo pamoja, na sie wa ughaibuni kadi za ACT tutapata wapi??
ReplyDeletemdau wa UK
ACT tuleteeni hizo kadi za 'Chama' huku Pemba, tuko wengi tuliochoshwa na siasa za huku.
ReplyDeleteTwanga zito twanga baba, tunataka mabadiliko, achana na hao wapambe wa CDM. watakufa kifo cha taratibu, ushabiki wetu ulikuwa ni wewe kwa vitu vikali ulivyokuwa unavitoa bungeni, wamepoteza lulu, wataitafuta hawataiona kamwe. haaaaaaaaa, haaaa wamebugi men.
ReplyDeleteKaka umefanya uamuzi wa busara, tukopamoja katika chama chetu cha wazalendo ACT. Mdau wa Dodoma
ReplyDelete