Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akinzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulishwa kwake kujiunga na Chama cha ACT-Tanzania, katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe Lugano Mwaikenda.Picha zote na Othman Michuzi.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akionyesha kadi ya Chama chake kipya yenye namba 007194 mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano wa Chama cha ACT-Tanzania,uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena,jijini Dar es salaam leo.  Kluia kwake ni Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe. Lugano Mwaikenda
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe  na Msanii Afande Sele wakionesha kadi zao za wanachama wa ACT-Tanzania.Wengine ni Dickson Ng'ili pamoja na Adam Shanzy.
Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe Lugano Mwaikenda akionesha vipeperushi vya chama chao wakati wa mkutano huo
 Sehemu ya Wanachama wa Chama ACT-Tanzania wakionyesha mabango ya kumkaribisha Mwanachama mwenzao Mhe. Zitto Kabwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Haaaa!Tunakutakia heri ingawa wahenga walisema mchagua jembe si mkulima,ajitengae na wenzake hujitafutia mambo yake mwenyewe na mvumilivu hula mbifu!natumie salama mamilioni ulopewa

    ReplyDelete
  2. CDM mmemfukuza ww ulitaka afanyaje?? halafu acha hayo ma methali ya kizamani eti mvumilivu hula mbivu, wakati mwingine mvumilivu hula zilizooza bwashee.. ZZK twanga twende tupo pamoja, na sie wa ughaibuni kadi za ACT tutapata wapi??
    mdau wa UK

    ReplyDelete
  3. ACT tuleteeni hizo kadi za 'Chama' huku Pemba, tuko wengi tuliochoshwa na siasa za huku.

    ReplyDelete
  4. Twanga zito twanga baba, tunataka mabadiliko, achana na hao wapambe wa CDM. watakufa kifo cha taratibu, ushabiki wetu ulikuwa ni wewe kwa vitu vikali ulivyokuwa unavitoa bungeni, wamepoteza lulu, wataitafuta hawataiona kamwe. haaaaaaaaa, haaaa wamebugi men.

    ReplyDelete
  5. Kaka umefanya uamuzi wa busara, tukopamoja katika chama chetu cha wazalendo ACT. Mdau wa Dodoma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...