Kiongozi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) katika Makazi ya Mishamo, Adolph Bishanga akimkabidhi chandarua na shuka raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses (kulia) baada ya kujifungua mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na UNHCR kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti.
Mkuu wa Makazi ya Ulyakulu, Abdulkarim Mnacho (kushoto) akimpongeza raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses baada ya kujifungua mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti.
Wakimbizi wanapewa uraia lakini wa tanzania wanaoishi nje na kuwa raia wa nchi hizo wananyimwa haki ya kuwa raia
ReplyDeleteHeri mimi manenge sijasema....asia na wapopo wanaochukua pasi kiulani na kutanua nazo ulaya....tunabaki midomo wazi mtu hajui lolote kuhusu Tz lakini ana pasi.
ReplyDeleteThe mdudu, nyie mwageni tu huo uraia kama mpunga lakini huko mbeleni mtakuja kujuta hivi O..kimbunga haikua mikoa yote? Hao kwao kushatulia na hakuna tatizo lolote sasa huo uraia niaje?
ReplyDelete