SIMON S. KAHEMELE
26th Julai 1965 – 14th Novemba 2014
Ni mwaka mmoja
sasa tangu ulipotuacha ghafla katika ajali ya gari.
Tukiwa tungali na majonzi
ya kuondokewa nawe katika ulimwengu huu, mambo mema uliyotufanyia ulipokuwa hai
bado yanaendelea kugusa maisha yetu.
Tunakukumbuka sana kila iitwapo leo na
nyakati tulizoshirikiana hazijafutika katika mioyo yetu. Mke wako, familia yako
na marafiki zako wanakupenda sana na kusikia upweke kwa kuondokewa nawe.
Leo
tumekusanyika Manda mahali ulipolala, ili kumshukuru na kumtukuza Mungu kwa
kutupa zawadi ya maisha yako hapa duniani na kwa kufungua rasmi kanisa (Simon’s
Memorial Chapel), hii ikiwa ni ukamilisho wa ndoto uliyokuwa nayo.
Shukrani za pekee ziwafikie ndugu, jamaa na
marafiki wote walioshirikiana nasi katika kufanikisha ndoto hiyo. Mungu
awazidishie pale palipopungua.
Daima Tunakukumbuka, Pumzika kwa Amani.
Ni kweli tulikupenda sana, lakini Mwenyezi alikupenda zaidi akakuchukua. RIP Simon.
ReplyDelete