Habari kaka Michuzi,
Naomba unifikishie katika blog yako maana naamini mpaka vyombo husika vitaliona hili.
Tarehe 16/11/2015 nilikua napita njia ya Kilwa,nilipofika mivinjeni nikakutana na hilo Gari la kubeba contena kama linavyoonekana katika picha,nikiwa nyuma yake likaingia Barabara ya vumbi iendayo bandarini kupitia Yara, nilimpigia sana honi na kumuwashia Taa huyo dereva asimame afanye taratibu za maksudi kunusuru uhai Wa RAIA wengine ila alikaidi,alishuka utingo wake akaangalia na kuendelea na safari, kiukweli lile kontena lilikua nje ya lock zake na lilikua likicheza sana kwenye njia ya vumbi na cha kushangaza kabisa lilipofika barabara ya bandari/shimo la udongo kulikua na traffic wanne barabarani lakini hawakuchukua hatua yoyote ile zaidi ya kuliangalia tu.
Tutaendelea kupoteza ndugu jamaa n marafiki zetu mpaka lini kwa uzembe Wa watu wachache wasiojali uhai wa wengine?
Wako Mdau.
Lori hilo likikata kona kutokea barabara kubwa kuelekea bandarini kupitia Yara.
Hii hatari sana! uzuri Kamanda Mpinga huwa anazungukia kwenye mitandao I hope atakua kaiona hii na kuchukua hatua muafaka!
ReplyDeleteThe mdudu, watu wazembe kama wewe mdau uliowaona siku nyingine wapigie mayowe kwa raia wema lazima wangesogea ulipo kisha unawaambia hawa watu wameingia huku na mgari wao mkubwa unaocheza ili udondokee watu au magari mengine lazima raia wema pamoja na wewe mngetoa kipigo cha mbwa ili iwe fundisho kwa washenzi kama hao
ReplyDelete