Hali si shwari hivi sasa katika eneo la Bonde la Mkwajuni Kinondoni jijini Dar es salaam, na inaelezwa kuwa hali sio shwari kwani baadhi ya Wananchi wamechoma mataili pande zote za barabara na hakuna gari kupita. Jeshi la Polisi lipo eneo la tukio hivi sasa kukabiliana na tukio hilo ambalo chanzo chake unadaiwa ni baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa walikuwa wakazi wa eneo lililobomolewa ambao wameingia barabarani na kufanya fujo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. TUKIWARUHUSU HAO WAHUNI NCHI YETU ITAKUWA KAMA SOMALIA. WAMEVUNJA SHERIA HALAFU BADO WANAHARIBU MIUNDOMBINU YA BARABARA NA KUZUIA WANANCHI WASIO NA HATIA KWENDA KAZINI NA KUHARIBU SHUGHULI ZA BIASHARA. KWA HAO WAHUNI SIYO KUPELEKWA TU MAHAKAMANI BALI WANATAKIWA WACHUKULIWE HATUA KALI ILI IWE FUNZO KUTORUDIA UPUUZI HUU. POLISI JITAHIDINI KUONGEZA NGUVU NA KUZUIA UJINGA HUO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...