Naibu waziri wa Wizara ya Maji Mh
Juma Aweso, akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la Maonyesho la Baraza
la Kilimo Tanzania katika viwanja vya Maonyesho ya wakulima nanenane Kanda ya
Mashariki yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Baraza la Kilimo Tanzania kuhakikisha linawasaidia wakulima ili wapate taarifa sahihi kuhusu pembejeo hasa mbegu ili waweze kuzalisha kwa tija.
Mh Aweso amesema hayo Agosti 05 mwaka huu mara baada ya kutembelea Banda la Baraza la Kilimo Tanzania katika Maonyesho ya wakulima kanda ya Mashariki yanayofanyika viwanja vya Mwl Nyerere Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi wa zamani Omary Mahita akifurahia jambo na washiriki wa maonyesho ya wakulima ndani ya Banda la Baraza la Kilimo Tanzania, pia alipata fursa ya kupata maelezo ya kina juu ya bidhaa ya mchele ya Rukwa Super Rice inayozalishwa na wakulima hao bila kutumia mbolea za kisasa.
IGP wa zamani Omary Mahita afurahishwa na juhudi za Baraza la Kilimo Tanzania katika kuwawezesha wakulima wanawake, katika picha akiagana na mkulima wa korosho kutoka Mtwara ambaye yuko ndani ya Banda la Baraza la Kilimo.
Mratibu wa Programu ya Ubia wa KIlimo Tanzania chini ya Baraza la Kilimo Bw. Mark Magila akipata maelezo ya bidhaa zinazoonyeshwa na mshiriki wa maonyesho ya Kilimo mwaka 2019,ndani ya Banda la Baraza la Kilimo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...