KATIKA kuadhimisha siku ya wanawake duniani Wanawake na viongozi wa chuo cha Furahika Education wametembelea hospitali ya 'Anglican Health Centre' na kufanya usafi hospitalini hapo sambamba naa kukabidhi vitakasa mikono 'Sanitaizer' na sabuni vyenye thamani ya shilingi laki tatu na nusu.
Baadhi ya viongozi waliotembelea hospitali hiyo akiwemo Mkuu wa chuo cha Furahika Education College David Msuya amesema wanaunga juhudi na kutambua thamani ya wanawake katika nyanja zote za ujenzi wa taifa na wataendelea kuenzi mchango unaoonyeshwa na wanawake katika ngazi zote kuanzia katika familia.
Kwa upande wake mganga mkuu na Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk. Samwel Ayoub ameshukuru uongozi wa chuo hicho kwa kushiriki katika kufanya usafi na kutoa vifaa vya usafi hospitalini hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...