Na Khadija Seif, Michuzi TV

JAMII ya waumini wa Kiislamu dhehebu la Waismailia wa Shia wameadhimisha siku yao kwa kuhudumia jamii na kushiriki kuboresha mazingira kwa kupanda miti.

 Akizungumza mbele ya jamii hiyo ,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo ametumia maadhimisho hayo kueleza  inaonyesha wazi kuwa kuanza kwa mpango  mpya wa kulinda na Kutunza Mazingira na kutekelzwa na jamii ya Waismailia wa Shia .

"Nafarijika kuona jamii ya Waismailia ikiweka matamanio haya katika vitendo na kupitia mpango wa kiraia wa Wanaismailia (Ismaili civic) mnaweka nguvu kufanya shughuli za usafi wa mazingira,upandaji wa miti,na uelimishaji katika Mikoa ya Dar es salaam,Dodoma,Mbeya,Mwanza na Visiwani Zanzibar na vilevile Kitaifa," amesema Waziri Jafo aliyekuwa mgeni rasmi.

Pia amesema maatumaini yake kuwa programu hiyo itakua kukua na kuguswa maeneo zaidi ya umma nchini."Mapema mwaka huu ,ofisi ya Makamu wa Rais ilianzisha kampeni endelevu ya kushughulikia changamoto zinazokabili Usafi wa Mazingira nchini ."

Ametoa mwito kwa jamii zingine ziige  mfano huo hasa kwa watoto ili waweze kuwa katika dhamira ya kutunza Mazingira pamoja na kupanda miti huku akiwaomba Watanzania kulinda, kutunza na kuboresha mazingira ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Kwa upande wake Rais wa Baraza la Jamii ya Waismailia nchini Amin Lakhani ameeleza kwa namna gani jamii hiyo imekua na moyo na nia ya kujitolea  katika kushiriki kuboresha mazingira ndani ya jamii tunazoishi.

"Katika siku hii tunajikita zaidi katika kufanya kazi za jamii katika nchi husika na kuonyesha nguvu ya mpango huu ulimwengu kote na kwa Mwaka huu Maudhui yetu ni usimamizi wa utunzaji wa Mazingira,ambao utahusika ukarabati naa Usafi katika Maeneo ya umma ili kuweka Hali njema na endelevu," amesema.

Lakhani amesema kutokana na siku hiyo adhimu kwa Waismailia duniani na mahususi nchini,wamedhamiria kuboresha mazingira ikiwemo shule na masoko kwa kufanya usafi,Kupanda miti au kuweka bustani,kupaka rangi, ukarabati na shughuli nyingine za kijamii.

"Dhamira yetu ni kuona kuwa tunasaidia sio kwa nuda mfupi bali kwa kuweka uendelevu wa huduma kwa matokeo mazuri,"amesisitiza.

Waziri wa nchi, Muungano na Mazingira Selemani Jafo akishirika katika shughuli za upandaji Miti katika shule ya Muhimbili jijini Dar es salaam kama sehemu ya kuadhimisha siku ya jamii ya kiislamu ya Ismailia na kuwataka wananchi kutunza Mazingira hayo

 Sehemu ya Burudani ikitolewa na wanafunzi pamoja na walimu wao katika Maadhimisho ya siku ya jamii ya kiislamu ya Ismailia jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...