Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo yya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt.John Jingu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu, Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia kilichopo Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam.  Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu, Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia ambao umefanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii, (ISW) leo jijini Dar es Salaam.Kamishina wa Ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt.Nandera Mhando akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia ambao umefanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam.Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Judith Kimaro akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia ambao umefanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam.  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo yya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt.John Jingu (katikati) akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia ambao umefanyika leo Jijjini Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wakishiriki katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia uliofanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam.  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo yya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt.John Jingu (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la KOICA Tanzania, Kyucheol Eo wakizindua Kituo cha Elimu, Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia hafla ambayo imefanyika katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii leo Jijini Dar es Salaam.


KATIBU Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu leo Novemba 15, 2021 amezindua Kituo cha Elimu, ushauri na Msaada wa Kisaikolojia kilichopo chini ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Jingu amewaasa watumishi wa Kituo cha Elimu, ushauri na Msaada wa Kisaikolojia kuanza kutoa huduma kwa njia ya mtandao ili kuweza kufikia watu wengi zaidi na kupunguza msongamano pindi wateja wakatapo kuwa wengi.
 
Dkt. Jingu ameeleza jinsi kituo hicho kilivyo na uhitaji mkubwa katika jamii yetu kwani kuna matatizo mengi katika jamii yetu ikiwemo mafarakano ya ndoa, kifamilia, misongo ya mawazo kutokana na ukosefu wa vipato toshelezi, na ajira, kukata tamaa kutoka na magonjwa sugu,watoto wa mitaani, uraibu wa dawa za kulevya, masuala ya VVU na Ukimwi na matatizo mengi ambayo yanaikumba jamii yetu ya Watanzania.
 
Dkt. Jingu ameipongeza Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa siku zote kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wadau kutoa huduma za ushauri na msaada wa kisaikolojia pindi majanga yanapojitokeza akitolea mfano maafa ya Moto mjini Morogoro ambapo Taasisi ilikwenda kutoa msaada kwa wahanga wa ajali hiyo ya moto.

Dkt. Jingu ameuasa uongozi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kukitunza na kukiendeleza kituo cha hicho cha elimu, Ushauri na Msaada wa kisaikolojia ili kiendelee kuwa msaada kwa Jamii yetu.

Akitoa ufafanuzi kuhusu kituo hizo Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa jamii, DKt. Joyce Nyoni amesema kuwa Kituo ukarabati wa kituo hicho umegharimu kiasi cha zaidi shilingi milioni 34 kutoka ufafhili wa Koica.

Dkt. Joyce amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia ustawi wa Jamii hasa suala la malezi na makuzi ya watoto.

Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Ustawi wa Jamii imekuwa ikitoa kozi mbalimbali kulingana na mahitaji katika jamii kwa ngazi ya cheti hadi ngazi ya uzamili.

Amesema kuwa taasisi ilianza kutoa huduma za ushauri mwaka 2007 kupitia kituo wakati huo kikijulikana kama Counselling and Information Center

Amesema Kituo kilichozinfuliwa kitatoa huduma kwa jamii inayotuzunguka kwa faraha zaidi.

Amesema kuwa huduma zitakazo tolewa katika kituo hicho ni pamoja na kutoa ushauri juu ya masuala ya Ndoa, ushauri nasaha, uraibu wa madawa ya kulevya, masuala ya kisaikolojia na magonjwa yasioambukiza.

Dkt. Joyce amesema kuwa Kukamilika kwa kazi ya kukarabati kituo hicho kutaboresha mazingira ya utoaji huduma na kitarahisisha upatikanaji wa huduma.

Hata hivyo Amewashukuru KOICA kwa ukarabati wa kituo utakaopelekea urejeshwaji wa huduma katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

Amewahakikishua KOICA, kituo hicho kitakwenda kutumika na kuleta tija na matokeo chanya kwa jamii ya Watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...