Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mh. Jakaya Kiwete akimkabidhi tuzo Meneja Mauzo na Masoko ya Kampuni ya SGA Security, Faustina Shoo baada ya kampuni hiyo kuibuka kidedea miongoni mwa makampuni ya ndani yanayotoa huduma katika migodi mbalimbali nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa SGA Security wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionesha tuzo hiyo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya ulinzi ya SGA Tanzania Limited imeibuka mshindi wa tuzo ya mtoa huduma bora zaidi kwa mwaka 2021 katika sekta ya madini na kuyashinda makamupni mengine yanayotoa huduma hizo kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura ya 123.

SGA ilipokea Tuzo na Cheti cha ushindi wakati wa Tamasha la Usiku wa Madini lililoandaliwa na Wizara ya Madini lilofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, ulioko Jijini Dar es Salaam.

Tuzo ya mshindi bora ilitolewa kwa uongozi wa kampuni ya SGA na Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt Jakaya Kikwete.

Tuzo hii ya mwaka huu kwa washiriki wa ndani katika tasnia hii, ni muendelezo wa mafaniko ya utendaji bora unaofanywa na kampuni ya ulinzi ya SGA na ushindi huu unafuatia na tuzo nyingine tano za heshima ambazo ilizipata mwaka 2021.

Tuzo hizo ni pamoja na ile ya juu kabisa ya ubora wa ulinzi katika kitengo cha teknolojia ya usalama ya kielektroniki, ile ya watoa huduma za usalama zaidi katika sekta ya Madini kupitia Wizara ya Madini na taasisi ya Tantrade, tuzo ya mwaka kwa Kampuni ya Ulinzi inayotumiwa zaidi na wateja nchini Tanzania na Afrika Mashariki, tuzo ya taasisi inayopendelewa zaidi na wateja Afrika na Tuzo ya kiwango cha Platinum kama timu bora katika utendaji, ile ya Timu Bora ya Uaminifu ya Mwaka katika Afrika Mashariki na Kampuni Bora ya Usalama Afrika Mashariki na Tuzo ya chapa yenye Ubora kwa Afrika Mashariki.

Tamasha la Usiku wa Madini lilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya madini hapa nchini, ambapo lililenga kuhamasisha wadau wa sekta ya madini na pia kuipongeza serikali kwa mchango wake katika kuboresha sekta ya madini hapa nchini na pia pongezi za serikali kwa makampuni ya ndani na nje ya nchi ambayo yanatoa mchango mkubwa katika kukuza sekta ya madini hapa nchini.

Hafla hiyo pia ilipambwa na shughuli mbalimbali ikiwa ile ya maonyesho ya bidhaa zinazotokana na madini, mapambo, maonyesho, filamu kupitia video na pamoja na picha.

Dk. Kikwete amempongeza Waziri wa Madini – Dk Dotto Biteko kwa hatua yake ya kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ambayo yameongeza fursa za uwekezaji, ambapo alitoa ushauri kwa wizara hiyo kuongeza nguvu ili nchi iendelee kunufaika na raslimali zake za madini iliyojaliwa kuwa nazo.

Kwa mujibu wa Kanuni za Madini, makampuni yote yanayofanya kazi katika sekta ya madini yanatakiwa kuwasilisha Mpango wenye kuonyesha Maudhui na Utendaji wao wa Ndani kwa Tume ya Madini.

Tume ya Madini hupitia mawasilisho yote ili kuthibitisha uaminifu na uadilifu katika utendaji na kama yanakidhi wajibu wao katika kuhakikisha utekelezaji wa Mpango wa Maudhui ya Ndani kwa kuzingatia maelezo na matakwa ya Sheria ya Madini Sura ya 123 kuhusiana na Utendaji wa Maudhui ya Ndani.

SGA ilishinda katika kitengo cha Utendaji wa Maudhui ya Ndani, ambayo mahitaji yake ni pamoja na kampuni iwe imesajiliwa kufanya kazi hapa nchini na asilimia 20 ya umiliki wa hisa zake ziwe zinamilikiwa na Watanzania, ajira ilenge Watanzania kwa asilimia kubwa, aweko Mtanzania kwenye moja wapo ya nafasi za ngazi ya juu za uongozi, mpango mahsusi wa Watanzania kurithi watendaji wanaotoka nje ya nchi, ambapo kigezo kingine ni kuweko kwa programu nzuri katika kuchangia jamii kampuni inapofanyia kazi.

Ilikuwa ni vigezo vya kiushindani ambavyo pamoja na ushindani mkubwa uliokuweko SGA iliibuka kinara.

Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Mauzo na Masoko wa SGA, Bi. Faustina Shoo, amesema kuwa kampuni ya ulinzi ya SGA imepata heshima kubwa kupitia Tuzo hiyo adhimu ya Nafasi ya Kwanza katika utendaji kwa makampuni ya Ndani na kwamba pia ni heshima kubwa ambayo imepata kutoka Serikalini Kupitia Wizara ya Madini.

“Tuzo hii ni fursa nzuri na si kwa vile dhamira ya SGA katika kutii kikamilifu matakwa ya Udhibiti wa Serikali ikiwa ni pamoja na Kanuni ya Madini (Maudhui ya Ndani ya mwaka 2018), bali pia ni kutokana na mchango wake katika kusaidia usalama endelevu kwa wateja wetu na jamii yetu ya Watanzania kupitia hudma zetu bora zaidi na ubunifu wa wataalam wetu katika nyanja za usalama”, alisema.

Aliendelea kusema kuwa SGA inatoa mchango wake ndani ya jamii kwa kuajiri watu kutoka kwenye eneo inakofanya shughuli zake, kuchangia huduma za kijamii na pia kuchangia mapato ya serikali.

"Dhamira yetu inaunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuhakikisha kunakuweko na mazingira ya kiusalama hapa nchini yatakayowawezesha watu kuishi kwa amani huku wakifanya shughuli za mbalimbali zikiwemo za kibiashara kwa amani na utulivu”, alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...