*Dk.Mhede aahidi usimamizi wa mahiri kwa kupata mafanikio makubwa.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WAZIRIi wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-Tamisemi Angela Kairuki amesema kuwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) waendelee kudhibiti mifumo ya Mapato ya Kieletroniki ili kusiweze kuwa na uvujaji wa mapato hayo.
Kairuki ameyasema hayo wakati alipotembelea Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)Jijini Dar es Salaam , amesema kwa ziara hiyo ni ni kujifunza lakini kikubwa zaidi ni kutokana na mradi huo kuwa na umuhimu kwa uchumi wa nchi na mtu mmoja moja.
Amesema kuwa katika suala la kusimamia miundombinu kwa watu wanaokiuka kwa kutumia barabara za mabasi yaendayo haraka atashughulika nalo kwa kupeleka katika mamlaka za juu.
Aidha amesema kuwa DART waendelee kubuni vyanzo vya mapato ili kuendelea kuzalisha mapato kwa wingi na serikali kupata mapato hayo kwa ajili maendeleo.
Kairuki amewapongeza DART kwa kuweka mifumo imara ya ukolusanyaji mapato na kutaka kuendelea kufanya tathimini ya ukaguzi wa kila mara.
Kairuki amesema ametokea mtaani hivyo lazima afanye kazi watu wakimwangusha hataweza kukubali itokee hivyo.
"Nataka kazi ifanyike sina cha kupoteza hapa nimetokea mtaani hivyo kazi nitaifanya katika kuleta imani kwa mhe.Rais kuyafikia matarajio kuwepo Tamisemi" amesema Kairuki
Kwa Upande wa Mtendaji Mkuu wa DART Dk.Edwin Mhede amesema kuwa lengo ya DART ni kusafirisha abiria 450000 kutokana miradi ya ujenzi ya miundombinu itakapokamilika.
Dk.Mhede amesema kuwa mapato yanaongezeka kila mwaka kutokana na mipango na mikakati katika kupata fedha ambayo uaminifu wao kwa serikali
Amesema kuwa kuwa hakuna sababu kuwepo katika wakala huo kama uzalishaji unakuwa wa kusuasua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -Tamisemi)Angela Kairuki akizungumza na Wafanyakazi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) wakati alipofanya ziara katika Wakala huo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dk.Edwin Mhede akitoa maelezo kwa Waziri wa Tamisemi Angela Kairuki alipofanya ziara katika Ofiso za DART jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wakifatilia hotuba katika ziara ya Waziri wa Tamisemi alipotembelea DART Jijino Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...