
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Dk.Elirehema Doriye (kushoto) wakibadilishana hati ya Makubaliano na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani Asangye Bangu mara baada ya kusaini makubaliano Bima kwa maghala ya kurosho Jijini Dar es Salaam.
*Yaahidi kulipa madai yao ndani ya siku Nne kutokana na mifumo imara iliyowekwa
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) wamesaini mkataba wa makubaliano na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo nchini.
NIC kuingia makubaliano hayo kumetokana na kufanya utafiti na kuonekana wakulima wa zao korosho wanakula hasara kutokana na unyaufu hivyo bima inakwenda kufuta hasara hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye amesema wameamua kuingia makubaliano hayo ili kutatua changamoto katika ununuzi wa zao la korosho nchini kwa kuwa na bima katika maghala hali ambayo itaondoa changamoto hiyo ambayo imekuwa ikiishi kwa miaka mingi.
Amesema Bima hiyo itahusisha kulipa gharama za ajali ya moto zitakazokuwa zinatokea maghala ambapo awali wakulima na wafanyabiashara wa zao la korosha walikuwa wanapata changamoto kutokana na baadhi kutokuwa na bima ya mazao yao.
“Zao la korosho lilikuwa na changamoto kidogo, NIC kwa kutekeleza sera za serikali tumetafuta suluhisho ili ununuzi wa korosho usiwe na hasara au changamoto,”Amesema Dkt.Doriye.
Aidha Dkt.Doriye amesema NIC imepunguza siku za kulipa madai kutoka siku saba, hadi nne ikiwa ni sehemu ya kufanya maboresho katika kuwahudumia wananchi kazi hiyo inafanyika kwa mifumo iliyowekwa na shirika hilo
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu, amesema makubaliano hayo yataimarisha utendaji wa mfumo wa Stakabadhi za Ghala nchini kwa kuondoa kero ya malipo kwa wanunuzi baada ya kukosa mzigo kamili ghalani.
Pamoja na hayo ,Bw. Bangu amewataka wanunuzi wote nchini kuhakikisha hawafanyi uzembe wa makusudi wakitegemea kuna bima ambayo wamekata kwani wakifanya hivyo watajiondolea uaminifu.
Amesema baada ya kutolewa kwa bima hiyo bodi itafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara katika maghala na hata hivyo katika kipindi cha mwaka huu kampuni 20 zitaenda kunufaika na bima hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye akizungumza kuhusiana na makubaliano kati ya NIC na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani kwa zao korosho jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani Asangye Bangu akizungmza kuhusiana na Bima ya Zao la Korosho kwenye maghala itavyorahisisha wakulima salama na kilimo hicho , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Dk.Elirehema Doriye (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani, Asangye Bangu wakionesha hati za makubaliano mara baada ya kusaini makubaliano Bima kwa maghala ya kurosho Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...