· Airtel, UNICEF Kuunganisha Bure shule 3,000 na mtandao wa Airtel 4G.

· Ubia wa Airtel, UNICEF kuwezesha Wanafunzi,walimu kusoma BURE maktaba Mtandao ya mamlaka ya elimu

· Airtel, UNICEF yaungana na Serikali kutoa Elimu Bure kwa Sekondari kupitia Mtandao
 
TANGA, May 31, 2024. Airtel Tanzania leo imezindua rasmi mradi wa Airtel SmartWasomi utakaoendeshwa kwa muda wa mitano ukiwa na lengo la kuwezesha upatikanaji wa maudhui ya elimu kidijitali nchini kwa kuunganisha shule za sekondari za umma na mtandao wa kasi wa Airtel.

Katika Mradi huu Airtel wanashikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) ambapo utekelezaji wake utaunganisha shule za sekondari 3,000 na mtandao wa Airtel 4G kuwezesha upatikanaji bure wa maudhui ya kujifunza kidijitali kutoka maktaba mtandao ya mamlaka ya Elimu tanzania (TET).

Mpango wa Airtel SmartWASOMI, umekuwa na mafaniko katika awamu ya majaribio ambapo tayari imeshaunganisha shule 50 za sekondari zilizopo Zanzibar, Dodoma na Mbeya.

Pia mradi umefanikisha kutoa mafunzo ya walimu zaidi ya 2,000, na hivyo kuwafikia wanafunzi zaidi ya 55,000 wanaofundishwa na walimu hao. Mradi umeshafanya upembuzi wakujua hali ya upatikanaji wamtandao wa intaneti ya Airtel 4G kwa kwa shule 4,200 za Tanzania Bara na 500 za Zanzibar. Pia tumeondoa malipo ya bando ili kuwawezesha wanafunzi na walimu kusoma BURE bila malipo ya intaneti kwenye maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Shule Direct.

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi huo, Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema, “Uwiano wa sasa wa vitabu kwa mwanafunzi katika shule nyingi haukidhi viwango vilivyowekwa na Serikali.. Kujifunza kidijitali ndiyo njia ya haraka zaidi ya kuboresha matokeo ya kujifunza na kuandaa watoto wetu kwa ajili ya siku zijazo. Kwa hiyo serikali inaipongeza Airtel Tanzania na UNICEF kwa kuendeleza mpango kama vile Airtel SmartWASOMI ambao unasaidia juhudi za serikali zinazolenga kuongeza upatikanaji wa elimu ya kidijitali kwa watoto wetu.”

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda alieleza kuwa Airtel SMARTWASOMI sio tu itapunguza mgawanyiko wa kidijitali bali pia itafungua itaongeza tija wanafunzi wetu kuendelea kujifuna kupitia mtandao wa kasi ambao utatoa huduma bure kwa wanafunzi kupitia maudhui ya kidijitali kutoka makataba mtandao ya mamlaka ya Elimu.

“Mpango huu utasaidia kuongeza viwango vya ufaulu na ubora wa elimu kwani bila shaka utaimarisha vijana wetu kustawi kuwa na uzoefu zaidi katika ulimwengu huu wa kidijitali. Tunajivunia kuunga mkono jitihada hii na tunatazamia kushuhudia matokeo chanya katika elimu nchini Tanzania,” alisema.

Kwa Upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh alisema Airtel ilianza utekelezaji wa dhamira yake ya kusaidia elimu kidijitali tangu mwaka 2015 kwa kuzinduzia mradi wa VSOMO kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – hii ni aplikesheni ya simu janja inayowezesha upatikanaji wa kozi ya VETA bila kuwa na hitaji la kuhudhuria darasani.. Zaidi ya hayo, Airtel imekuwa na ushirikiano na DTBi kwa kuzindua maabara ya kidijitali inayowajengea vijana na wajasiliamali uwezo wa TEHAMA ili waweze kusimamia biashara zao kwa ufanisi kidijitali.

“Kupitia mradi wa Airtel SmartWasomi, tumekadiria kutumia takribani TZS128,262,608,000/- sawa na USD50,299,062 ndani ya miaka 5 ya utekelezaji. Lengo letu ni kuhakikisha tunatumia teknolojia ya mawasilaino katika kuwezesha na kutoa masuluhisho ya mambo mbalimbali katika jamii na hasa katika elimu nchini Tanzania.

Aliongeza: “Lengo letu ni kuziunganisha shule za sekondari 3,000 kuwa na intaneti ya Airtel ili wanafunzi waweze kusoma kidijitali ndani ya miaka mitano ijayo. Tutaanza kuunganisha shule 1000 na mtandao wa Airtel kwa mwaka wa huu , kisha kila shule ya sekondari iliyounganishwa itakuwa ikipata GB 1,200 kwa mwaka ili wanafunzi na walimu wetu kuweza kusoma kupitia maktaba ya mtandaoni ya TIE isiyo na viwango.

Kwa upande wake, Elke Wisch, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) alisema kuwa data zinaonyesha kuwa mamilioni ya watoto barani Afrika wanapata changamoto katika kupata nyenzo bora za kujifunzia kutokana na rasilimali chache, huku akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya UNICEF na Airtel ni muhimu katika kuboresha hali ya utoaji elimu kwa watoto kwa mafanikio makubwa, ." Alisema.

Kupitia taarifa ya pongezi kwa Tanzania juu ya uzinduzi wa mradi wa Airtel Smart Wasomi uliotumwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Africa, Sunil Taldar, alieleza kuwa mradi wa Airtel SMARTWASOMI unadhihirisha dhamira halisi ya Airtel katika kutatua changamoto ya matumizi ya huduma kidijitali kupitia njia hii ya kuwezesha kizazi kijacho cha Afrika.

“Tunaona fahari kwa kutoa fursa sawa za upatikanaji wa mafunzo ya kidijitali hususani kwa watoto ambao hawajafikiwa na huduma kama hizindani ya bara la Afrika.Tunaishukuru sana serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wao na tunaishukuru UNICEF kwa kuwa mshirika muhimu katika kutekeleza mpango huu maalum,” alisema.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...