WACHEZAJI wa gofu 24 wa kulipwa na chipukizi kati ya 68 walioshiriki mashindano ya Lina PG Tour wanatarajia kuendelea na raundi ya tatu ya michuano hiyo inayofanyika viwanja vya klabu ya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam, baada ya kupata alama za juu kuliko wenzao.
Shindano hilo ambalo limeandaliwa na familia ya Said Nkya kwa lengo la kumuenzi Mchezaji wa zamani timu ya Taifa ya wanawake ya gofu, Lina Nkya limeanza Julai 17 na linatarajiwa kumalizika Julai 20,2025.
Wachezaji waliofuzu kuendelea kwa upande wa wakulipwa ni Iddy Mzaki, Juma Said, Athumani Chiundu, Frank Mwinuka, Hassan Kadio, Nuru Mollel, Fadhil Nkya, Abdallah Yusuph, I. Wanyeche, B. Nyenza, Angel Eaton na E. Lembris.
Kwa upande wa wachezaji chipukizi waliofuzu ni Hawa Wanyeshe, Ally Isanzu, Enosh Wanyeche, Gabriel Abel, Salim Shariff, Cloud Mtavangu,N. Mwansasu, M. Nobert, Samwel Kileo, J. Mbunda, Julius Mwinzani, Likuli Juma, P. Emanuel na P. Bonzo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo, miongoni mwa waandaaji na waanzilishi wa mashindano hayo, Yasmin Chali alisema mashindano hayo yameanza kwa wachezaji wa kulipwa na chipukizi kucheza na kwamba Julai 19,2025 waliofanya vizuri katika kundi hilo wataendelea na michuano hadi Jumapili ili kupatikana washindi.
Alisema Wachezaji hao 24 ni wale waliocheza vizuri kuliko wote ambapo kwa upande wa wachezaji gofu wa kulipwa watakuwa 12 na chipukizi watakuwa 12 pia na kwamba kundi hilo litaendelea na raundi inayofuata hadi watakapopatikana washindi siku ya Jumapili Julai 20,2025.
Chali ambaye pia ni mtoto wa marehemu Lina Nkya alisema Julai 19 na 20, 2025 watacheza wachezaji wasindikizaji 82 wa michuano hiyo ambayo yanafanyika kwa ajili ya wachezaji wa kulipwa na chipukizi.
“Wachezaji hawa 82 wataanza kucheza kesho (leo) kwa ajili ya kusindikiza haya mashindano,kwenye idadi hiyo wapo wanawake, wazee, watoto hawa wote kwa sababu kiwango chao cha gofu hakipo juu sana hivyo kwa kucheza hivi wanaongeza kiwango chao hivyo baadae wanaweza katika kundi la chipukizi na hata kupanda na kuingia kwa wachezaji wa kulipwa,” alisema
Hata hivyo Chali alisema mashindano hayo yalianza kwa kumuenzi marehemu Lina na wanatamani yaendelee kuwa makubwa na yenye kuvutia lakini wamekuwa wakikwama kwa kukosa wadhamini.
“Tunafurahi watu wanavyofurahia mashindano haya lakini kuyaendesha ni gharama na kitu ambacho kinatusumbua bado hatujapata wadhamini mpaka sasa kutoka ndani ya nchi, tunapenda mashindano haya ya we makubwa zaidi ila tunakwama kwa kukosa wadhamini.
“Tunaomba mashirika mbalimbali na watu binafsi wajiyokeze kudhamini mashindano hayo ili iwe rahisi kwetu kuendelea kuyakuza na kukuza vipaji vya watu mbalimbali,” alisema Chali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...