Dar es Salaam, Oktoba 2025
TAASISI za elimu za Atlas Schools zimezindua rasmi maandalizi ya Atlas Day 2025, tukio linalotarajiwa kuvuta maelfu ya Watanzania na wageni wa kimataifa katika viwanja vya Atlas Schools Madale, Jijini Dar es Salaam, Oktoba14, 2025.

Atlas Day mwaka huu itajumuisha shughuli mbalimbali ikiwemo Atlas Schools Half Marathon, Mahafali ya 20 ya wanafunzi wa Nursery, Darasa la Saba na Kidato cha Nne, Maonyesho ya kazi za wanafunzi, pamoja na burudani kemkem.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Wakili Didas Kanyambo amesema mbio za mwaka huu zitakuwa na viwango vitatu vya umbali 21km, 10km na 5km zote zikianzia na kuishia katika viwanja vya shule hizo Madale.

“Lengo letu ni kuhamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira na kuenzi mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere. Ndiyo maana kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Protect Nature, Preserve the Future,’” alisema Mwenyekiti huyo.

Usajili wa washiriki unaendelea katika shule zote za Atlas na Mlimani City kuanzia Oktoba 10, kwa ada ya Tsh 35,000 kwa mtu mmoja, huku vikundi vya watu 20 au zaidi wakipata punguzo la asilimia 10 (Tsh 31,500). Washiriki wote watapewa vifaa vya mbio kama Fulana, Kitbag, Bib number, na Wristband, pamoja na huduma za maji, matunda, huduma ya kwanza na viburudisho maalum.

Kamati ya maandalizi imesisitiza kuwa usalama wa washiriki utaimarishwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, SGA Security, na Chama cha Riadha Tanzania (RT).

Zaidi ya 2000 wanariadha wanatarajiwa kushiriki, huku idadi ya wageni ikifikia zaidi ya 10,000.

Mbali na mbio, siku hiyo itapambwa na maonyesho ya kazi za wanafunzi, michezo ya watoto kama jumping castle, maigizo, na ngonjera, pamoja na muziki wa live band na DJs.

Atlas Schools pia itafanya mahafali ya 20, ambapo zaidi ya wanafunzi 700 watatunukiwa vyeti na medali kama kumbukumbu ya mafanikio yao.

Tukio hilo limepata uungwaji mkono kutoka kwa wadau mbalimbali akiwemo Mix by Yas, CRDB Bank, ASAS Dairies, Bonite Bottlers (Maji ya Kilimanjaro), 4JS Fitness Center, Miziki Sound, The Bambaz, na Kuambiana Investment.

“Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kutuunga mkono kwa miaka saba mfululizo katika Atlas Half Marathon na miaka 20 ya Atlas Day. Ushirikiano wao ndio unaoifanya Atlas kuwa sehemu ya kumbukumbu nzuri kwa wanafunzi, wazazi na jamii,” aliongeza Wakili Kanyambo

Atlas Day 2025 inatarajiwa kuwa tukio la kipekee litakalounganisha elimu, michezo, utunzaji wa mazingira na burudani, ikiwa ni kumbukumbu ya kipekee kwa kila mshiriki chini ya kaulimbiu inayohamasisha kizazi cha leo kulinda mustakabali wa kesho.






Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...