NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
BAADA ya wananchi kulalamika huduma zisizoridhisha katika usafiri wa Mwendokasi hasa kwa wasafiri wa njia ya Kimara, leo Oktoba 2,2025 Serikali imeongeza mabasi mapya na wananchi wameshukuru ujio wa mabasi hayo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya abiria wa Kivukoni wameipongeza Serikali kwa kuweza kusikia kilio Chao na kuruhusu mabasi mapya kuingia katika njia ya Kimara.

Alex Michael ambaye ni mtumiaji wa muda mrefu wa mabasi hayo amesema wamekuwa wakikaa muda mrefu vituoni kwa kukosa usafiri wa uhakika kwenye mabasi hayo hivyo kumfanya kutumia gharama kubwa kupanda usafiri mbadala ambao ni bodaboda.

"Baada ya kuanza kwa mradi huu karibu miaka 10, mwanzo huduma ilikuwa nzuri na ilikuwa inavutia sana, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda huduma inakuwa mbovu na mabasi mengi kuharibika". Amesema Michael

Nae Amina Ramadhani mkazi wa Kimara Baruti amesema Serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba mabasi hayo ambayo yameletwa katika njia hiyo yawe yakudumu na si baadae kuondolewa kwani inasemekana mabasi hayo ni kwaajili ya kutoa huduma kwa njia ya Mbagala-Gerezani.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...