Na Janeth Raphael - MichuziTv.
Serikali imesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda, biashara na taasisi za kifedha ili kuongeza uzalishaji, kuimarisha uchakataji wa mazao na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Msisitizo huo umetolewa leo Agosti 2, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, alipofanya ziara katika Viwanja vya Dk. John Samwel Malecela, Nzuguni, kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea katika Maonesho ya 33 ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane).
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Balozi Omar amesema maendeleo ya uchumi hayawezi kufikiwa kwa ufanisi ikiwa kila sekta itafanya kazi kwa kujitegemea, akieleza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya sekta hizo ni msingi wa kuongeza tija, kuvutia uwekezaji na kuinua kipato cha wananchi.
Amesema Serikali inalenga kuona uzalishaji unaongezeka sambamba na kuongeza thamani ya mazao kupitia uchakataji, huku taasisi za kifedha zikiendelea kuwezesha maeneo yenye kipaumbele ili kuharakisha maendeleo ya sekta za uzalishaji.
"Ni muhimu kuwa na mtazamo wa pamoja wa kukuza uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao kupitia uchakataji na kuhakikisha sekta zote zinashirikiana kwa manufaa ya wananchi na uchumi wa Taifa. Taasisi za kifedha zinapaswa kuendelea kuunga mkono maeneo ambayo Serikali imeyapa kipaumbele ili kuongeza kasi ya uwekezaji," amesema.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amesema Serikali inaendelea kufuatilia matumizi ya matrekta yaliyotolewa kwa wakulima ili kuhakikisha yanatumika katika maeneo yaliyokusudiwa na kuchangia kuongeza tija katika uzalishaji wa kilimo.
Aidha, amewapongeza wajasiriamali wanaozalisha bidhaa zenye ubora, huku akisisitiza umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi ili kuongeza ushindani wa bidhaa zinazozalishwa Tanzania.
Ameongeza kuwa pamoja na kuongeza uzalishaji, kuna haja ya kuwekeza zaidi katika utangazaji wa bidhaa, kuimarisha mifumo ya masoko na kuboresha mazingira ya biashara ili bidhaa za Kitanzania zipate nafasi kubwa katika masoko ya kikanda na kimataifa.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...