Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU) kimetangaza kufunguliwa kwa msimu mpya wa ununuzi wa zao la mbaazi utakaoanza katikati ya mwezi Agosti, huku kikieleza kuwa kimejipanga kuhakikisha uzalishaji unaongezeka na wakulima wanalipwa kwa wakati kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 2, 2026, katika Maonesho ya Kilimo Nanenane Kitaifa, Mjumbe wa Bodi ya TAMCU, Nurdin Raisi Chakilo, alisema chama hicho tayari kimefunga msimu wa zao la ufuta na sasa kinaelekeza nguvu katika maandalizi ya msimu wa mbaazi.
Alisema TAMCU imejipanga kuhakikisha mnyororo mzima wa mfumo wa stakabadhi za ghala unafanya kazi kwa ufanisi, huku ikiwahamasisha wakulima kukusanya mazao yao, kuyaandaa kwa ubora na kuyapeleka kwenye maghala ya mnada ili kupata soko na malipo kwa wakati.
Chakilo alisema chama hicho kinajivunia mafanikio ya mfumo huo kutokana na minada kufanyika kwa wakati na wakulima kulipwa kwa wakati, hali iliyoongeza uelewa na imani ya wakulima katika mfumo wa stakabadhi za ghala.
Aidha, alisema TAMCU imeongeza thamani ya mali zake kutoka shilingi bilioni 1.5 hadi kufikia shilingi bilioni 5, sambamba na kuanzisha mradi wa usafirishaji wa mazao na mizigo mchanganyiko unaotoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini kwa kutumia magari yenye uwezo wa kubeba tani 32 kwa kila safari.
Aliongeza kuwa chama hicho kimejipanga kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kupitia mpango wa kujenga kiwanda cha korosho wilayani Tunduru pamoja na jengo la utawala lenye ghorofa tano litakalokuwa na ukumbi wa watu zaidi ya 700, ofisi za TAMCU na maeneo ya kupangisha.
Chakilo alisema TAMCU, inayohudumia vyama vya msingi Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma pamoja na baadhi ya wakulima wa mkoa jirani wa Njombe kwa zao la korosho, kimeendelea kunufaika na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kupitia upatikanaji wa pembejeo za kilimo, hatua iliyochangia kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...