Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kupitia Chuo cha VETA Mkoa wa Mbeya ikishirikiana na Jeshi la Magereza mkoani Mbeya imeanza mchakato wa kutambua, kutathmini na kurasimisha ujuzi wa ufundi stadi kwa wafungwa 100 walioupata wakati wakitumikia vifungo.

Mchakato huo ulioanza tarehe 27 Agosti 2026 unafanywa kwa ushirikiano na Chuo cha Ufundi cha Jeshi la Magereza Ruanda, jijini Mbeya, na unatarajiwa kukamilika Septemba 15, 2026.

Akizungumza kuhusu mchakato huo, Meneja wa Kanda ya Kusini Magharibi, Shomari Chololo waombaji waliojitokeza ni wamegawanyika katika stadi Ufundi Umeme (8), Ufundi Bomba (10), Ufundi Seremala (15), Ufundi Uashi (41), Uungaji na Uundaji Vyuma (12), Ushonaji (11), Huduma za Ndani na Usafi pamoja na Utengenezaji wa Sabuni (3).

Kupitia mchakato huo, wafungwa watakaokidhi vigezo wanatarajiwa kupata vyeti vinavyothibitisha ujuzi wao, hatua inayolenga kuwawezesha kutumia ujuzi huo kwa tija, ikiwemo kujiajiri, kuajiriwa au kuanzisha shughuli za uzalishaji baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao

Mchakato huo ni sehemu ya jitihada za kutambua na kuthibitisha ujuzi unaopatikana kupitia mafunzo na uzoefu wa vitendo, ili wahusika waweze kuwa na uthibitisho rasmi wa uwezo wao wa kiufundi na kuutumia katika maisha yao baada ya kumaliza vifungo.

VETA huendesha programu ya Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo (RPL) ambapo mafundi hufanyiwa tathmini ya ujuzi wao, kubaini upungufu walio nao katika stadi husika, kisha kuandaliwa mafunzo ya muda mfupi kuziba upungufu na hatimaye kutunukiwa vyeti vya urasimishaji ujuzi wao.


















Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.




Benki ya NMB imejiunga kwa mara ya kwanza kuwa mdhamini wa Mbio za Mbuzi za mwaka 2026, zinazolenga kukusanya Sh milioni 200 kwa ajili ya kusaidia vijana 150 kujiunga na vyuo vikuu na mafunzo ya ufundi. Tukio hilo litafanyika Septemba 19 katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum wa benki ya NMB , Getrude Mallya, amesema uamuzi huo umetokana na uzoefu wa benki hiyo kama mshiriki wa tukio la mwaka jana pamoja na ulinganifu uliopo kati ya malengo ya Rotary na uwekezaji wa NMB katika elimu.

NMB hutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi kila mwaka kwa uwekezaji wa kijamii. Mwaka 2025, benki hiyo ilitoa madawati 6,365 kwa shule 124 nchini, hatua iliyonufaisha takribani wanafunzi 19,095.

Rais wa Rotary Club of Dar es Salaam Oysterbay, Paul Muhato, amesema Sh milioni 163 kati ya Sh milioni 167 zilizokusanywa mwaka jana zimesaidia wanafunzi 136, wakiwemo 100 waliojiunga na vyuo vikuu na 36 waliojiunga na mafunzo ya ufundi.








 

Mashabiki wa burudani za kasino mtandaoni wamepata burudani mpya ndani ya Meridianbet baada ya Vaso Psycho kuingia rasmi na kuleta upepo mwingine wa msisimko. Mchezo huu umebuniwa kwa mtindo wa kisasa unaokupa burudani, taharuki na nafasi ya kupata ushindi mkubwa. Tofauti na michezo inayokupa matukio yale yale kila raundi, Vaso Psycho huja na sapraizi zinazoweza kubadilisha kabisa mwenendo wa mchezo, jambo linaloufanya kuwa kivutio kwa wachezaji wanaopenda burudani yenye presha na ushindi.

Kinachofanya Vaso Psycho kuwa gumzo zaidi ni namna kila raundi inavyoweza kuandika simulizi yake. Unaweza kuanza ukiwa unacheza kawaida, lakini ghafla raundi ya bonasi ikaingia na kubadilisha kila kitu. Hapo ndipo presha inapopanda, macho yakabaki kwenye skrini na kila sekunde kuwa muhimu. Raundi za bonasi zimeongezwa ili kuleta ladha nyingine ya mchezo, huku wachezaji wakisubiri kuona kama bahati itageuka na kuwapa tukio kubwa la siku.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Lakini kama kuna kitu kinachowafanya mashabiki kuendelea kuutazama mchezo huu kwa hamu, ni vizidishi vinavyoweza kufika hadi mara 10,000 ya dau. Hii ina maana kwamba kila raundi huja na matarajio yake, huku nafasi ya kupata kizidishi kikubwa ikiifanya safari ya mchezo kuwa na msisimko zaidi. Hakuna anayejua raundi inayofuata italeta nini, na hiyo ndiyo ladha inayofanya Vaso Psycho kuwa mchezo wa kusubiriwa kwa hamu.

Mbali na mfumo wake wa kucheza, Vaso Psycho pia imekuja na muonekano wa kisasa pamoja na sauti zinazoongeza msisimko kila hatua. Kuanzia mwanzo wa raundi hadi kusubiri bonasi au kizidishi kikubwa, mchezo umejengwa kukuweka kwenye hali ya uangalifu. Ni aina ya burudani inayokufanya ufuatilie kila kinachoendelea kwenye skrini huku ukisubiri kuona kama raundi hiyo itakuwa ya kawaida au itageuka kuwa tukio la kukumbukwa.

Kwa mashabiki wanaotafuta burudani mpya ya kasino mtandaoni, Vaso Psycho sasa ipo Meridianbet tayari kwa kujaribiwa. Ingia Meridianbet, tafuta mchezo huo na ujionee mwenyewe ladha ya raundi zake, bonasi na vizidishi vinavyoweza kufika mara 10,000 ya dau.

 

Bayern Munich inaanza safari yake ya UEFA Champions League 2026/27 nyumbani dhidi ya Bodø/Glimt, katika mchezo utakaopigwa siku ya leo Alhamisi, Septemba 10, saa 22:00 usiku kwenye dimba la Allianz Arena.

Bayern inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na jukumu la kuanza kampeni yake kwa ushindi, hasa kutokana na ukubwa wa klabu hiyo na matarajio makubwa yaliyopo chini ya kocha Vincent Kompany. Ratiba rasmi ya Champions League inaonyesha kuwa huu ni mchezo wa kwanza wa Bayern katika hatua ya ligi.

Kwa upande wa Bayern, mchezo huu unakuja baada ya kuanza msimu kwa matokeo yenye mchanganyiko. Mabingwa hao wa Ujerumani walifungua Bundesliga kwa ushindi mkubwa wa 5-1 dhidi ya VfB Stuttgart, lakini baadaye wakashindwa kupata ushindi dhidi ya Schalke 04 baada ya kutoka sare ya 0-0. Hata hivyo, ushindi wa 4-1 dhidi ya Osnabrück katika DFB-Pokal unaonyesha kuwa kikosi cha Kompany bado kina uwezo mkubwa wa kuzalisha mabao na kutawala mchezo.

Bodø/Glimt, kwa upande mwingine, si timu ya kubezwa. Klabu hiyo ya Norway imefanya kazi kubwa hadi kufika hatua ya ligi baada ya kupita kwenye mchujo wa Champions League, ikishinda NEC Nijmegen kwa jumla ya mabao 6-1. Pia imeendelea kuwa na matokeo mazuri ndani ya ligi yake, jambo linaloonyesha kuwa inakuja Munich ikiwa na kujiamini. Changamoto kubwa kwake itakuwa kukabiliana na Bayern katika uwanja wao wa nyumbani, ambako kasi, presha na ubora wa wapinzani vinaweza kuwa tofauti kabisa na ilivyo kwenye ligi ya Norway.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kimbinu, Bayern inatarajiwa kutaka kumiliki mpira kwa muda mrefu, kusukuma safu yake ya ulinzi mbele na kutumia upana wa uwanja kuvunja mpangilio wa Bodø/Glimt. Hapa ndipo mchezo unaweza kuamuliwa, kwa sababu Bodø/Glimt inaweza kulazimika kucheza kwa nidhamu kubwa bila mpira na kutafuta nafasi za kushambulia kwa mipira ya haraka. Bayern pia inapaswa kuwa makini isije ikawa inashambulia kwa wingi na kuacha nafasi nyuma, kwa kuwa Bodø/Glimt tayari imeonyesha uwezo wa kufunga mabao kwenye safari yake ya kufuzu.

Kwa ujumla, Bayern Munich ndiyo inayobeba presha kubwa zaidi ya kushinda kutokana na kucheza nyumbani na kuwa na uzoefu mkubwa katika mashindano haya. Hata hivyo, Bodø/Glimt inaweza kuifanya mechi kuwa ngumu kutokana na namna wanavyocheza. Kwa Bayern, ushindi utakuwa mwanzo muhimu kuelekea hatua ya mtoano, wakati kwa Bodø/Glimt, kupata hata pointi moja Allianz Arena kutakuwa tamko kubwa kwamba haijafika Champions League kwa bahati.


SportPesa XUP turns every football lead into an early payout moment

SportPesa XUP turns every football lead into an early payout moment 

The new European football season has already brought its share of familiar chaos. Favorites can dominate the game, take the lead, and then lose control due to a late set piece or a swift counterattack. These dramatic turnarounds are what make football so captivating, but they also reveal the difference between strong moments during the game and the final result. SportPesa Tanzania addresses this tension with an early-payout option that settles bets before the final whistle.

SportPesa XUP gives football fans a different way to read a match because a lead can matter before the final whistle. Through 1UP, 2UP and 3UP markets, eligible selections can be settled early when the chosen team reaches the required goal advantage during the match. On XUp, the selected team can trigger an early payout by reaching the required lead before full time, depending on the market selected. 

A lead now carries meaning before the final whistle

A typical match-winner bet depends on the score at full time. The new early-payout football feature, however, recognizes an earlier turning point. In the 1UP market, your bet wins as soon as the supported team takes a one-goal lead. Even if a late equalizer changes the score, it does not undo a bet that is already settled.

Imagine a team leading 1-0 but conceding late to end the match 1-1. Normally, a win bet would lose because the game finished as a draw. But with the SportPesa 1UP, 2UP and 3UP option, your bet would have already won when that initial goal gave the team the lead. This key difference highlights the product’s value as it puts a clear worth on taking the lead itself.

“1UP, 2UP and 3UP make every lead more meaningful because fans do not only wait for the final whistle. When a selected team reaches the required goal margin, the market can settle early, which adds another layer of excitement to eligible football fixtures,” said SportPesa Tanzania Head of Marketing Tracy Humplick.

Why early-payout bets have different odds

The three levels reflect different expectations in a match. A one-goal lead triggers the 1UP market, whether the score is 1-0, 2-1, or 3-2. The next level, 2UP, requires a two-goal cushion, while 3UP demands a three-goal advantage. Each level poses a distinct question, can the team get ahead, establish firm control, or dominate the game with a commanding lead.

According to SportPesa 1UP early-payout, these bets often come with shorter odds than traditional full-time markets because reaching a lead is usually easier than maintaining it until the final whistle. Higher thresholds like 2UP and 3UP happen less frequently, so they typically offer bigger payouts than the 1UP option. Choosing the right one depends on anticipating how the match is likely to unfold, not just picking the favorite.

The launch meets a season defined by shifting momentum

Timing is everything. The Premier League, La Liga, Serie A, and Bundesliga regularly showcase matches that shift after substitutions, tactical tweaks, or a late surge of pressure. A strong favorite might score early but then face a fierce comeback, while another may need most of the game to break through. By focusing on the moment a team reaches a set lead, this new market captures the drama fans are already watching.

SportPesa offers this feature on selected match fixtures, with each available threshold clearly shown alongside the match on its platform. This keeps football at the heart of the experience and ties the platform to the lively debates that fill group chats, radio shows, and fan conversations every weekend, about who starts fast, who controls the game, and who stays vulnerable after taking the lead.

XUP on singlebets and multibets

Settlement works differently depending on the bet type. For a single bet, once the selected team reaches the required lead, that bet is settled immediately. In a multibet, the qualifying leg is marked as won, but the entire bet slip remains open until the other selections are decided. This means an early win in one match resolves only part of the overall bet, leaving the rest to play out.

This distinction mirrors how modern football fans watch the game. They follow multiple matches simultaneously, switch between live scores and broadcasts, and expect digital platforms to react quickly to on-pitch events. SportPesa adds valuable context, while the early-settlement feature turns a key moment in the game into a clear, decisive outcome on the platform.

Conclusion

SportPesa XUP gives football fans a more exciting way to follow selected matches by making every lead matter before the final whistle. With 1UP, 2UP and 3UP, eligible bets can settle when the chosen team reaches a one-goal, two-goal or three-goal advantage, adding more meaning to match momentum. For players using SportPesa, the key is to understand how each market works, check availability before placing a bet and enjoy the experience responsibly.

TCB Chief Executive Officer and Managing Director 
Adam Charles Mihayo



By Issa Michuzi


The Tanzania Commercial Bank (TCB) is again footing the bill for the annual gathering of board chairpersons and chief executives from public bodies, signing on as principal sponsor for the third year in a row.


The event, hosted by the Office of the Treasury Registrar, will take place in Arusha from 28 to 30 September.


TCB Chief Executive Officer and Managing Director Adam Charles Mihayo confirmed the support today, 9 September 2026, at a breakfast briefing with news editors at the Hyatt Kilimanjaro in Dar es Salaam. 


The bank, he said, is “honoured to participate in the important gathering and proud to serve as its principal sponsor for the third consecutive time.” 


He added, “We greatly appreciate the honour extended to us by the Office of the Treasury Registrar to participate in this important meeting.”


For Mihayo, the forum is no mere ceremony. Over three days, leaders from public institutions and corporations will swap experiences, audit their own performance, and hunt for workable ways to improve service delivery and deepen their contribution to national development.


He also pulled the media into that mission. 


When coverage is steady and clear, he said, Tanzanians can track the work of the Treasury Registrar and the bodies it oversees. “Better public understanding keeps those institutions moving toward greater transparency and accountability”, he added.


TCB’s lineage reaches back to 1925, when it opened as the Tanganyika Post Office Savings Bank. 


Today it is a full commercial bank, the government holding the majority stake, with other public institutions owning the rest. 


The bank offers retail, SME, corporate, treasury, and digital banking, and says its focus remains on innovative financial solutions and wider financial inclusion.


Renewing the sponsorship, the TCB chief adds, is one part of its broader promise to back efforts that strengthen public institutions and push Tanzania’s development agenda forward.


By Issa Michuzi

 More than 700 board chairpersons and chief executives from state institutions and corporations will gather in Arusha from 28 to 30 September to review their performance and strengthen their role in delivering Tanzania Development Vision 2050.

 

Acting Treasury Registrar Ms Lightness Mauki (pictured) outlined the agenda today, 9 September 2026, during a breakfast briefing with news editors at the Hyatt Kilimanjaro hotel in Dar es Salaam.

 

The briefing highlighted the growing role of public institutions in advancing national development and set the tone for the upcoming high-level forum.

 

She said the Arusha gathering will be guided by a theme centred on three priorities: high performance, inclusiveness and resilience.

 

The goal is to build public institutions capable of driving Vision 2050 while remaining responsive to changing circumstances.

 

Beyond translating the Vision into day-to-day action, Ms Mauki said the forum will give leaders under the Treasury Registrar’s oversight an opportunity to exchange lessons and make better use of existing experience.

 

She noted that the gathering is going to be more than a routine meeting, but a platform to align experience, resources, policy papers and government directives with faster and more efficient delivery.

 

Ms Mauki, who also serves as the Treasury Registrar’s Director of Planning, Research and Business Development, said government investment in the institutions has risen by 75 per cent in three years to Sh92 trillion.

 

Revenue performance has also improved, she said.

 

“In the financial year ending 2026, the entities remitted Sh1.307 trillion, up seven per cent from Sh1.208 trillion collected in the previous year,” she said.

 

She described the figure as the highest amount collected since the Office of the Treasury Registrar was established.

 

The Office of the Treasury Registrar of Tanzania was established on 13 November 1959 through Treasury Registrar Ordinance No. 35 of 1959 to acquire, hold and manage government investments. The legislation is now known as the Treasury Registrar (Powers and Functions) Act, Chapter 370.

 

“Numbers like these show that our institutions are ready to play their full part in Tanzania Development Vision 2050, whose implementation formally began in July,” she said.

 

“As leaders in government and public institutions, we have a duty to translate our responsibilities into practical action and deliver the expected results,” she said.

 

“I encourage Tanzanians to follow our activities and the discussions that will take place during the meeting of board chairpersons and chief executives,” she said.

 

“Above all, I invite everyone to join us in celebrating the achievements recorded so far, while renewing our commitment to discharging our responsibilities efficiently, patriotically and with dedication,” Ms Mauki said.


Na Karama Kenyunko Michuzi Tv


SHAHIDI wa tano wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, John Heche, ameieleza Mahakama namna matukio mbalimbali aliyodai kuyashuhudia katika chaguzi yalivyosababisha chama hicho kufikia msimamo wa “No Reforms, No Election” (Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi).

Heche, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, ametoa ushahidi huo leo Septemba 9, 2026, katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dustun Ndunguru.

Akijibu maswali ya Lissu, Heche amesema Desemba 2, 2024, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikaa na kujadili masuala mbalimbali yaliyohusu chaguzi, ikiwemo ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi, kuenguliwa kwa wagombea wa chama hicho na matukio ya mauaji yaliyohusishwa na chaguzi.

Heche amesema kutokana na hali hiyo, hususani uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 na chaguzi nyingine alizoshiriki na kuzishuhudia, chama hicho kiliona kuwa hazikuwa chaguzi za kawaida bali “uchafuzi”, jambo lililopelekea Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Mbowe, kufikia msimamo wa “No Reforms, No Election.”

Amesema mabadiliko yaliyokuwa yakihitajika yalihusisha marekebisho makubwa ya Katiba na sheria, pamoja na kuondoa madaraka makubwa ya Rais katika uundaji wa Tume ya Uchaguzi na uteuzi wa watendaji wa uchaguzi.

“Kamati Kuu iliazimia mabadiliko makubwa ya kikatiba na ya kisheria,” amesema Heche.

Amedai chama hicho kilitaka Tume Huru ya Uchaguzi ambayo ingekuwa huru na isiyo na upendeleo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine.

Heche amesema Aprili 3, 2025, CHADEMA ilikutana na watia nia waliokuwa wakitarajia kugombea kupitia chama hicho katika makao makuu ya chama, Mikocheni, Dar es Salaam, na kuwaeleza sababu za kuendelea na msimamo wa “No Reforms, No Election” uliokuwa umechukuliwa tangu Desemba 2024.

Akieleza matukio aliyodai kuyashuhudia katika chaguzi mbalimbali, Heche amesema ameshiriki chaguzi akiwa mgombea na kiongozi wa chama, ikiwemo uchaguzi wa Arumeru, Busanda, Igunga, Kinondoni pamoja na chaguzi za mwaka 2015 na 2020.

Amedai chaguzi hizo ziliambatana na matukio mbalimbali, ikiwemo mauaji ya wanachama, kuenguliwa kwa wagombea wa CHADEMA, kunyimwa fomu za viapo vya mawakala, mawakala kuondolewa vituoni wakati zoezi likiendelea, polisi kupiga watu na kuvuruga mikutano ya kampeni ya chama hicho.

Amedai pia kuwa wagombea wa chama hicho walinyimwa fomu za matokeo, huku akidai kulikuwa na kura za uongo kuingizwa na baadhi ya watu kubeba vibegi vya kura feki.

Akijibu maswali ya Lissu kuhusu matukio ya mauaji aliyoyakumbuka katika chaguzi hizo, Heche ameeleza tukio la uchaguzi wa mwaka 2015 katika Jimbo la Busanda, ambapo amesema kiongozi wa CHADEMA na mgombea wa ubunge, Alphonce Mawazo, aliuawa.

Amesema Mawazo alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita na Mjumbe wa Baraza Kuu la chama hicho.

Alipoulizwa kama kuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika na mauaji ya Mawazo, Heche amesema hakumbuki vizuri mwisho wa kesi hiyo hivyo hawezi kueleza kwa usahihi.

Katika tukio lingine, Heche amesema wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020, alipokuwa akifunga kampeni Nyamongo, Kata ya Matongo, alivamiwa na kushambuliwa kwa risasi, ambapo watu wawili waliuawa na wengine kujeruhiwa.

Lissu pia amemuuliza Heche kuhusu tukio jingine la mauaji katika jimbo lake.

Heche amesema polisi walimuua mdogo wake, Suguta Heche, ambaye alidai alikuwa amefungwa pingu mikono yote na kuchomwa kisu.

Alipoulizwa kuhusu hatua zilizochukuliwa, Heche amesema Kamanda wa Polisi wa wakati huo alitoa taarifa kuthibitisha kuwa Suguta aliuawa na polisi na kwamba hatua zingechukuliwa dhidi ya waliohusika.

Hata hivyo, amesema polisi huyo aliachiwa na mpaka sasa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi.

Ushahidi huo umetolewa wakati Heche akiendelea kujibu maswali ya Lissu katika hatua ya utetezi wa kesi hiyo.

Shauri hilo limeahirishwa hadi kesho, ambapo Heche ataendelea kutoa ushahidi wake, huku Majaji wakitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu mashahidi wengine waliowekewa pingamizi.

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba nchini TMDA imefanikiwa kunasa shehena mbili kubwa za dawa na vifaa tiba zisizo sajiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA Terminal 3. Thamani ya jumla ya mizigo hiyo inakadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 360.Akizungumza na vyombo vya habari leo, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo amesema shehena ya kwanza ilikamatwa tarehe 7 Septemba 2026 wakati wakaguzi wao wakifanya ukaguzi wa kawaida kupitia mfumo wao wa udhibiti.


"Wakaguzi wetu wamefanikiwa kukamata mabegi 20 yaliyokuja kutoka India. Yalikuwa na dawa nyingi sana zenye thamani ya shilingi milioni 310. Hapakuwa na nguo wala vyakula. Tatizo kubwa ni kwamba dawa hizo zote hazikuwa na usajili wala vibali vyovyote vya TMDA," amesema Dkt. Fimbo.
Dkt. Fimbo ameongeza kuwa tarehe 9 Septemba 2026, wamefanikiwa tena kunasa shehena nyingine yenye thamani ya shilingi milioni 50. Ndani ya shehena hiyo kulikuwa na sindano za lignocaine, bupivacaine, adrenaline na vitamini.

Pia kulikuwa na dawa za kutibu magonjwa ya saratani, kifafa, shinikizo la damu na kisukari. Miongoni mwa dawa hizo ni OZEMPIC na GLP-1 ambazo ni sindano maarufu sasa hivi mitandaoni zinazotumika kupunguza unene. Shehena hiyo pia ilikuwa na vifaa tiba vya meno bandia.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, dawa zisizosajiliwa ni hatari kubwa kwa afya ya wananchi kwani ubora, usalama na ufanisi wake haujathibitishwa na TMDA. Matumizi yake yanaweza kusababisha madhara kama kuchelewa kupona, usugu wa dawa, ulemavu na hata vifo.

Dkt. Fimbo amebainisha kuwa mpaka sasa watu watano wameshakamatwa na vyombo vya usalama na bado wanaendelea na uchunguzi zaidi. Amesisitiza kuwa dawa zote zilizokamatwa zitaenda kuteketezwa mara tu uchunguzi utakapokamilika.

TMDA imetoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuzingatia sheria na taratibu za uingizaji na usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini. Amesema ni marufuku kuingiza bidhaa za tiba bila kupata kibali cha TMDA na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote.




 

Dar es Salaam, Septemba 8, 2026  

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kimeanzisha programu mbili mpya za Shahada katika Kampasi ya Tabora na kuongeza programu ya Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Kampasi ya Dar es Salaam kwa Mwaka wa Masomo 2026/2027.

Kampasi ya Tabora imeanza kutoa Shahada ya Usimamizi wa Kumbukumbu, Nyaraka na Taarifa (Bachelor Degree in Records, Archives and Information Management) pamoja na Shahada ya Uhazili na Utawala (Bachelor Degree in Secretarial Duties and Administration). Hatua hiyo inaifanya Kampasi ya Tabora kuanza kutoa elimu ya ngazi ya Shahada katika maeneo hayo kwa mwaka huu wa masomo.

Kwa upande wa Dar es Salaam, TPSC imeongeza Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (Bachelor Degree in Human Resource Management) katika programu zinazotolewa na Kampasi hiyo. Programu hiyo inalenga eneo la usimamizi wa rasilimali watu, ambalo ni miongoni mwa maeneo muhimu katika uendeshaji wa taasisi za umma na binafsi.

Kwa mujibu wa TPSC, mabadiliko hayo yanaendana na jukumu la Chuo la kutoa elimu na mafunzo yanayokidhi mahitaji ya Utumishi wa Umma pamoja na mabadiliko ya mazingira ya kazi na mahitaji ya wataalamu katika taasisi mbalimbali.

Akizungumzia kuanzishwa kwa programu hizo, Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Chuo kuongeza programu za elimu ya juu katika maeneo yanayohusiana na mahitaji ya kitaaluma na kiutendaji.

“Kuanzishwa kwa programu hizi za Shahada ni hatua muhimu katika juhudi za TPSC za kupanua fursa za elimu ya juu kwa Watanzania. Tunataka kuhakikisha kwamba wananchi wanapata fursa ya kujenga taaluma katika maeneo ambayo ni muhimu kwa ufanisi wa taasisi na maendeleo ya Utumishi wa Umma,” amesema Dkt. Mabonesho.

Kuongezeka kwa programu hizo kunatoa nafasi kwa wanafunzi na watumishi wanaotaka kuendeleza elimu yao katika fani za usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa kumbukumbu na taarifa, pamoja na uhazili na utawala.

Hatua hiyo pia inaongeza idadi na mchanganuo wa programu za elimu ya juu zinazotolewa na TPSC katika kampasi zake, huku ikizingatia maeneo ya kitaaluma yanayohusiana moja kwa moja na utendaji wa taasisi na utoaji wa huduma.

Programu hizo zinapatikana katika Mwaka wa Masomo 2026/2027, ambapo TPSC inaendelea na mchakato wa udahili kwa waombaji wanaokidhi vigezo vilivyowekwa.

 







DODOMA, TANZANIA — September 8, 2026.

Day One of the Bootcamp at Msalato Girls Secondary School in Dodoma began with the girls taking an active role in the learning process.

Working in groups, the students engaged in discussions, sharing ideas and exploring different challenges that could be addressed through technology.

The discussions gave the girls an opportunity to work together, listen to different perspectives and develop ideas as a team.

After the group discussions, the students came together for presentations.

Standing before the whole class, the groups presented the ideas they had developed during their discussions, giving each student an opportunity to participate and share what her group had explored.

Through this process, the girls were beginning to build important skills in teamwork, communication, confidence and problem-solving.

It was the first practical step of the Bootcamp—moving from discussion to presentation, and creating a foundation for the hands-on technology sessions that followed.

Day One had begun with an important lesson: ideas become more powerful when they are shared, challenged and developed together.

Na Mwandishi wetu, Mirerani

MWENYEKITI wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara, (MAREMA) Elisha Nelson Mnyawi amewaasa wanasiasa wenye agenda nyepesi kuwaacha wachimbaji madini wafanye kazi zao na kutowachafua kuwa wanatorosha madini.

Mwenyekiti huyo wa MAREMA Elisha ameeleza hayo katika mkutano wa wachimbaji madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani, wakati wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Elisha amesema wachimbaji wasiwakubali kamwe wanasiasa wenye agenda nyepesi za kuwachafua kwani wengine wapo kwa ajili ya kuangalia maslahi yao pekee.

Amesema wachimbaji hawataki vikwazo wanataka wafanye kazi kwa saa 24 kila siku ili wapate madini kwani hivi sasa madini ya Tanzanite hayapatikani kwa wingi ila baadhi ya wanasiasa wanawakwamisha.

"Wachimbaji wanaposemwa vibaya naumia mno, tunapokuchagua kiongozi utuongoze siyo fimbo ya kutuchapia, agenda za kutuchafua wachimbaji tusikubali kamwe," amesema Elisha.

Amewaasa wachimbaji madini wawe wanachuja wanasiasa wakuchaguliwa pindi wakati ukifika kwenye uchaguzi ili wasiachiwe bomu.

""Tunapozungumzia uchumi wa Mirerani wasilete utani au kuwasingizia uongo wachimbaji na mwanasiasa mwenye agenda nyepesi atupishe, tuwe tunawauliza kwanza unatoka wapi, tumjue balozi wake," amesema Elisha.

Katibu mkuu wa MAREMA, Tariq Kibwe amesema kiwa wao wachimbaji siyo wanasiasa na wanajibana na kujinyima katika kuchimba madini ili wafanikiwe.

Kibwe amesema wachimbaji wapo sambamba na Mwenyekiti wa MAREMA Elisha katika kuwasemea na kuwatetea kwenye changamoto zao zinazowakabili.

"Baadhi ya wanasiasa wanatulalamikia kuwa wachimbaji tunawachangia viongozi wa juu, jamani wanapaswa kuelewa sisi hatukuchangia mtu tulichangia chama," amesema Kibwe.


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameitaka Afrika kujenga uwezo wake wa ndani wa kugharamia, kusimamia na kuzalisha mahitaji muhimu ya huduma za afya, badala ya kutegemea misaada na mifumo ya nje kwa muda mrefu.

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumatano Septemba 09, 2026, wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Huduma za Afya ya Msingi unaofanyika jijini Arusha, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2,700 kutoka mataifa 27.

Amesema Afrika inapaswa kubadili namna inavyoelewa na kutekeleza dhana ya kujenga uwezo, akisisitiza kuwa haipaswi kuishia katika miradi midogo isiyojenga uwezo wa kudumu, bali iwekeze katika uzalishaji wa dawa, vifaa tiba, teknolojia na wataalamu.

“Enzi zile nikiwa Waziri wa Fedha nilikuwa nawaambia nchi za Afrika zimeshashuhudia muda mrefu sasa wa maisha ya misaada na misaada inayoelekezwa pengine katika maeneo ambayo yanatofautiana na malengo ya ndani ya nchi kwa jina la capacity building. Capacity building. Capacity building. Na ndio tunaishia chapati, mandazi, sambusa. Hatuwekezi kitu kitakachodumu na kikawa endelevu.”

Dkt. Mwigulu amesema malengo ya ndani ya nchi yanayokwenda sambamba na malengo ya maendeleo endelevu yanapaswa kuheshimiwa na washirika wa maendeleo, ili misaada na uwekezaji viweze kuacha matokeo ya kudumu katika maisha ya Waafrika.

Amesema Tanzania inaendelea kuweka nguvu katika kuimarisha huduma za afya, ikiwemo kuongeza miundombinu, rasilimali watu na utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, ambayo Serikali imeanza kutekeleza mwaka 2026.

“Tunapozungumza kuhusu afya ya msingi, tusizungumzie tu kujenga vituo vya afya. Tujenge pia uwezo wa nchi zetu kugharamia huduma hizo, kuzalisha mahitaji yake na kutumia teknolojia zetu wenyewe,” amesema.

Aidha, amesema Tanzania imeanza kuwekeza katika uwezo wa ndani wa uzalishaji wa dawa ili kupunguza utegemezi wa misaada na kuhakikisha upatikanaji wa dawa unaendelea kuwa wa uhakika hata wakati dunia inapokumbwa na changamoto zinazoathiri minyororo ya usambazaji.

Amesema Serikali pia itaendelea kuboresha mazingira ya watumishi wa afya, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za watumishi na kuongeza ajira katika sekta hiyo.

Dkt. Mwigulu amesema mkutano huo unapaswa kuzaa hatua mahsusi zinazoweza kutekelezwa na kupimwa, badala ya kuishia katika mijadala na maazimio.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), Dkt. Jean Kaseya, amesema Afrika ya mwaka 2026 si Afrika ya mwaka 1960 na kwamba wakati umefika kwa washirika wa maendeleo kubadili namna wanavyoshirikiana na serikali za Afrika.

Dkt. Kaseya amesema serikali za Afrika zinapaswa kuwa na umiliki na uelewa wa rasilimali zinazotolewa kwa ajili ya afya, huku fedha za washirika zikiendana na mipango ya kitaifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa WHO, Profesa Mohammed Janabi, amesema changamoto kubwa si kukosa suluhisho, bali ni kukosa ujasiri wa kuyafadhili, nidhamu ya kuyatekeleza na uwajibikaji wa kuyadumisha.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, amesema Serikali itaendelea kuongeza uwekezaji katika afya ya msingi kwa kuwa ndiyo ngazi inayohudumia wananchi wengi zaidi.

Amesema asilimia 95.6 ya wajawazito wanaojifungua nchini wanapata huduma katika ngazi ya afya ya msingi, huku asilimia 86 ya mahudhurio ya wagonjwa wa nje katika vituo vya umma yakihudumiwa katika ngazi hiyo.

Profesa Shemdoe amesema kati ya vituo 8,288 vya afya vinavyomilikiwa na Serikali, vituo 7,946 sawa na asilimia 95.8 ni vya ngazi ya afya ya msingi, hivyo uwekezaji katika ngazi hiyo ni uwekezaji wa moja kwa moja kwa wananchi wengi.

Mkutano huo wa siku tatu unajadili namna ya kuimarisha huduma za afya ya msingi kuelekea upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, kupitia ufadhili endelevu, ufanisi, ubora wa huduma, ubunifu, ushirikiano wa kikanda na kujenga mifumo ya afya inayostahimili majanga.