
Ni ajabu na kweli. kuna kuku hapa tz wanaolea bata. ukiwa dar tembelea bamboo bar, kinondoni kwa John Fedha, utajionea. kwa mujibu wa uchunguzi wangu, jirani ya bar hiyo kuna jamaa anafuga kuku na bata. huwa anachukua mayai ya kuku na kuyaweka kwenye kiota cha bata ambaye anayaatamia hadi kutotoa. ujanja utumikao ni kwamba kwa vile uatamiaji wa kuku huchukua siku takriban 14, wakati bata ni siku kati ya 29 na 40, jamaa hukadiria muda wa mayai ya bata na kuyaweka chini ya kuku ambaye, baada ya kutotoa, hujua ni vifaranga vyake. na huvilea kama vitoto vyake, na ni mkali kama kawaida ukivisogelea. ni sayansi nyepesi lakini yenye kuhitaji ubongo na uvumilivu.









