Hawa ni wanagu alihassan (kushoto) na Marenga. Nyuma yao ni mkokoteni wangu ambao unaonesha jina la kijikampuni changu na tujikazi nifanywato, na kuniwezesha kuwapeleka ali na marenga shule nzuri n.k. Kilonzo sura hizi si ngeni, tsj 1996 alumni (hahahahaha). yote tisa, nawauliza enyi muishio ughaibuni, kwa nini hamrejei hom huku bongo mambo poa, ni bongo lako tu. unaambiwa sasa tuna mabenki 27 na yanapiga hodi hadi manzese kutafuta watu wa kukopesha. hivi hamuoni noma kuolomea huko ugenini wakati nchi yawahitaji. Mti Mkubwa (mkavu?) upo? hata nyie kina mwaipopo, ida nkya, ndesanjo macha, eggidio (bubu umekuwa?), mwaipopo, semkae na wengine wote mnaosoma ujumbe huu. RUDINI NYUMBANIIIIIIIII!!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. kaka michuzi,

    hongera sana maana kama mzazi ninaelewa jinsi gani mtoto anapokuwa na afya njema na hivyo tena unajitahidi kumpiga na pamba za kung'aa inapendeza namna huyo!

    nyumbani tutarudi tu mbona tunawaza siku ya kurudi? na huyu kikwete alivyoongea juzi bungeni ananipa matumaini hayo...maana kama tutasaidiana kujenga taifa na kila mtu ataheshimiwa kwa mchango wake nadhani ipo hiyo haja!

    nilisikiliza hotuba yake juzi, naona amesikia kilio chetu. ataunda wizara ya kushughulikia uraia na hakiza raia. bado hajajua kama ataiweka kwenye ofisi kati ya kwake au ya makamu. sasa basi na makamishna wenyewe ndio tumejaa humu glubuni! tutamsaidia tuu!

    amenipa sana matumaini juzi kwenye hotuba ya uzinduzi wa bunge! nikipata muda nitaichambua hotuba yake....

    ndio maana nina wasiwasi kuwa kiwete naye anablogu!

    cheers

    ReplyDelete
  2. pia hongera sana kwani ni kweli kuwa mazingira ya nyumbani hasa haya ambayo unafanyia kazi bado hayajakaa vizuri! lakini jitihada zako za dhati zinaonekana. ubunifu na jitihada katika kazi! mtu kama wewe sasa unastahili kubebwa! tuombe mungu!

    cheers

    ReplyDelete
  3. Egidio yuko Moshi. Ni mwanafunzi wa chuo cha ushirika, Hayuko Ughaibuni. Na watu kama akina Nkya wanajichukulia shahada zao za udakitari sidhani kama kuna sababu za kurudi na kuacha elimu ufunguo wa maisha. Mimi nitarudi siku Mrema akiwa rais!!! (natania jamani).

    ReplyDelete
  4. Michuzi,
    Huku tulipo ni kama msituni.Tunapanga mikakati ya jinsi ya kurudi nyumbani japo na mkate na siagi kama tunaenda Kilwa kusalimia wazee!

    ReplyDelete
  5. Tunarudi mazeeeeee.... Tena aisee hongera naona kweli TSJ alumni ilisaidia sana. That was the best choice tulifanya maishani. Ona sasa watoto wanavyopendeza. Mambo ya product za milimani. Kitu na box.

    Sasa leaving lugha ya kimtaani aside, inabidi kweli tuwe serious. Hiyo photopoint inabidi mi uniajiri kama manager halafu wewe uzingatie shughuli zingine. Then mimi niende nikawaone hao jamaa wa mabenki huko Manzese ilituweze kupata mkopo wa mashine ya kuprintia T-shirt in time for 2010 general elections.

    ReplyDelete
  6. wote mmenena lakini kwa haraka haraka baragumu kasema. ila kasahau kwamba mtaalamu kama yeye ndiye chachu za kuleta maendeleo ambayo kwayo undugu na rushwa hutindia. huko watu wamesahau sababu wametumia taaluma zao KWAO pamoja na mali kibao walizopora kwetu na kujikuta wameendelea. mnaonaje nanyi mpore mali (hasa taaluma) na kuleta huku kuliko kusubiri tuwachagulie Mrema awe rais ndio mjilete. semkae nimesema manzese kuna watu si mabenki, mabenki bado yako mjini. ila jamaa hufuata watu kuhamasisha wakope. kuhusu ajira photo point ni ngumu kwa raia wa nje. hivyo samahani... sina uwezo kulipia weking pamit yako (hahaha!) na ifikapo 2010 si t-shirt tena bali ni pin-stripped suits za majina ya wagombea. siku hizi t-shirt zinatengenezwa magomeni mapipa na kariakoo na vijana wa kawaida tu, tena kwaliti. nipe address nikuletee moja ya kikwete ambayo photopoint tumetengeneza, mali ghafi toka kiwanda cha arusha

    ReplyDelete
  7. kaka michuzi,

    sawa lakini nikija huko nikifanya kazi yangu kinapofika suala la malipo si nasikia wanasema iwe ni wito? je wao za kwao inapofika kwenye malipo wanalipwa kwa wito? wakati za kwao sio za wito? maana inaonekana hapo bongo ukitaka kuwa vizuri ni lazima uwe mwanasiasa/mbunge! na wengine mpaka tupate hela ya kugharamia kampeni ikibidi dhidi ya chama kubwa si mchezo! - ila kama alivyosema semkae, T shirt za 2010 hamuna kuchapishia nje ya nchi!

    ReplyDelete
  8. Ndesanjo bora umenitetea!
    Bwana Michuzi mimi nipo Bongo hii!.Kweli, nipo Ushirika... lakini sasa hivi hiki ni chuo Kikuu jamani, Kile Chuo cha ushirika sasa hivi hakipo tena(Ndesanjo una siku sana nyingi ujarudi nyumbani).Sasa Kinaitwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Stadi za Biashara(MUCCoBS)

    ReplyDelete
  9. Moshi University College of Co-operative and Business Studies (MUCCOBS), came into being as a result of upgrading the status of the former Co-operative College Moshi into a constituent University College of Sokoine University of Agriculture. The University College is established under the Declaration Order No. 22 of 2004 as a semi-autonomous organization with its own Governing Board.

    ReplyDelete
  10. mark uko nje ya alama kabisa. wito siku hizi ni neno geni, na si lazima uwe mwanasiasa upate tenda. we rudi uone. mie nimekataa kazi reuters (fleet street, london) kwa nini? sawa, dau lao kubwa lakini mie napata mara nne yake hapa hapa bongo. Upo hapo? jamani, muwe mnarudi rudi siku moja moja. siku hizi wakenya, waganda, warundi, wakongo, wanamibia, warundi, wazambia wanaifanya bongo kuwa dubai yao. hakuna anayekwenda uae tena! na uliza basi wabongo twaenda wapi - chiiiiiinnaaaaa. vitu kibao bei chee. si unajua tena saa za kilo (hahahaha!!!)

    ReplyDelete
  11. duh nakupata sasa inaelekea inabidi kufanya utafiti maeneo na maeneo. maana sasa juzi ninashangaa eti hawa madaktari wanalipwa hata laki mbili haifiki, wakafanya madai, waziri kayapinda pinda halafu wakawafukuza na wananchi wakaiunga mkono serekali bila kujua waathirika ni wenyewe. kwani daktari akipata milioni na nusu kuna tatizo gani? si ndio photogenic kungekua mara 100?

    tunashukuru kwa feedback hiyo kuhusu nyumbani. ni kweli kuwa kuna watanzania wengi ambao waliiba hela nyingi sana tangu enzi za mwalimu ukiacha huyu mheshimiwa wa mufindi wakatoroshea nje ya nchi. kama utaweza kuwa karibu na kikwete mwambie awabembeleze wazirudishe hapo ndani tu uchumi utaibuka kidedea. sisi huku tunaiba utaalamu tu. ni wanyonge wenzio.

    sielewi vyema hii concept ya bongo kugeuka dubai. ninachojua ni kwamba kutokana na uwezo wa watanzania kupurchase (kunununua) kuwa mdogo - maana hata waganda wametupita, bidhaa zikiletwa hapo zinauzwa kwa bei ya kubangaiza ili watu waweze nunua. nitatoa mfano wa biashara za hapo. mfano, hapa afrika kusini mtu akienda kukata nywele tena upara itamgarimu shilingi 3000. kwa hiyo mtu hata akikata vichwa 6 siku imetengemaa -japo hukata vingi tuu. na unakuta ikifika saa 10 mtu anaenda kupumzika. tofauti na hapo, bongo kichwa kimoja ni 300. inabidi apate vichwa 60 ili afanane na vichwa 6 vya huku. baada ya hapo kufunga kona ni saa 6 usiku ili aweze kumudu maisha (ushahidi ni daladala za mbagala zinajaa watu mpaka wa manane). anyway labda ndo kucapitalise on scale. nitembelee bloguni kwangu huwa ninaongelea sana masuala ya macro economics.

    na sasa mnapokula wali wa shilingi 200, huyo mkulima mlimlipa vyema kweli jasho lake?

    cheers

    ReplyDelete
  12. mmenigusa kwenye anga zangu, hivyo mtu akifanya biashara mfano hiyo yako. au la kuna jamaa yangu mkenya tena alizamia tu huku, sasa ana viduka vya kawaida vitatu size ya kuntena pale durban, kila kimoja kinamuingizia rand 10,000 kwa siku. maana yake akifunga macho mauzo ya siku mbili ni 60,000 ni milioni 10,800,000 ya bongo, ana uwezo wa kutinga kwa shop na kuchana fiat palio au tata indica, kwenye manailoni. akisubiri subiri siku tu zaidi - zikifika sita anavuta corola kitu macho ya panzi ya 120,000

    ninachosema ni kwamba muda ya kufanya biashara katika mazingira ya kulia lia uliishapita. kwani mafuta bei ni ya kidunia, gari bei ni ya kidunia, kamera yako bei ni ya kidunia, kwa nini mchele wetu na huduma zetu bei ya kitanzania? ndio maana unakuta inamchukua mtu muda mrefu kupata gari, nyumba, na vitu kama hivyo, simenti watu wanashindwa kununua na bei mfano sasa ni kama ya huku nje. tusichoshindwa kununua ni bia tu ambayo nayo bei yake ni ya kimataifa pia. - hivi ndo vitu vilikuwa vinamkera lipumba na mbowe! insurance ya afya (CHF)ya 5000 inawashinda wengi sana bado. je daktari atafanya biashara na nani? vitu kama hivyo lakini ni sababu ya mazingira ya kuukumbatia ufukara yaliyoendekezwa kwa miaka mingi na mwalimu ambayo inabidi tuyafute!

    cheers

    ReplyDelete
  13. Mark, upo tena nje ya msitari. Tatizo wewe unasema kibongo wakati unawaza kighaibu. jamani, bongo ya sasa si ya mwalimu tena. ni bongo ya bongo. haina mtu. kama ni mtu au watu ni sie wenyewe. hapo ujue mie ni mfanyakazi serikalini lakini hakuna anayetia noma kwenye biashara zangu ambazo ni halali. unataka nini tena mark?

    ReplyDelete
  14. nakushukuru kaka michuzi kwa shule kali. pia ninashukuru wale fikra mgando kama kina mama anna hawapo tena serekalini. kikwetre ameonesha nia kwenye hotuba yake kuomba ushirikiano wa watanzania walio ndani na wa nje. tutampa ushirikiano kama azma yake ni hiyo!! - nia ni kujenga si kubomoa!

    ReplyDelete
  15. Mchuuzi,

    Awali, napenda kusema hoja nzuri ya kukumbushana kurudi nyumbani. Natumaini wengi kati yetu tuliopo ughaibuni tuna matumaini ya kurudi nyumbani siku tukimaliza kufanya yaliyotuleta. Waswahili husema "..Msahau kwao mtumwa.." na wengine husema "..Mwenda omo na tezi marejeo ngamani.."

    Pili, sioni kama kuna ubaya wowote kama baadhi yetu tuliopo ughaibuni kuamua kubaki huku milele. Hayo ni maamuzi binafsi ambayo hakuna anayeweza kuyaingilia. Zaidi ya hivyo sioni kuna ubaya gani Watanzania kuishi popote watakapo. Kwani hata nyumbani Tanzania utakuta Mkerewe kama mimi ni mzawa, mkuzi, nimetamakani na kusakini mjini Dar es Salaam na sijafanyiwa rai au kupigiwa kelele na Mkerewe yeyote nirudi kwetu Ukerewe au miye mwenyewe kujisikia kurudi kutamakani na kusakini kisiwani Ukerewe. Hali kadhalika wazungu ambao wametapakaa ulimwenguni kote na kujiita aidha Waafrika ya Kusini, au Wazimbabwe, au Wanamibia, au Watanzania, Waaustaralia, au Wanew Zealand, au Wakanada, au Wamarekani, au Wacarribean wametamakani na kusakini ndani ya nchi hizo na wanaendelea kuishi huko ughaibuni bila kuwa na shaka yoyote. Mfano wa karibu ulionijia ni wa Rais Bill Clinton ambaye ana asili ya Kiairishi ambapo ndugu zake bado wanaishi Ireland na anawafahamu na anawatembelea. Mfano mwingine ni Wahindi waliopo Tanzania. Wametamakani na kusakini na wanaendelea kuishi bila kubugudhiwa na kurudi India. Mifano ya karibu ya wazungu waliotuwama, kutamakani na kusakini nchini Tanzania ni pamoja na ambao wamewahi kuwa mawaziri wetu kama vile aliyekuwa waziri wa Afya Marehemu Dr Leader Sterling, Mbunge wa Kinondoni (ambaye ndiye mbunge aliyepata kuongoza kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi katika historia ya Tanzania!) Merehemu Dereck Bryson. Aliyekuwa Waziri wa Fedha Bwana Amir Jamal, Bwana AlNoor Kassum, Bi Shamim Khan, na Waziri wa Fedha wa serikali ya awamu ya nne Bi Zakhia Meghji. Wengineo ni Mbunge wa Singida mjini Mohamed Dewji na nduguze. Aliyekuwa Mbunge wa Kilombero Marehemu Abbas Gulamali. Mgeni mwingine ambaye ni mfano wa karibu katika hoja hii ni pamoja Meneja wa kampeni wa Rais wetu wa awamu ya nne Bwana Rostham Aziz amabye ana asili ya Kiiran kama sijakosea.

    La tatu, wapo waliowahi kurudi nyumbani kwa dhana kama anazozitetea Bwana Mchuuzi na wakajikuta wamepotea. Nina mfano mmoja wa karibu tena wa uhakika kabisa. Mwaka jana 2005 wakati Rais alipokuja Helsinki, Finland. Kuna kijana aliyejitoa kurudi nyumbani na akaahidiwa na Rais kwamba pindi atakapofika atashughulikiwa masuala ya ajira. Kijana akaondoka wiki mbili baada ya Rais na msafara wake kurejea Nyumbani Tanzania. Mpaka sasa hivi yupo hapo Dar es Salaam anasubiri ahadi yake itimie kama itatimizwa.

    La nne, kuwanasihi Watanzania kurejea nyumbani kwa kigezo cha uwekezaji katika sekta za shughuli za mkono kwa mkono(trade)na siyo biashara (business)hilo pia ni jambo la kujadiliwa. Bwana Mchuuzi (Michuzi), kama utakumbuka tulipokutana Chelsea Sports Pub suala la uwekezaji katika sekta ya biashara lilikuwa ndiyo kiini cha majadiliano yetu kwa jioni ile. Hoja iliyosimamiwa na wengi siku ile ni kwa Watanzania kuangalia uwekezaji katika sekta akili sambamba na mali. Kwa mfano, tumeona jinsi mahoteli mengi yanavyofunguliwa na wawekezaji lakini hatuwaoni wawekezaji hao hao wakiwekeza kwenye kufungua maktaba za vitabu, kuwekeza taasisi za elimu kama vile mashule na vyuo!

    Nisingelipenda kuandika sana kuhusu nyumbani na ugenini kwa sababu Bwana Mwandani kaliandika suala hili kwa kina na kwa ufasaha zaidi. Kwa wale ambao hawajasoma maoni ya Mwandani juu ya suala hili mnaweza kupata maoni yake kupitia www.mwandani.blogspot.com

    Ni miye mchumia mbali,

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  16. Bwana Michuzi tusaidie kujibu swali hili...Arnold Schwarzenegger kwao ni wapi na anaishi wapi sasa?

    Mtanzania.

    ReplyDelete
  17. nashukuru sana Tungaraza kutoa ufafanuzi katika mjadala huu. maana inawezekana kabisa ukirudi bila mipangilio ukaongeza namba ya mikokoteni ya kuuza maji dar, au vikontena vya soda halafu unaongeza matatizo kwa wenzio badala ka kutatua matatizo.

    haya mliyozungumzia huko chelsea club ningependa niyaone yalipo pia niyasome niyatafakari na kuyaexpose kwa wenzetu pia.

    cheers

    ReplyDelete
  18. Asante mti mkubwa mkavu kwa jitaada zako za kutaka kuniita mchuuzi, sio wa uuzaji bali wa kumtia mtu kamba. pia bwana alama sijamjua yu upande gani. kwa aliyeonana na rais aliyetembelea new york baada ya helsinki atakumbuka jibu kikwete (wakati huo waziri) alompa yanki mmoja aliyetaka kujua kama mambo homu ni bomba ili arudi. akaambiwa wewe unamn'goja nani akutengenezee nchi ili wewe urudi ufaidi? nami nawauliza, jamani mwangoja nani awawekee mambo sawa ndipo mrudi? kesi moja moja au kwa kimombo exceptions kama hizo za shwazniga, braisoni na kina jamal zingenoga endapo mti mkubwa mkavu ungekuwa angalau diwani hapo helsinki, na si mchezaji hatari wa chelsea club.
    naomba bwana mti mkubwa mkavu usichoke kujadili. pia jamani tembeleeni www.mbongo.com kuna vijivitu vya hom kwa jam..

    ReplyDelete
  19. bwana mchuuzi, mie nipo kwa bwana mbeki nikijaribu jaribu kuangalia kama bongo inaweza kurudishwa rula ilipopita. bwana michuzi pia ni bora kujua kuwa watanzania wanaipenda inji yao, lakini kwa miaka wamekataliwa fursa na ruhusa. hizi kwa miaka miiingi zimewafanya wazazi wetu wadidimie kila kukicha mbele ya macho yetu. hii imekuwa ni uzoefu mbaya kwa wengi sana hasa wa kizazi chetu. ukihoji inakuwaje unaonekana mhaini na usiye tayari kuendeleza amani na utulivu uliojengwa chini ya misingi imara ya askofu mkuu nyerere. wengi hawako teyari kuitwa mbwa,wasaliti, wahaini,au wasio na wito kama mnavyowaita wenzenu hapo tanzania. hii inakuwa mbaya zaidi t shirt na kofia ambazo hazikuchapishwa pale pale bongo zikishirikiana na magazeti kuweka viongozi.

    ReplyDelete
  20. kaka michuzi katika macroeconomy kuna GDP na GNP sio lazima kila mtanzania awe anachangia tu kwenye GDP watanzania wa nje wanachangia kwenye GNP.kuna watanzania wanaendesha makampuni yao vizuri tu huku nje,je unashauri wayahamishie bongo?cheki GNP ya India.cha muhimu nadhani ni kukumbuka nchi yetu na kushiriki katika kuiendeleza.kuwepo nyumbani physically sio lazima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...