jeff msangi utaacha lini kukwea ukuta neshno? si unaona sasa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Jeff kwanini usiwe unakwenda zile mechi za pale Magomeni mapipa?

    ReplyDelete
  2. kukamata majambazi hawawezi hawa, lakini kukamata waruka ukuta na kuwaumizaumiza raha sana kwao,jj

    ReplyDelete
  3. Safi sana wacha wathibitiwe

    ReplyDelete
  4. Ndiyo maana ninaheshimu mambo mengine mengi sana ya ulaya kuliko ya kwetu. Mojawapo ya mambo ninayoyaheshimu sana huku ulaya ni suala la haki za binadamu. Ninaafiki kwamba hata Ulaya upo ukiukwaji wa haki za binadamu. Lakini unyama, ushenzi, na upuuzi kama huu na ule wa mgambo site huku Ulaya hamna. Hata akama ukiwa umevunja sheria polisi hawatakuburuza kama mbuzi.

    Jinginewe, ninawaheshimu sana wazungu kwa kujifahamu(sense of self-awareness). Ninakereheka sana na kutojifahamu kwetu na ndiko kunakoufanya umma kama huo nyuma ya picha kuona ni jambo sahihi kwa askari kumdhalilisha raia. Ndiyo kunakofanya kuwe na maoni kama hayo hapo juu "Safi sana wacha wathibitiwe"(wadhibitiwe kwa usahihi).

    Uchunguzi wa kisosiolojia umebaini kwamba mapsychopath kama Foday Sankoh huwatumia sana walala hoi katika mapambano ya silaha. Mungu pishilia mbali Tanzania pasitokee kama yaliyotokea Liberia, Sierra Leone, na Somalia.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  5. niko na wewe mtimkubwa, hilo tatizo sio kwa police tu, hata viongozi wakuu wa sehemu mbalimbali, kiongozi anayestaafu na kuwa na mali nyingi ndiye shujamaa kwa jamii, ile yule aliyestaafu bila kuiba mali ya umma na kuishi maisha ya kawaida ya hata kupanda daladala huyo,anakuwa mjinga machoni pa jamii, tena wanamwita yule mzee bwenge alikuwa na posti nzuri sana zamani, "amechoka sasa"
    matokeo yake,, kila mtu ataiba akipewa posti, kamasivyo utachekwa uzeeni" kazi kwako,jj

    ReplyDelete
  6. Mti Mkubwa Mkavu wachagga wanashida sana katika kutofautisha 'dh' na 'th'. Kule Bongo kuna mchagga mmoja maarufu sana (hata watoto watoto wake tu wakututangulia kwenye jicho la haki wanaitwa 'mahayati')Pamoja na shule yake utamsikia "Kondomu ni kinga 'mathubuti'"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...