
amiri jeshi mkuu jakaya kwikete akiwa na igp mpya saidi mwema (gwanda buluu), dci robert manumba (suti kulia) mkuu wa fedha na utawala clodwig mathew mtweve nyuma yao ni alfred tibaigana bosi wa dar na paulo amani moses chagonja anaekuwa mkuu wa operesheni na mafunzo. hii ni baada ya kuwaapisha leo ikulu. anaepiga chebo nyuma shoto ni igp zilipendwa omar mahita
sawa nadhani hapo mheshimiwa JK kafanya kweli! huyu bwana na kikosi chake wanafanania na kitu inaitwa uzalendo! tunamtakia kila la kheri IGP Saidi Mwema!
ReplyDeleteJK fanya kweli na visiwani fumua fumua tafuta vijana wa kueleweka waweke kule pia! utashangaa Tanzania itakuwa peponi, sio hawa walikuwa wanaweka vinyesi kwenye visima na kuwasingizia raia! utajiwekeaje kinyesi kwenye kisima chako mwenyewe?
Michuzi,
ReplyDeleteKwa sisi tulio ughaibuni kupata picha za "reo reo" namna hii huwa ni faraja sana.Wengine tulikuwa hata hatuwajui sura zao watu hawa.Mimi huwa nawajua sura wale ninaopambana nao uwanja wa taifa wanaponiwekea zengwe nisiwaone vijana wa jangwani!
Kile kicheko cha Mahita cha kweli au...Haya basi twausubiri wema wa kamanda Mwema.
ReplyDeleteHuyu jamaa si mchezo hata kimataifa anaheshimika. Tulisikitika-ga sana aliponyakuliwa-ga kutoka u-RPC Mbeya kupelekwa interpol Nai. Hali ilikwishaanza-ga kutulia-ga mkoani kwangu.
Jeff taratibu baba unatuvunja-ga mbavu.
bwana mwema kasema anamshukuru sana bwana mahita kwamba ndiye kiongozi aliyewapika maofisa wengi katika jeshi hilo na kwamba watayaendeleza aliyoacha. jamani mpo hapo? mambo ni yale yale hakuna mpya!jj
ReplyDeleteHuyu bwana(mwema) anaonekana yupo simple lakini mahiri.Mahita anapaswa kujifunza kwa huyu kua uchapakazi si lazima uonekane umenuna mda wote!!!!
ReplyDeleteBwana marumba anaonyesha kweli mpiganaji kwani hadi ngumi ameshakunja tayari kwa mapambano.Tunawaombea kila la kheri hawa waheshimiwa.
jj kwa nadhani kwa mtu mwenye akili kwa kawaida huanzi na kumtukana mtu tena aliyekuachia ofisi. ila unaanza baada ya hapo na vitendo ndivyo huongea zaidi!
ReplyDeletekwani unaonaje JK kuitosa top brass yote ya polisi? inamaanisha nini? huyu Jk nadhani ni mtaalamu wa Disputes Resolutions.
ila tunashukuru sana wanablogu kumchimba mwara Omari kaogopa kuingiza timu kwa siasa! wakati anastaafu alisema anaelekea kijijini kwake kulima na hatoingia kwenye siasa kama "tunavyoandika". halafu baadae kidogo wakati anakabidhi ofisi akasema kijijini haendi mtu ng'o! atang'ang'ania pale pale dar! na ameuliza "we umeona wapi mtu anastaafu halafu anaingiza timu kijijini?" ahu ahu ahu !!!yani kajichanganya mwenyewe ndani ya siku 2! kapumzike bwana na ushike ahadi yako fanya biashara zako!
kama wamepikwa na aliyeoza basi nao wameoza, hakuna excuse ya kuchagua waliooza kwa sababu ni top brass! wapo wengine ambao hawajapita mikononi mwa kina mahita. mambo ni yale yale, ila watu tofauti tu, ndio mwendo wa kibongobongo.jj
ReplyDeleteNanukuu kadhaa aliyosema Kamanda Mwema zaidi ya moja la feya well kwa Mahita ambalo principally limesema kuwa alikuwa IGP kwa kipindi fulani (ndio maana ya kupika) na ni ukweli kuwa alikuwa IGP - hapo sioni neno bora zaidi maana huwezi kuita kupika kuwa ni sifa. Kamanda Mwema pia anatambua kuwa kuna document ambazo zitakuwa zimeliwa na mchwa pahala na ni Mahita pekee atakuwa na kumbukumbu hiyo.
ReplyDeleteSpeaking to reporters immediately after being sworn-in by President Jakaya Kikwete at the State House yesterday, IGP Mwema, (53), said that success in his new position depends on the support of the people.
’’There can be no security for citizens without co-operation between the police and the public.
He said that he was gratified that the public had expressed confidence in him upon his appointment.
’’I thank Tanzanians for their show of confidence. This shows that they are ready to support me,’’ Mwema said.
naomba niwe wakili wa Mwema, historia inaonyesha kote alikopita, ameacha mema na watu walisikitika alipohamishwa!!! - amekataa watu kuonewa, amechukia rushwa, na amekuwa mguswa wa mambo yanayohusu raia wake aliopewa dhamana kuwachunga.
amekiri kuwa anahitaji msaada wa watu. ameomba hilo. nadhani ni jambo la kwanza na la msingi kabisa! amewashukuru pia.
ni kwamba japo samaki akioza katika tenga ni vizuri kuwapeleka walobaki maabara na kupima kama pia wameharibika na kuepuka kutupa samaki wote na kula hasara ambayo siyo ya msingi.
mie kwa kweli upande wangu sioni tatizo kwa uteuzi huu, umma umekubali, huyu bwana ni msomi na ana sifa, ni mwenye maadili kama ripoti zinavyojieleza, na sioni chaguzi bora zaidi ambayo JK angeifanya. maana panapochemshwa huwa tunasema, panapoenda vyema ni vema basi tusifie - yaani tusiwe kama wanasiasa na majimbo yetu ya bloguni!. labda kama ipo namna nzuri zaidi ambayo angeifanya basi ni vizuri kuileta jamvini na sie tuifahamu na tutaipigia kidedea..na kujua kasoro. nia ni kurekebisha.
labda ilikuwa ni concept ya kutafuta IGP toka JWTZ! hii kitu pia ina side effect yake! kuna tofauti sana kwenye mafunzo ya wanajeshi na kipolisi! maoni yangu ni kuwa polisi kama polisi ikikaa vizuri bado ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi zake.
Naungana na wewe Mark Msaki
ReplyDelete