huyu ni haji manara, mwanae sunday manara 'kompyuta', ambaye bahati mbaya ama nzui kipaji chake ni cha kuongea na si kabumbu kama alivyokuwa baba yake. haji ni mtangazaji mashuhuri wa redio na pia mtoa mada moto kwenye mihadhara ya soka kama anavyoonekana hapa akichangia sababu za kuporomoka kwa soka bongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Sasa Haji kazi yake hiyo ya kuchonga imewezaje kusaidia kabumbu kupanda. Mwambie naye agombee TFF badala ya kubaki mchongaji tu.

    ReplyDelete
  2. Mdahalo uchangia ktk kuleta maendeleo katika soka ambapo pande mbili ukaa chini na kuangalia matatizo yanayo kabili. Kila mtu hawezi kuwa mgombea bali wengine watakuwa washauri maana kila mtu ana kipaji chake hapa ulimwenguni.

    Ndio maana unaona kuna wanasiasa, wakulima, engineers, Madokta na n.k

    Mtu kama Haji kama akiongea yale mazuri (facts) na yakiweza kufuatwa basi twaweza kufika mbali.

    Pia hii ni free world ambapo democracy ipo kila kona ambapo mtu waweza kuongea na kufanya lolote ambalo lipo ndani ya sheria.

    Soka la Tanzania limeshuka chini kutokana ya kwamba watu hawafuatilii vipaji vya watoto toka chini kabisa (mashuleni), Kama kungekuwapo na academy za michezo za kila timu ama binafsi kila kona ya nchi kama tunavyosikia majuu tungefika mbali siku nyingi.

    Nchi za kigeni wanafuatilia mchezaji toka chini kabisa na kujua vipaji vyao.
    Kuna ma-agents kibao utumwa kila kona ulimwenguni kuangalia wachezaji wenye vipaji na baadae ununuliwa.Mchezaji wenye vipaji ununuliwa mamilioni ya pesa akiwa na miaka 16, 18 n.k mfano Wayne Rooney wa Manutd au Theo Walcott wa Arsenal fc

    Tatizo letu tunalo, mtu awe kiongozi ama member ktk organisation yoyote ya michezo nchini kwetu uwa na mawazo ya kujinufaisha yeye binafsi kwa rushwa na n.k ndio maana tumeona wengine wakipelekwa mahakamani na kufungwa.

    Kwa ufupi hakuna proper structure and systems zitazo wezesha Tanzania kufanikiwa maana kila kona kunanuka rushwa rushwa tu.

    Jiulize lini Tanzania itaweza kufika world cup na Africa Cup of Nations au tutabaki kuangalia ktk luninga tu mpaka mwisho wa dunia unapofika!

    Tukitaka mafanikio tunabidi kuwekeza serious ktk michezo kipesa, kimawazo, ki-elimu (training) n.k

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi wasomaji wengine, Na kama nimewaudhi nawaomba mnisamehe.Ukweli Utabaki Ukweli.

    Nashukuru.

    ReplyDelete
  3. Namfahamu kwa fix hajambo kwelikweli.

    ReplyDelete
  4. Tulipokuwa wadogo huyu bwana ndio alikuwa Ahmed Jongo wetu mtaani.Alikuwa anachambua soka kama mtu mzima vile.My classmate Haji nasikia aligombea udiwani Ilala,ilikuwaje tena? Michuzi ukimuona mwambie namsalimia yeye na dadiye Hamida.

    ReplyDelete
  5. nimekupata mike. nashukuru kwa kunitembelea-ga (nikimnukuu jmwaipopo). nafarijika sana. hope wala kitabu kama si kutafuta mtaji kama wengine. ila naomba usiolomee. mambo iko huku kaka. walai tena, ingawa jamaa wengine wananilaani kwa 'kuwashupalia' kurudi bongo. uko wapi na wafanya nini sasa. tumia issamichuzi@gmail.com. sio mbaya ukileta na snepu, maana ni longi, au vipi kaka. huku redio wani wanakabwa sana koo na claaaaaaaudz. unajua jamaa wana tawi la prime time linaloandaa matamasha kibao. leo t.o.k toka jamaica wanatua kwa shoo mbili. mwisho wa mwezi shaggy anatia timu. hivyo utakuta wanajikombea umaarufu si wa kawaida. wastue jamaa zako wabadilike waende na taimu na wakaribishe mawazo mapya. ama rudi uwasaidie. hapa afadhali east afrika redio na tv. ila toka motie atwaliwe na bwana mambo yamepoa kidogoi ila kuna watoto wakali sana kama vile salama na josh. nawazimia sana. kwa leo yatosha...

    ReplyDelete
  6. Ahsante sana kaka michuzi,habari ni nyingi.Nitakuona kule kwenye email basi tunon'gone kidogo.Nakumbuka ile Miss X-mass miaka ileee pale Kilimanjaro Hotel? eeh bwana wale "waliobahatika" bado unaonana nao mjini? ile ilikuwa hatari kubwa.

    ReplyDelete
  7. haya blogi zinakuwa. Mike Mhagama, karibu kiwanja ufungue jabo blogi!

    MK mawazo mazuri sana, sasa tuanzie wapi? namba zenyewe ndio hizo mawazo mgando na zimegeuza vyama vya soka personal enterprises! mark

    ReplyDelete
  8. yelloman huyu anaongopa sanaaaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...