
hii ni ndoa ya mkeka ambayo ni ndoa ya kiislamu ambapo muoaji anapeana mkono na ba mkwe na kujibu maswali ya ndoa akiongozwa na shehe. mke mtarajiwa huwa chumba kingine, viapo vya ndoa vikikamilika ndipo mume anaenda kumshika mkono. neno 'ndoa' ya mkeka limekuja baada ya zoezi hili kufanyika wakati mtu anafumwa na mtoto wa mtu ambapo kinachihitajika hapo no mkeka na shehe tu. picha hii ni ndoa halali ilofanyika ijumaa ilopita kule kigamboni...
Vipi wanarushusu mkristo kuoa binti wa kiislamu kwa mkeka. Maana naona hii safi sana. Na yaweza wafaa walio wengi ambao kuyapata maukumbi, makina-Michuzi, matarumbeta na mabaluni kwao ni nuhali. No gharama kubwa.Kashata, kahawa na juisi imetoka. Au ndio mpaka usilimishwe kwanza?
ReplyDeleteAsante kwa somo Michuzi. Inaelekea unanusa sana kwenye pilau ndugu yetu. Jeff anajulikana kwa kuruka ukuta uwanja wa taifa, wewe naona unajulikana kwa kunusa kwenye mashaba...itabidi niwe nakaa karibu yako maana kwenye pilau hunitoi.
ReplyDeleteSHEKH KACHINJA KUKU KICHWA KABANIAAAA!!!!! HAAAA.shunghuli ni watu, kaa mkao wa kula! jamjuah
ReplyDelete