sasa we john mwaipopo ndo nini kuturusha roho na kadaladala kako namna hii?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Si utani.

    ReplyDelete
  2. Huu ni ule utani wa kweli.tetete! Umenikumbusha mbali sana na hivi Vipanya vya Sinza, n.k. Kumbe bado vipo tu? Hapo ajari ikitokea haponi mtu!

    Usafiri ktk Bongo yetu kweli bado hupo nyuma kabisa. Asilimia kubwa ya mabasi yetu hayafai kuwa barabarani kabisa.

    Serikali na wadau wengine wangeliangalia hili swala na kutuletea Usafiri wa salama na unao aminika.

    Lakini hipo siku tutafika kwa maendeleo kama ya wenzetu wa huku ughaibuni.

    Wote tulio nje tukiona maswala kama haya na mengine tuwaze jinsi gani ya kuleta maendeleo ktk Taifa letu na Wananchi wetu na sio kudumisha na kuiendeleza rushwa na ubinafsi.

    Mataifa mengi yalio endelea yalitokana na Viongozi wao pamoja na wananchi wenyewe kuwa na uchungu, Hekima na Busara za dhati mbele ya kuleta maendeleo ktk Mataifa yao.

    Kwanza kabisa sijui ilikuwaje mpaka gari hili likaruhusiwa barabarani? Sijui ndio rushwa yenyewe? Yaani nina uchungu sana lakini ndio hivyo majority wa Wabongo wanajali nafsi zao na familia ama marafiki zao tu.Ukiongea maneno kama haya wataona unawaboa au kuwayeyusha.

    Tuwe na uchungu na Taifa na wananchi wetu na tusiwe tunakubali kuwa kama dampo la kutupia magari haya mabovu.Wanauza magari yaliyo tumika bei rahisi kwasababu ni vigumu ku-recycle ktk nchi zao hivyo wanaogopa yatakuwa kama takataka.

    Naona niishie hapa maana nina Hasira na Jaziba kubwa.Maana mfano jiulize kwanini DSM isiwe safi kama New York au jiji lolote europe? Kipi kigumu? Uongozi au Wananchi? Barabara zinajengwa na kuwekwa maua lakini watu wanapita na kuyakanyaga na mwishowe kufa. Jiulize leo ukipata jibu, kesho mfundishe ndugu, jirani, jamii ata mtoto wako ustaarabu utakao leta maendeleo ktk Taifa.

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

    Nashukuru.

    ReplyDelete
  3. Mk umesema ukweli. ni ukweli na kati ya matatizo makubwa yaliyokuwapo labda sasa yanaanza kupungua ni walio ndani ya nchi walikuwa wanawaona walio nje ya nchi wanaringa na kujidai wanaposema ukweli! walio ndani husahau kuwa hawa walio nje hata wao walikuwa wanafikiri vivyo viyo walipokuwa ndani! sasa basi cha muhimu ni kufunuana macho na fikra zaidi ili turekebishe haya mambo. cha kwanza kabisa ni kukubali ukweli!! tusing'ang'anie kuwa mambo ni sahihi japo sio sahihi!!na ndio suala zima la umuhimu wa kila mtanzania kuwa na blogu!

    uliyoyasema ni ya ukweli! cha ajabu utakuta hizo ngoma zimejazana hapo hapo dar wakati mkoani usafiri bado ni shida! nakumbuka kuna wakati mitaa ya Musoma nikiwa na kifaili changu ilipidi nisafiri (kwa kulipa nauli)juu samaki wakavu waliokuwa juu ya keria ya land cruiser stesheni wagoni!!! na tulikuwa wengi! mungu wangu! si unajua land cruiser ilivyo ndefu halafu tena unakaa juu ya mzigo...na terrain zenyewe za barabara, usipoangalia unatupwa chini.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2006

    MAJIBU YA NINI?MWAIPOPO UNAJUA JAMAA ANACHOJUTIA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...