
wanafunzi wa jangwani wakisubiri kumlaki madiba siku alipozuru bongo mara baada ya kutoka gerezani mwaka 1990. hii pia ni mojawapo ya picha zangu za awali. aliesimama na bango nyuma ya neno amandla ni jamillah mwanjisi (alikuwa mwandishi sasa ni bosi ngo ya kimarekani ya pact) anayekenua nyuma ya neno jangwani ni fatma fereji nasikia yuko ughaibuni kwa sasa. wengine nimewasahau. nawakumbuka hawa wawili sababu waliulizia picha hii ilipotoka gazetini.
Michuzi umejitetea vizuri. nafikiri ulibashiri ujio wa maswali ya uliwajua/fehemu vipi hao?
ReplyDelete