Home
Unlabelled
siku ya siku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
zanzibar ndio nchi iliyowahi kuongozwa na raisi mjinga kuliko raisi yeyote yule duniani.naye ni hayati sheikh abeid amani karume.
ReplyDeletena hapo anasaini dili na raisi mwenye kichwa kuliko wote.
hicho kikopo hapo mezani kina wino wa dole gumba kwa ajili yake, ila yeye akagoma akashika peni. kazi hipo. jamjam
Vipi hati za Muungano zilishapatikana Michuzi au kesi inaendelea?
ReplyDeleteUnapimaje weledi wa mtu? Yawezekana Karume hakujua kusoma na kuandika vema, lakini walau katika mazingira yake, alijitahidi kuifikisha Zanzibar hatua chache mbele. Je leo hii baada ya "Rais mjinga kutokuwepo Zanzibar iko wapi?"
ReplyDeletekweli bwana, hapo naona anatia siginecha.
ReplyDeletetena aliiba dola milioni moja kampa bakhresa, ndio mwanzo wa utajiri wake.
ndio maana bakhresa akuguswa hata na sokoine.
Michuzi,
ReplyDeleteSio siri. Mimi hapo nimemtambua Nyerere na Karume peke yake.
Naomba nikupe mji - Mtwara!
Sasa tusaidie kutegua kitendawili.
Kulia nyuma ya Hayati Mwalimu Nyerere, namuona Marehemu Oscar Kambona na katikati ya Hayati Mwalimu Nyerere na hayati Abeid Aman Karume namuona Marehemu Kassim Hanga kama sijakosea.
ReplyDeleteSijui Marehemu Karume kama angekuwa hai mpaka leo yale maghorofa kama ya Michenzani yangekuwa yameenea Zanzibar nzima, TV ya Zanzibar pengine ingekuwa ndiyo BBC ya Afrika Mashariki au Afrika nzima, na labda Zenji ndiyo ingekuwa social welfare state ya kwanza ya dunia ya tatu.
Viongozi wa kariba ya Hayati Karume kwa Kiingereza huitwa technocrafts, viongozi wa kariba hii wao huwa ni mabwana fanya siyo madomo kaya. Tukianza kuchukulia usomi wa madarasani kama kigezo cha uongozi basi kina Dr Kamuzu Banda, Dr Leopold Senghor, Dr Kofi Busia, Dr Milton Obote, Dr Félix Houphouet Boigny, na hata Dr Jonas Savimbi wangeweza kuzifikisha nchi zao kimaendeleo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiteknolojia, na kisayansi mbali sana.
F MtiMkubwa Tungaraza.
Mtimkubwa kupotea kwako kunapunguza upatikanaji wa weledi. maneno yako yote yana ukweli.
ReplyDeletewe jinga kabisa, we unaona magorofa ya michenzani ndio kitu cha maana?
ReplyDeletewe unaona TV mdio kitu cha muhimu kwa wakati huo?
hatuzungumzii madakata dakta dakta dakta hapa, majina unatoa kwenye vitabu vya historia.
huyu alikuwa jinga na hata mwane alioko madarakani sasa ni jinga.
we unaweza kuangalia tv wakati unanjaa?
kwanza hata umeme wenyewe hakuna.
kwanza aliyewakomboa wazanzibar ni JOHN OKELLO sio baharia karume
ReplyDeleteMjadala huu kuhusu nani alikomboa Zanzibar (Karume au Okello) au kama Karume alikuwa mjinga na ujinga wake uliiathiri Zanzibar (au alikuwa mjinga ila ujinga wake haukuzuia uwezo wake wa kujua mambo yapi muhimu kwa Zanzibar, sio mjadala wa juu juu. Wala tusianze kuitana majina. Kama mtazamo wangu ni tofauti na wako, bado sote ni binadamu. Tofauti ni kuwa tuna mitazamo au ufahamu tofauti. Blogu ni kama soko la mawazo na fikra, ukiweza kuuza fikra na mawazo yako bila kuitana majina, bila jazba, bila matusi tutakuwa tunajenga jumuiya ambayo ni sawa na benki ya maarifa na majadiliano.
ReplyDeleteKwa ufupi, tuendeleze mjadala huu. Kama kuna watu wana ushahidi na vielelezo zaidi vya madai wanayotoa ingekuwa vyema vingetolewa. Kwa mfano, suala la Bakhresa. Nina hamu sana kujua undani wa hili. Kuna watu wenye taarifa zaidi?
Asante sana bwana Ndesanjo mimmi binafsi nashindwa kuvumilia hasusan pale ninapoona watu huitana majina na kutukanana kwa sababu tu mtu mwingine anamawazo au ufahamu wa tofauti na wake juu ya jambo hilo. Na matokeo yake tunabadili kabisa nia na mantiki yote ya blog. Aksanteni, Upendo na amani vizidi na idumu inchi yetu Tanzania .......
ReplyDelete