Home
Unlabelled
amina
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Michuzi naomba tuwekee na ya Lucy Mayenga.
ReplyDeleteHuyu mheshimiwa anajitahidi ila shule inamleti down. Anaishi kwa ujanja ujanja wa mdomo tu. Kaka Michuzi mshaurini aende shule kidogo angalau itamsaidia atafika mbali. Mwambieni ajiandikishe angalau Open university.
ReplyDeletemija shiya nimekupata,naifanyia kazi. grill sina cha kusema kwani sijui ntaanzia wapi. eniwei, nitajaribu kutafuta njia salama ya kufanya hivyo
ReplyDeleteakitumia muda mwingi kujipendezesha na kufikiria gari gani atokenalo hili kila mtu amuone atakuwa mbunge wa kujiwakilisha mwenyewe nafikiri atakuwa wakwanza kujiwakilisha katika historia ya tanzania.
ReplyDeleteKama ni ambisheni amefikia mshauri hapo ndo mwisho hawezi kuvuka sasa mshauri atafute jinsi ya kutatua matatizo ya vijana. Vijana hawana ajira, hata wenye elimu ya juu!!!. Sijui atawasaidia je? mungu wangu tanzania ina vituko.
Kitu kinachonifurahisha ni kuona vijana wa kike na kiume wanajitahidi kuingia kwenye ulingi wa siasa ni jambo zuri, lakini ktk elimu naona wanablog wengi wanalitilia mkazo sana hasa mh Chifupa mim binafsi sioni ni suala la kuliongelea sasa hivi tunachotaka ni kuona anafanya kazi ipasavyo hasa kama yeye bado ni mrembo na kijana anafahamu ugumu na tabu za watu mbalimbali kimaisha tumpe muda tuone atafanya nini sio kashfa zinazotolewa kuhusu elimu aliokuwa nayo.Mh Chifupa fanya kazi unayopaswa kufanya GOD BLESS U.
ReplyDeleteKitonga ....said
hana sifa za open university ama college yoyote ambayo inasisitiza elimu.Kumshauri kitu kisichowezekana ni kuidharirisha Elimu ya JUU.Bunge letu halijatoa vigezo vya elimu, hivyo mwacheni aendelee kuwepo pale DOM.
ReplyDeleteShule ni kitu ambacho unakwenda kwa sababu unataka siyo kwa sababu ya kulazimishwa na mtu mwingine. Mkimwambia dada huyu ajiandikishe sijui chuo, mtamfanyia homework zake? Maana chuo kinahitaji discipline na personal DRIVE. Ukijiandikisha kwa sababu fulani katoa ushauri utakuwa unasoma kishingo upande.
ReplyDeletehuu mtindo wa nywele wa AC unaitwa shpaghetti.kuutengeneza unatumia masaa 14.kwa standard ya aliyeubuni hautakiwi kukaa kichwani zaidi ya wiki mbili.
ReplyDeleteIli uwe mwanasiasa mzuri inabidi uwe hujasoma vizuri kama AC. Kwa sababu ndani ya siasa ni usanii mtupu ambao wasomi wengi wanashindwa. Ukijua kubwabwaja inatosha sana, hauhitaji kuwa na basic degree kujua matatizo ya wananchi wako. Tumeona watu wenye PHD wanashindwa ubunge kwa sababu wanashindwa kuwadanganya wapiga kura
ReplyDeleteJamani mimi sikutoa ushauri wa kwenda shule kama kashfa. Mie nimemshauri tu kuwa kwa sasa mheshimiwa pamoja na nafasi aliyonayo kwa uhakika wa kutuwakilisha vizuri na kuwa na confidence zaidi anahitaji shule hili halina ubishi kama tunamtakia mema.Sasa hivi sawa bunge halina kigezo cha elimu lakini itaendelea kuwa hivyo hivyo milele. Mheshimiwa bado kijana na bado tunamtegemea siku zijazo. Kwa kumbukumbu zangu ndogo nilizo nazo Mheshimiwa alimaliza Makongo na hakufeli sana inatosha kabisa kumuwezesha kujiendeleza zaidi
ReplyDeleteje nyie mnao mpinga huyu ni wanachama hai wa CCM? au ummesahau kuwa huyu ni mali ya CCM, na ndio wao wameona anafaa na wakamtuma bungeni,cha msingi ni nyie kujiunga na CCM,kuwa wanachama hai, mumpinge ndani ya chama,ubunge sio cheo cha kiserikali, kapelekwa bungeni na wanachama wake, sasa nyie hamtaki?
ReplyDeletechama kilichomtuma JK ndio hicho hicho kimemtuma yeye bungeni na kilipima kikaona anafaa, mbona mnamuonea dada wa watu?. kupata sifuri shuleni sio mwisho wa mapambano ya maisha.,
hii ni changamoto kwa kinadada walio wasomi wajitokeze.
jamjuah...said
Mhe. Amina Chifupa continue with Ur work, and like we say just brush Ur shoulder off. Do Ur best to serve wanawake na vijana, na Mungu Akubariki.
ReplyDeleteMie binafsi Amina nampenda sana, unajua kwa nini... yaani hivi mnavyomsakama yeye ndio huwa anapenda! Huwa hababaiki hata robo na maneno madogo madogo, anajua anachokifanya. Hiyo form 6 hakuzungusha kwa makusudi. Ilitokea bahati mbaya tu kama mtu yoyote anavyoweza kutokewa. Mipango yake ilikuwa kwenda University... kama mtakumbuka alikuwa akiongea mwenyewe redio clouds kabla majibu hayajatoka. Lakini kuzungusha hakumaainishi kuwa hawezi kuingia University.
ReplyDeleteAnaweza akatumia hiyo Diploma yake ya chuo cha uandishi ikasupplement form 6!
kwani lazima usome chuo kikuu ndio uwe kiongozi bora?hakuna roketi sayansi kwenye ubunge, ni mambo ya kawaida tu,mbona simba wa vita(kawawa) alikuwa na elimu ndogo tu, lakini mavitu yake kila mtu anayajua? msimtishie na elimu yenu ya chuo kikuu.
ReplyDeleteje hamuoni kuwa ni makosa kuchukuwa watu kama kina sarungi na kuwapa ubunge/uwaziri?
mtu kama sarungi angekuwa more productive zaidi kama dokta na sio waziri,angeponya wengi sana kama Dokta, kazi ya uwaziri/ubunge hata Ditopile/makamba..nk wanaweza kufanya.
na sio sarungi tu, wapo wengi kina mwakyusa,mwandosya, ect ect.
wataalam wetu wa hali ya juu wanishia kuwa mawaziri, wapi na wapi!jamjuah
Na mimi namuadmire Chifupa. Nafikiri anaweza kufika mbali kwa sababu haogopi kujaribu chochote. Kuna 'waliosoma' ambao wataendelea kumkatisha tamaa hata akipata degree (wakikumbushia matokeo ya form 6) lakini akiendelea kuwa strong atafikia status na respect za kina sofia kawawa, bibi titi na maria nyerere. She has that potential.
ReplyDeleteSystem ya Form 6 na vyuo vyetu ni shady. Kuna watu wana uwezo wa kuimanipulate kwa sababu kama za kisiasa etc. I've been there and I'm the living proof. Ili afanikiwe namshauri abaki tu CCM na ASIWACROSS WAKUBWA, rules mbili kubwa.
Anon hapo juu , please can you elaborate to me in laid man terms , what did you mean by ASIWACROSS WAKUBWA ?
ReplyDeletenATANGULIZA SHUKRANI.
Wanasema ujanja ni kupata si kuwahi, bibie keshapata, wenye wivu tujinyonge.Eti anonymous mmoja anadai eti alizungusha, hivi ni kweli?
ReplyDeleteSasa atawezaje kufuatilia mijadala yenye masuala mengi ya kiufundi yanayohitaji taaluma? Nitafuatilia kipindi kizima cha bunge la bajeti nione kama ataweza kuchangia mada ndio nijue hii kasi mpya ni utapeli tu, unajua mambo umafia.
Hivi, michuzi naomba kuuliza, huyu bibie keshachangia mijadala mingapi tangu bunge jipya likutane?
Kwa aliyeniuliza swali 11:13 AM, namaanisha asije kurukia mambo kama kashfa za serikali au watu fulani kwa kutoa maoni yake, kwa sababu mpaka aje kujenga 'secret empire yake' na click ya vigogo ya kumlinda yeye atabaki slave wa CCM na afunge mdomo wake kwa mambo kama hayo.
ReplyDeletePande zote mbili, za CCM na yeye, wanafaidika na uhusiano huu, kwa sababu ya attention vijana wanayompa. Lakini the minute anafyatuka, she's over (I can see situation kama hizo zikija, na kuna watakaomset up, labda kwa sababu zao binafsi, ili ajump in). Otherwise, sky is the limit for her.
Kwa ambao wanamdismiss kwamba hawezi kuchangia mijadala ya Bunge, nadhani mnamuanderestimate sana AC (na sisemi kwambe yeye ni genius au hata close to genius). Namkumbuka ameshiriki sana debates za wanafunzi Dar wakati yupo Kisutu, hata hivyo siwezi ku-recall uwezo wake kwenye hizo debate. Hiyo ukichangia na experience ya radio na natural talent ya kuongea utagundua ameanza na experience kubwa kuliko wengi ambao wanaingia bungeni kwa mara ya kwanza.
Ino
ReplyDeleteSo far ninachojua Amina kasema bungeni ni ule mchango wake wa kuipa lugha ya kingereza umuhimu ktk shule za msingi. Pia juzi juzi akiwa UDSM aliwaeleza vijana kuwa anaanda hoja binafsi ya kuomba wanawake wawe empowered kutongoza wanaume. Hizo ndio hoja za mheshimiwa.
Nadhani hoja ya elimu kwa wabunge ina umuhimu. Nadhani tumeona wimbi la ubatilishwaji wa sheria na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa na serikali na kupitishwa na bunge. Tunapokuwa na wabunge wengi wa aina hii sio rahisi kwao kuona katiba ambayo ndio sheria mama inavunjwa matokeo yake wao wanapitisha tu.
Nadhani kuna haja ya mdahalo wa kitaifa wa kuangalia sifa ya elimu kwa nafasi ya uraisi na ubunge, watu wa type ya Chifupa kielimu kwangu mie ni sawa na kupoteza hela za nchi tu wanapokuwa wabunge
Mawazo ya waliowengi ni mazuri sana. Je ni lazima mtu awe amosoma sana ili awe mbunge?, kama wengine walivyoweza kudanganya na vyeti feki vya PhD ili wapate ubunge?. Mimi nasema jama si sawa. Nakumbuka kuna mweshimiwa mmoja alisema katika muda wake ameboresha masirahi ya wabunge mpaka maprofesa wakakimbilia bungeni. Hii ni sikubaliani nalo, maprofesa ni aghali kuwapata hivyo wabaki vioni.
ReplyDeleteMimi nafikiri mbunge awe na basic knowledge na uwezo wa uongozi ambao amina anao. Hila kwa sababu wanafanya mabo makubwa ambayo yanagusa jamii basi kuwe na kiwango cha elimu hapa angalau basic certificate in Law.
Ili akipewa makabrasha ya bunge yasiozee kwenye sijui Lexus. Hivyo kuwa mbunge kama Amina nafikiri anafaa ili mradi ajiendeleze kidogo ili ajue jinsi ya kutofautisha hoja ya ubunge na mitaani.
AMINA CHIFUPA HUMU KATUMA ANONYMOUS KADHAA ILI WAJE KUMUUNGA MKONO.HIYO COMMENT MOJA HAPO JUU KAANDIKA YEYE MWENYEWE.INAELEKEA HAJIAMINI,AMNGEKUWA ANAJIAMINI ANGEACHA HII IWE FREE DISCUSSION.MLIO NJE INAWEZEKANI HAMUELEWI VIZURI HALI YA SIASA NCHINI KWA SASA ILA UBUNGE SIKU HIZI NI BIASHARA.AMINA ALIKUWA NA MTAJI WA KUTOSHA NDIO MAANA YUKO HAPO.KAMA TU BW. SADDIQ ALIVYOKUWA KULE MOROGORO.KULIKUWA NA WAHINDI KIBAO WALIONYAKUA NAFASI KWA STYLE KAMA YA CHIFUPA ILA WAKATEMWA.HAKA NI KAUBAGUZI TU TULICHOWAFANYIA WENZETU WAHINDI KWA KISINGIZIO KUWA WAMETOA RUSHWA.ANGALIA ADAMJEE PALE KAWE ALIVYOKUWA SUBSTITUTED FOR MAMA MLAKI.KUNA MIFANO MINGI.
ReplyDeleteHaki ya nani watanzania bado tupo mbali sana na nadhani umaskini tulio nao tutaendelea nao mpaka kiama. Kijana wa leo unalinganisha uongozi unaotakiwa sasa hivi kwa maendeleo ya nchi na uongozi wa Mzee Kawawa, KITUKO. Watu tunafikiria uongozi ni uwezo wa kuongea tu basi tuwapeleke akina Mzee jangala bungeni kwa sababu wanajua kuongea. Suala la mbunge sio kuchangia tu ni validity na analytical ability ya anachochangia. Lazima ifikie kipindi tujiulize kwa nini nyingine rate yao ya kuendelea inatofautiana sana na ya kwetu. Angalia nchi kama China wanavyoprogress kwa nini sisi badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma?
ReplyDeletegrill mimi nakubaliana na wewe.inabidi tuache uvivu wa kufikiria.vilevile nakubaliana na anonymous aliyesema kuna mkono wa amina chifupa katika hizi comments,angalia comment ya 9:47 aliyeandika anadhihirisha ukaribu wake na mheshimiwa.hapa ndio swala la elimu linapokuja,mkitaka kufanya manouvre tumieni njia za akili zaidi.we are smarter than you think.
ReplyDeleteNasukuruni sana kwa maoni yenu, sasa hivi nashukulikia wananchi, na kama nitahitaji hiyo Elimu kuporesha matakwa ya wananchi...nitaenda kusoma , na hela sio tatizo sasa hivi. Shule ni kukazana, na hapo njuma sikutilia umuhimu. Bwana Mija, Grill, anomy, sem, inno, zema naombeni maoni yenu from now forward, haturudi nyuma.....Aksanteni ! Karibuni nyumbani watu wa majuu. Amina
ReplyDeleteAmina, kama kweli ni wewe uliyeandika hapo juu nina ombi binafsi, kwamba ufungue blogu yako ili tuweze kusaidiana zaidi kimawazo. Kwa nafasi uliyo nayo sasa hivi mimi naona ukiwa na blogu inayojadili masuala ya vijana itakuwa vizuri sana maana utapata muda wa kubadilishana mawazo na vijana wote ulimwenguni, kitu ambacho kitakusaidia sana kupata hoja nzito nzito za kupeleka bungeni.
ReplyDeleteNaomba kuwasilisha hoja, na ninaomba sana ombi langu usilitupie kapuni.
Vijana Tz wamekuwa Marginalized sana nadhani tunatakiwa tuwe na sehemu ya kuwasiliana na kupeana mawazo jinsi ya kuendeleza nchi yetu. Nadhani wale wawakilishi wa vijana tafuteni sehemu ya kuweza kupeana mawazo ili tuweze kupunguza hata hii mizee inayodhani kuwa sisi ni taifa la kesho. Hawa wazee wana mawazo ya kujinufaisha tu na kijilimbikia mali. Anzisheni web ya vijana tuwe tunatolea mawazo yetu hapo vizuri bado tunaipenda nchi yetu na tunapenda kurudi kushirikiana ila tukifiria hiyo mizee ilivyoshikilia kila kitu tunaishiwa nguvu. watu wanafanya ofisi ya serikali kama ya kwake tabu kweli kweli.
ReplyDeleteAnapendeza sana mama huyu. Apewe hongera zake
ReplyDeleteWatanzania hamkosi cha Kusema. Amina Dada Yangu endelea na juhudi zako. Mambo ya Elimu ya darasani wala hayasaidii. Kwani kuna shule yenye degree ya kuwa mbunge?? Elimu uliyopata mtaani na ujanja wako binafsi unatisha kabisa kutusaidia sisi vijana bungeni.
ReplyDeleteMambo 3 ya kuanzia Dada yetu ambayo naweza kukushauri ni
1. Ajira kwa vijana
2 HIV/AIDS
3. Mikopo kutoka bank kwenda kwa SMEs za vijana.
While U are at it, U can also deal with education, Health and so forth.
No degree required for dealing with these issues that will benefit the country as a whole.
Aminia Mama Fanya Mambo!!!
Amina dada endelea na moto huo huo muhimu tu fanya juu chini ukutane mara wka mara na vijana na kusikiozia hoja zao .Na pia waliopo hata majuu unaweza kwua na website watu wanadiscuss humo hoja zao kupata details watu wanapenda nini. Mambo ya shule yatakuja yenyewe Umebahatika dada na mungu akuonyeshee njia usaidie vijana wenzako .
ReplyDeleteCindy
Mija nashukuru wa wazo lako zuri sana, sasa hivi tupo kweney early stage....Vijana tunabidi kustand zaidi ya wazee wetu. Mambo ya website/blog yako mbioni, na tutawatumia wakina Mr. Michuzi kuvikisha habari kwa wananji. Nguvu, Kipaji ninacho...na karibuni tutakuwa na better communication. Jamani ni usiku wa amanane hapa nyumbani.....Asanteni
ReplyDeleteUongozi hauitaji elime ni kipaji cha mtu na elime inasaidia pale ambapo lugha za kiufundi zinatumika. AC(air con) sijui kasoma kiasi gani na swali langu kubwa na nafikiri mzee michuzi utanisaidia, alichaguliwa kwa vigezo vipi? kitu gani amefanya kubadilisha maisha ya wanawake na vijana? na kweli hakuna vijana watanzania ambao wana vipaji na elimu? sina mapenzi na siasa na hasa pale inapofikia kwenye masuala kama haya.
ReplyDeleteGuyz enough pictures and stories of this Lady MP. Let's use Michuzi blog wise for more useful debates. I believe she is not the first MP to get to the Parlianment with such history nor will she be the last. Politics is more about WHO YOU KNOW and not WHAT YOU KNOW.
ReplyDeleteAMINA WE KIBOKO NAKUPONGEZA KWA KUPENDWA NA WATZ!!!! COMMENTS 35 HAIJAWAHI TOKEA NAKUMBUKA HATA NILIPOKUWA BONGO SIKU AKITOKA KWENYE MAISHA AU KASHESHE BASI UJUE GAZETI LITAUZA SIKU HIYO MPAKA BASI
ReplyDeleteKWELI NIMEAMINI MTU WA WATU HA HA HAHA HAHAHAA WATZ KAZI HAKUNA.....
Kweli nimekubali kwa nini amina anajidai sijui niseme wanampenda sana nafikiri amina anaweza kuleta mabadiliko kwa vijana Amina fanya kazi. Vijana wanakupenda Mnnooooo. Hila Usijiwekembali nao. Chukua ka Mark II. Ili Vijana Wawae kukusogelea.
ReplyDeleteNafanya study kuona association ya elimu na uchangia hoja katika bunge. Nitatumia data zilizoko kwenye website ya bunge ila tatizo wabunge wengine hawajaweka sifa zao. This is a sort of prospective study ambyo results zitakuwa nje mwaka 2010 nadhani nitakuwa na hoja ya kusema kuhusu elimu na effectiveness ya ubunge na kuomba watanzania tupigie kelele mjadala wa kitaifa wa sifa za ubunge. Nadhani mambo yanabadilika na viongozi wa serikali watafika siku kuona kuwa wanatakiwa kusikiliza wananchi mradi tunayoyasema yako supported na sayansi
ReplyDeleteshavu la mheshimiwa hilo au macho yangu mabovu ? maana ........... mhh!!!!
ReplyDeleteIla michuzi mimi namuunga mkono sana GRILL, jitahidi kadri ya uwezo wako kumshauri tunajua wewe ni mtu ambaye uko karibu na watu wengi akiwapo huyu mheshimiwa
Hii ni topic ya MWAKA,
ReplyDeleteComments 40+ kwa topic isiyo ya UDAKU au Uroda! SI MATANI
jamani yule jamaa anayetaka kuoa mtoto wa kikwete imefikia wapi?Wabongo kwa ubitozi,jamaa anadhani akioa mtoto wa rais mambo yake yatakuwa safi,hes wasting his time.
ReplyDeletekwa maana hiyo mtoto wa JK hana haki ya kuolewa?
ReplyDeleteLets do our best to improve our economy. Watu wanakimbilia ughaibuni kwa sababu tumezoea ujana ujanja lakini I am telling you kwamba whatever is done in the US that make it attractive to many youths, can also be done in TZ coz we have resources, is a matter of being seriuos and assume our responsibilities in our respective position to better mobilze our resources. Thanks Michuzi for being such a creative person to come up with this. Hope mheshimiwa AC will take initiative to start something that will enable sharing of ideas among youths. Benny78.
ReplyDeletewewe Benny78 toka hapa na Kiswangilish chako. Unaona mada humu zinaandikwa kwa kiswahili wewe unatuletea kigagagigikoko chako humu! Tueleweje sasa kwamba huo uchanganyaji wako hakuna lugha yeyote kati ya hizo ulizotumia unayoimudu vema?
ReplyDeleteNa kweli huyu benny anatuchanginyi tu wengine... we huoni hata michuzi mwenyewe analonga kitanzania. Sasa wewe unatuletea kikristu chako wengine humu waislamu!
ReplyDeleteHuyu Benny naye katoka wapi huyu? inawezekana ni mlevi wa pombe kali huyu, ni wa2 wa kuogopwa sana na jamii, hawa ndiyo wanaharibu lugha yetu
ReplyDeleteBenny umesema kweli.
ReplyDeleteBenny
ReplyDeletebado unachanganya changanya lugha" specialized courses" na usifikiri kwamba watu hawaelewi kiingereza humu kwa kutafsiri, hapana, kila mtu anajua kiingereza hapa
Benny,
ReplyDeleteSasa hapo umepatia. KIDUMU KISWAHILI CHETU
AMINA UNA COMMENTS 53 SASA NIMEANZA KUSTUKIA DILI HUYU ANAANDIKA MWENYEWE NYINGINE KAMA 20 HIVI ZAKE HUYU,MAANA YEYE NA MUMEWE KWA KUPENDA PUBLICITY SIDHANI KAMA KUNA MTU ANAWAFIKIA ANAPENDA HUU MJADALA JUU YAKE UENDELEE...TUMEKUSTUKIA MAMA ACHA UJINGA.
ReplyDeleteMimi niko Uganda hapa Entebe na ninamfagilia sana sana Amina Chifupa,,,hongela dada
ReplyDeleteni kweli ata mimi nimeshtukia!!!!!!!!!!! ebu angalia picha ya nyrerere maoni machache lakini ya huyu demu aliye zungusha zero form six maoni kibao utadhani umuhimu wake ni mkubwa kuliko nyerere???????
ReplyDeleteHuyu kama ulivyo sema uenda anaandika mwenyewe sababu inapenda sifa sana wezi hawa na wauza unga huyu na kijisaloon kidogo, vi taxi vichache basi mamilioniea si ujinga huo???? Wakati umewadia kwa Tibaigana na Mwema kuwazukia hawa ndio wale wauza unga na wanaofuga majambazi.
Amina Acha Ujinga wa kuandika maoni yote juu ya nafsi yako huku ukibadilisha majina sio dili bali ni uzumbukuku.
Kwanza unapokaa tunapajua huna kitu zaidi ata ya jirani yako hapo kulia mwenye gorofa ni bure ajifagilie yeye kuliko wewe fara uliye jiuza zamani na sasa.Una bahati huyo fala mwenzio alikuchukua wakati unakijina pale clouds kwakuwa naye anapenda misifa lakini isingekuwa hivyo ungeendelea kupigwa vitu na wanamwaga nyuki 88.4 si unakumbuka kazi yako? Kama Unabisha sema nije na ushaidi tena nitampa bw. michuzi abandike mwenyewe!!!!!
Nina uhakika utakaa kimya na ukiendelea nitatoa ushaidi ili Tanzania yote na Wabunge wenzako wote wakucheke na kuamini kwamba kweli wewe si chochote wala si lolote.
Au umesahau uliyo yafanya miaka iliyopita ya kugawa uchi kwa wenye majina!! Au unadhani ujapigwa picha na hao wenyewe unao wapa kama pipi ili mradi wakupe kitu kidogo au unasahau unayo fanya sasa!!! Mimi ni dawa wa hiki kifupa.
Sijapenda sana comment ya mwisho inaonekana hayo ni matatizo binafsi au chuki binafsi kuwa na comment nyingi nafikri inawezekana kuna kitu vijana wanaweza kusoma hapa. Amina ni mwakilishi wa vijana na vijana ndo wanaandika hapa nafikiri wanapeleka ujumbe kupitia kwa mwakilishi wao kuwa hawajalala. Kwako Benny nashukuru kwa mawazo yako. Lakini Umechanganya kidogo kuwa uko US na elimu ya tanzania haina vitendo, ukazungumzia china, japan walivyoendelea. Vijana wa Kitanzania tayari Amina ni mwakilishi wetu kwa miaka takribani mitano. Benny hakuna nchi yoyote iliyoendelea kwa kutegemea vyuo vya nje. Hatuwezi watanzania wote kusoma US. Nauli tu ya kumtoa mtu Tanzania kufika US tayari ni fee ya kusoma Master Bongo. Nafikiri nchi kama India, Japan, South Africa, Misri, China zimeendelea kwanza kwa kuboresha Elimu yao kwenye nchi zao kwanza wakapata waalamu wa kutosha ndo hao wataalam wakaenda kusoma/kufanya kazi hata huko marekani na kwengineko. Nafikiri mimi hata Elimu ya Bongo kama ikitiliwa mkazo inatosha sana kumuendeleza mtanzania hata akashinda Elimu itakayopatikana Marekani na China.
ReplyDeleteMradi tu tuwekeze katika Elimu ilenge kutukomboa watanzania. nashukuru kwa kumalizia kuwa ungependa kusoma nawe bongo make bila kuweka hilo vijana wote tungeandamana kuoma viza kuja huko kupata elimu bora.
Kwa sababu haka ka ujumbe kamepitia kwenye saiti ya mweshimiwa mwakilishi wetu na fikiri atakaweka kwenye diary na kukakakarabati.
Mwisho Amina ajitahidi sana kuwa karibu na vijana bado pamoja na kutokuwa na elimu kubwa kama kaka yangu benny ila ni mwakilishi anaye weza kutuongoza hata sisi.
kaah ni kweli bwana mimi nilikuwa nimesahau kuwa alilamba ziro ndio nakumbuka alilamba ziro kidato cha sita huyu.
ReplyDeleteUliyesema anaubongo wa samaki na si mwakilishi wako unakimbia kivuli chake. Kwanza nafikiri hujui unacho kisema unasema tuuu ilimradi. Kuwakilishwa siyo kupenda. Hata kama humutaki anakuwakilisha labda tuombe atoke uende wewe na utuwakilishe. Mimi Amina simjui kabisaaaa, kabisaaa nilimskia wakati akiwa Tambaza miaka hiyoooo. Ninachoongea hapa ni kwamba tayari ni mbunge kwa sasa labda kama tunaona Elimu yake ni duni tupendekeze viwango vya elimu tupige debe hata nimuombe yule mzee wa masters aje angalau atusaidie tumuweke mtu atakaye tufaa. Kelele za nani fara hazisaidii sanaaa. Na usisahau anapita CCM uhende hukooooo.
ReplyDeleteNyie wote mnaongea unadhani hawa wote wana amua kuwa wabunge kuwakilisha vichwa vyenu? Wanakuwa wabunge kutafuta maisha! na wengine wanaonga kabisa wapate hizo nafasi! uwezi kujua naye alionga huyo akachaguliwa kuna vijana wangapi wanachama wa ccm wenye elimu zao hawakuchaguliwa si sababu hawana kitu sasa wabunge wote wezi hasa hasa wahindi wananunua nafasi hizi kupata green light za biashara zao. Wezi wakubwa hao msiseme wana ushujaa wa kukuwakilisha wewe kama kijana kwa lipi? kaongea nini mpaka sasa la vijana si anatafuta madili yake na ya bwana wake huyo.mi nitabaki kucheka na akili zenu finyu watanzania na kudanganywa na kukubali mbunge awe ni yule aliye pata ziro kidato cha 6 na kidato cha nne aliona pepa feki. hasara tupu kwenu na kwa haka kainchi.ndio maana uwa nikiwa bongo sipigi kura sababu naona nachagua mabwege kuongeza nchi.Eric
ReplyDeleteEric na anon wa 5.50AM siwaelewi kabisaaaaaa. Tunachotafuta ni jinsi gani tutamaliza matatizo kama haya nyinyi mko juu mno. Tunapingana lakini hatugombani,wa kwanza 5.50AM kachanganyikiwa, sijui amekuta kwenyea account hanana kitu simuelewi kabisaaaaa. ukiwa bongo huwa hupigi kula wazila wenzako wala na hawa wanawapenda watu kama eric. make wameishakubali kutawaliwa na yeyote yule hata kama ni jiwe. Sisi tunatafuta ni njia zipi tuzitumie.
ReplyDeleteByeeeeee
Bongo kweli hovyo na mikashfa yote ile lakini bado kapata na ubunge wenzetu nje wanaweza kukusamehe kama umepata kashfa ukiwa madarakani na utendaji wako ni mzuri lakini si kabla ya kupewa madaraka
ReplyDeleteEric,
ReplyDeleteJibaba umenena yote. Kuna watu ati wanasema wanawakilishwa, sijui nini tena vile. Bongo hatuna wabunge period. Watu wametumia pesa kuingia pale wakatafute pesa kwisha.
Na wewe anony unayemwambia benny78 kuwa elimu ya ndani ndio msingi embu acha maskhara. Sijui unasema nini, tutapendaje elimu wakati wafanya maamuzi ndio hao wasokuwa na elimu? Mapinduzi ya elimu yatakujaje wakati vyeti na degree feki ndio vinaongoza nchi? Mi simo na nasema Amina Chifupa haniwakilishi bali anajiwakilisha yeye na familia yake!
nimeshituka michuzi ana muonea huruma na anafuta comment nyingine. Usizifute ziache zote wazi nimeona comment kibao zimefutwa. hacha uhuru wa habari uendelee.
ReplyDeleteJamani sikiliza hii maanake ni kali mbavu sina sijui nyie wenzangu itakuwaje. Ni mazungumzo kati ya Sunche(Mtanzania mwenye asili ya kihindi) na biti(binti wa kitanzania)
ReplyDeleteSunche: wee iko itwa nani
Biti: Biti
Sunche: Wee iko maliza dasa la gani?
Biti : Form four
Sunche : We iko taka edelea na sule ?
Biti : Ndio nataka nisome mpaka form six and mlimani, univesity.
Sunche : Wee iko taka somea nini ?
Biti: nataka kusomea kitu kama uinjinia, Uhasibu au sheria-law.
Sunche: Iko engineer au asibu pata pasha kashi gani?
Biti: Kama Laki tatu, nne au tano kwa mwezi.
Sunche : Hahaaa dola gapi hiyo?.
Biti: Dola mia nne au mia tano kwa mwezi.
Sunche : Wee iko taka mimi, hina haja kwenda sule, mimi pesha ipo, iko peleka wewe buge na pata dola elsu mbili kwa mwezi na changingi lakini iko kaaa .......
Biti : ha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Sunche : Iko taka jimbo au viti malum.
Biti : Hai labda maalum
Sunche : Maalumu pitia pigiwa kura au wekwa tu pendeleo wee mmke
Biti : kama ni kupigiwa kura au upendeleo hiyo itakuwa juu yako make itatakiwa pesa ya kutoa.
Sunche : Pesha ipo kuna tatiso
Biti : asante thank you
Sunche : Iko taka pitia chama aaaani ?, which part
Biti : Chama cha bibi na babu zangu cha damu damu.
Sunche : Taka pata buge tu au na waziri.
Biti : aka !!!!!!!!!!!!!!, naogopa siwezi kukaa karibu na rais wa nchi, halafu ni mkali atanistukia na kunifukuza.
Sunche: aya fuata mimi chaguzio fika peleka we bugeni.
Biti: Asante, sasa bungeni nitakwendaje make hata gari sina?.
Sunche: Karabati wewe siwe shaka hata englisi media peleka wewe ongea zugu zuri toa hoja buge zungu. Siwe wasi na gari pitisa pale TRYA tumia wewe jina mesimiwa. Pata nafuu suru.
Haya kazi kwenu jamani hiyo ndo ilikuwa Tanzania au ndo Tanzania?.
Hiyo noma siyo mchezo
ReplyDeleteAMINA AMINIA KIBOKO YA MJI, WENYE KUSEMA NA WASEME WEWE KULA KWA RAHA ZAKO
ReplyDeleteKa Amina kazuri Jamani!!!!
ReplyDeleteZemarcopolo hilo ni suala zito mno.
ReplyDeleteZEMARCOPOLO,MEKANIZIM YA KWANZA NI VYAMA VYENYEWE KUCHUNGANA. NYINGINE NI MAHAKAMA HIYOHIYO AMBAYO IMEANZA KWA KUTAMBUA WAJIBU WAKE KUWA SIO KUONGOZWA NA SERIKALI BALI KUFUATA KATIBA.
ReplyDeleteJINGINE NI ELIMU YA URAIA KWA WANANCHI(AMBAO WENGI WANAFAHAMU NI KOSA KUPOKEA AU KUTOA TAKRIMA WAKATI WA UCHAGUZI ILA KWA UMASIKINI,UROHO,TAMAA,UJINGA WANAPOKEA AU WANATOA HIYO TAKRIMA)HAPO NI SAWA NA KUNUNUA/KUUZA HAKI YAKO YA MSINGI.
MTOA TAKRIMA NA MPOKEA TAKRIMA WOTE WANA HUKUMU MOJA MBELE YA SHERIA.
ILA HAKUNA JAMBO BAYA KAMA KWELI SERIKALI INATAKA KUKATA RUFAA KUHUSU HUKUMU HII YA HAKI HATA MBELE ZA MUNGU.SIO ETI KWA KUWA SHERIA INARUHUSU KUKATAN RUFAA BASI UKATE TU HATA KWA MAMBO YALIYO WAZI.WATAKAOKATA RUFAA MUNGU AWALAANI.
KWA KUWA DADA AMINA NI MBUNGE WA CHAMA KINACHOONGOZA SERIKALI,WAELEZE HAO WANAOTAKA KUKATA RUFAA WATAFUTE MAMBO MENGINE YA MAANA,TUMESEMA HATUTAKI RUSHWA KWELI IWE HIVYO POPOTE!LABDA KAMA TUNADANGANYANA.KAMA TUNAITAKIA MAPENZI MEMA NCHI YETU KAMA WAZEE WETU WALIVYOJITOA MUHANGA KWA AJILI YETU KATIBA IPITIWE UPYA NA KUREKEBISHWA INAPOBIDI NA TUIHESHIMU NA KUIFUATA HIYO KATIBA ITAKAYOZINGATIA MISINGI YA HAKI NA USAWA.
TUKUMBUKE MANENO YA BABA WA TAIFA,KAMA KWELI TUNAMUENZI.
ASAVALI TOPIC YA AMINA INAELEKEA UKINGONI MAANA TUSHACHOKA SASA
ReplyDeleteUMECHOKA NA NINI?HIVI UNA HAKIKA WOTE WANAMCHUKIA AMINA KAMA WEWE?ACHA ROHO YA KOROSHO,MWACHE DADA WA WATU!ZALI LIMEMWANGUKIA BASI!
ReplyDeleteWe uandikiae kwa herufi kubwa. Uwe unabonyeza shift ili kutoa hizo herufi kubwa then uendelee kuandikia. Herufi kubwa huwa zinatumika mwanzo wa sentensi!
ReplyDeleteSITAKI,KAMA HAZISOMEKI KWAKO ACHA KUSOMA."HERUFI KUBWA HUWA ZINATUMIKA MWANZO WA SENTESI!"HIVYO HIVYO EEEH!NDIO MWALIMU WAKO ALIISHIA HAPOHAPO!
ReplyDeleteANONY 3:59 AM,MBONA NATAFUTA HIYO SHIFT SIIONI?HAPA NAONA "CAPS LOCK"AU KOMPYUTA YANGU YA ZAMANI?
ReplyDeletenyie mmepagawa nini sasa mnafanya nini baada ya point, wazee wa nyanga kutoka mnajifanya kuchezea hapa toka kabisa. Mnachezea kwenye uwanja wa amina. Atawatungia sheria!!!!!! Amina wafunge hao wanacheza nyumbani kwako.
ReplyDeleteKWELI,SASA MWISHO NA DADA YETU APUMZIKE KWA AMANI......POISON,UTAONGOZA SALA YA KUFUNGIA MJADALA!
ReplyDeleteSumu tena mimi sioni kama hana sifa za kusoma sala atamumaliza dada yetu mpendwa mimi namuomba macopolo (menye rangiya bluu) labda.
ReplyDeletePoison ni asavwali kuliko Makopolo!Samtaimu anajificha kwenye anoni!
ReplyDeletemmechonga hadi mmechoka wenyewe mmbwa koko nyie,vpi comments zimeisha au?
ReplyDeleteAmina mbunge wa vijana wote tanzania.
ReplyDeleteMAKOPOLO naomba anwani yako na GIRILI natamani muwe rafiki zangu jamani huwa mnanichekesha sana.
ReplyDeleteNgoja tumechishe na idadi ya maoni kwa Amina,sasa basi!
ReplyDeleteYAANI KWELI HAMTOI MAONI KWA AMINA?NYIE WATU WA AJABU KWELIKWELI,HUYO NI MBUNGE WA VIJANA!Heeee!
ReplyDeletehaya watanzania kweli inaonekana kumekucha huko nyumbani.lakini mimi nachowezakusema nikuwa, elimu ni uwezo unao mwezesha mtu:
ReplyDelete1.kuyatambua mazingira halisi aliyomo.
2.kuyatambua matatizo yanayomkabili na kuyapanga kwa kutegemea uzito wake.
3.kubuni njia za haraka zamuda mrefu nazamuda mfupi zakuyatatua matatizo hayo.
4.kufanya upembuzi ni kwakiasi gani amefanikiwa kuyatatua,na nikwakiwangogani hakufanikiwa,kisha kupanga mkakati mpya kwa haraka bilakupotezamuda wakuyatatuatena.
kama mtuyeyote anao uwezo huo basi ana elimu.lakini kama hana basi atapaswakuutafuta iwe ni kwakuketi darasani ama kwanjia nyingine yeyote,ilimraditu aupate.
Swala la majungu nachukibinafsi vime kwamisha nchiyetu tanguzamanihizo,ndio maana hatukuendelea,wazungu,wachina ,wajapani nawahindi tunasomanao hapa lakini tunawashindapia darasani.
siriyao ya mafanikio ni discipline(adabu).yaani,kufanya jambosahihi kwa wakatisahihi unao paswa kulifanya bila kupotezamuda wala kuleta mbwembwe za longolongo.
tunalalamika umaskini lakini tungejua wenzetu wamepitia wapi hadiwakafika hapa,walatusingelalamika sisi tunayonchi yenyemalighafizote, ujinga,uvivu wakutojishughlisha kwa mikono na akili ndo vinatuangamiza.sio wabunifu kabisa,na tuna mitizamo mifupi yakuona hadi kiganjanitu ndomaana tutaendelea kuwa maskini.
nchi kamajapan mwalimu akifundisha mwanafunzi hatakiwi kuuliza swali,anachopaswa kufanya nikuwa makini nakutekeleza atakachofundishwa,kama jeshi!
si mnaona wanavyo endelea kwa kasi.
nchi nyingine nibarafutupu,jua linawaka miezi2tu.wasinge kuwa wabunifu si wangekufa njaa na kwa baridi.
wabongo majirayetusafi mwakamzima, ndomaana hatahivi juli niliona ktk tv moja hapa ulayawanaonyesha WAHADZABE WA ARUSHA(sijui ndo manyara kwasasa)wanavyo ishi kwakuokota matunda na kuwinda wanyama na ndege kwa mishale ya vijiti.
yani tunaishi kulakilichopo ushibe ulale uote huku unajamba,ukipata vijisenti kidogo uanawaza kunywa na mademu kisha tunawalilia wazungu AIDS inatuuwa tupeni dawa!!
wasomaji wahii blog, iweni chachu ya maendeleo nyumbani,hadi tutakapochoka na umaskiniwetu na ujinga,na maradhi tukaamua kila mtu binafsi akawa na mkakati wake ,kisha familia,mtaa,kijiji,kata,tarafa,wilaya,mkoa,kanda,hadi taifa.ndo tutaendelea.
vinginevyo tutaishia kulia,kulogana,kulalamika,kuwamaskini,kuugua,na mwishowe kuchukiana na kuanza kuuwana kwavita .huku wenzetu wanachekelea wanauzasilaha zao,tufe waje kuchukua ardhi.
watu weupe akilala ameshika kichwa,wakati ngozi nyeusi akilala ukono uko ktk nguo ya ndani,akiamka anawaza jiraniyangu hanitakii mema.
sina uhusiano na kina amina wala michuzi,lakini nayasema haya kutokana uchungu nao upata nikiona jinsi jamaazangu wanavyoteseka katika nchi ambayo haikupaswakuwa maskini.hata mtu akikuuliza we unatoka nchi gani ukisema TZ anaenda ktk internet,jibu atakalokuja nalobaadae, nihili:yni nchiyenu ni maskini kiasihicho?utarudi TZ ukimaliza masomo?mbona kuna kiwangokikubwa cha wagonjwa wa AIDS?
tuziduke jamani tuanze kufikiri kwa upana,ubunifu binafsi,na mawazo endelevu.
mwisho sijamlenga mtoamaoni yeyote,ila nimejikuta ktk hii blog leo ndomaana nikaona nimahalimuafaka pa kuwapeni nadukuduku langu hili.
asanteni.(mbongo mwenzenu)
jamani naendelea(mbongo mwenzenu).
ReplyDeletekuna watu wengi ambao wamekwenda darasani hadi chuo kikuu kama mimi,lakini ule uwezo wa kukaachini akabuni mkakati wa kumkwamua hata yeye binafsi anakuwa hanao, sasa una dhani mtu huyo ulikabidhi kundi la watanzania milioni5 ambao wamegubikwa na umaskini ili aandae mkakati wa miaka 5,kisha watu tuone mabadiliko ya jamii hiyo ya watu milioni5 ataweza? jiulize nawewe msomaji je ungekuwa ndo wewe nakuuliza hiliswali unaweza?
ukionwa na jibu la HAPANA ujue ndio taabu tulio nayo huko nyumbani.yaani watu walio soma lakini hawanaelimu(hawajaelimika).hata kama ana PhD kama hawezi kuitumia kumtoa yeye na kundi linalofuatana naye ktk dimbwi chafu akasogea mbele penye unafuukidogo basi elimu yake haijamsaidia.
cha msingi sasa tunze kujenga tabia ya kujiamini na kuwa na uwezo wa sikufikiri tu,bali na kuanza kutekeleza kwa vitendo japo walau kidogo yale tunayo fikirikuwa yatatukwamua.
tabia ya kulalamika inatufanya waafrika kuwamaskini,chukuwa mfano rahisitu,kijana kamaliza kidatocha 4,amepata div4,katoka kijijini kaja huko DAR kutafuta maisha,sasa anacho fanya nikuuza katika duka la muhindi nanalipwa Tsh40,000/= kwa mwezi.na analipachumba 15,000, umeme5000,sasa unategea mtuhuyu akiamua na wenzake wakaenda kule mukuranga wakaanzisha kilimocha matikitimaji kwa mwaka 1 akatumia nguvuyote pamoja na uduniwazana alizo nazo,hawekuwanatofauti kuliko kazi nayofanya ya kumtajirisha muhindi huku yeye anazeeka bila mwelekeo?
mimi nilianza hizo harakati ikawa imesalia wikimoja tu nianze jembe pale mkuranga,ndo inshalah mungu akanijalia scholarship ikatoka nikajahuku kusoma.sikuwa na mawazo ya kujivunga eti hikisiwezifanya maana mimi ni form6 na div.one!
tunapaswa kuwa flexible kwanyakatizinazofaa na zisizofaa.hata hapa utakuta kuna mtu mzima anakwambia mimibaba anapesa siwezi kujishughlisha,atanitumia na huyo ni kijana mtanzania ana miaka labda30.wakati wenzie tunachacharika na kufanyamambo bila kujali wazazi wetu wanafedha aula!kuelimika ni wewe kuanza kufikiri namna ya kujikomboa kwanza ili ukipata msaada kidogotu unakutoa au mnasemaje wa TZ wenzangu?
sasa simba huyo anakuja(umaskini,maradhi=ukimwi,njaa) acha usipande kwenye mti ubaki unalia eti serikali,yaani mambomengine ni aibu kabisa japo pia hata serikali ina wajibu wake kufanya kwa watuwake.
kijana hajafanikiwa kwendasekondari sasa abweteke eti kwakuwa hajapatacheticha f4?jisomee hata vitabu,majarida,ili upanue ufahamuwako.ukitizama tv nini unachoondoka nacho cha kukufanya upige hatua?au unaishia kutizama na kuondokatu?
hata magazeti,pamoja na kusoma ya udaku tusome na makalapia za kupanua akili na uwezo wa kufikiri.
watanzania niwavivu wakujisomea,na mambomengi na siri za maendeleo zimo ktk vitabu wasivyo taka kusoma,ndio maana sisi na viongozi wetu hatuzipati siri za maendeleo na hatuendelei.
ndugu zanguni nime ruditena(mbongo mwenzenu)
ReplyDeletehaya sasa yaleokalitena,mnaonaje tukimtuma mbunge wavijana akaiomba serikali kupitia wizara husika ikaanzisha mradi unao fanana na JKT lakini sio JKT,ukilenga kuzalisha mazao ya kilimo na mifugo kwa kutunia nguvu ya vijana wasio katika sekta maalum,wala katika sekta ya elimu.
yaani vijana wasio na kazi atachagu mwenyewe iwe mwaka mmoja au 2 anakwenda kuzalisha, serikali itenge maeneo,iwape na matrekta,navitendea kazi vingine,wazalishe,kisha serikali hiyohiyo inunue hayomazao yalozalishwa yatumike kupigha vita njaa badala ya kuagizatoka nje.kisha pato la fedha wagawiwe wazalishaji,atakayependa kuendelea aendelee,anayetaka kubadili na kuanza biashara atakuwa na kamtajikake.
hii isaidie kupunguza wapigadebe,wavutabangiwavijiweni,machangudoa na maambukizi ya HIV,vijana wa majumbani wasio na kazi kaziyao kula kulala. hii itapunguza hata wimbi la vibaka wanaokuw hawana chakufanya. pia katika makambihayo kutakuwa na waalimu wa kutoa elimu mbalimbali nyakatiza mapumziko.
hii inaweza kusaidia kuwa wanya washughlishe ubongo.maana kuna msemo usemao"ubongo usio jishughlisha ni karakana ya shetani" unaanza kuwaza maovu ya kuichafua jamii.
serikali ikikubali ikafanaufanyia majaribio ukafanikiwa,iwe ni lazima kwa kijana yeyote asiye nacha kufanya kinacho eleweka apelekwehuko lakini kila mwisho wa mwaka alipwe malipo sawakabisa na uzalishaji bila dhuluma na kunyonywa.na watalaam wa kilimo na mifugo watumiwe hapo kuonyesha uwezo waowa uzalishaji.
roma haikujengwa kwa siku moja,tumpeni muwakilishi wa vijana mawazo endelevu apeleke serikalini,tuache kupiga kelele maana haitatokea siku wote twende tuka iambie serikali fanyahili.tuache lawama hazijengi bali zina katishatamaa na kubomoa.
kunajambo aliwahi niambia rafikiyangu mzungu mmoja ambaye ni mmiliki wa ule mgahawa wa steers hapo bongo,kipindi hicho nilikuwa bado mdogo niko form2 naye alikuwa mkurugenzi wa shirika fulani hapo tanzania,ambalo katika siku zijazo nta litoa hapa linaweza kutusaidia pia wabongowenzangu.sija lisahau hadi leohii nipo chuo kikuu.
zubeda.
ReplyDeletenikweli kabisa namuunga mkono huyo( mbongo mwenzetu) kwa changamoto alizozitoa, ni kweli umefika wakati sasa watanzania tuamke kisha tufikiri kwa upana na kupeana mawazo endelevu.
kweli uvivu wa kutenda,na wa kufikiri ndio aduiwetu namba2, huku namba moja akiwa ni kukata na kukatishana tamaa kuwa hatuwezi leta mabadiliko kama tukinuia kuendelea.tujitume kama askari aliyevitani akijua kuponakwake ni kumuua adui.
nduguyangu mbongo mwenzetu unamawazo mazurisana yanayo leta ujasiri na kujiamini kwetu vijana ilitujikwamue wenyewe kila mmoja kwanguvuyake kwanze kabla ya kusaidiwa.