jk akitembelea magereza ya dar leo. bahati mbaya/nzuri wapiga picha hawakuruhusiwa kuingia ndani. ila kwa nje wafungwa walisikika wakimwimbia jk kwa shangwe na vifijo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2006

    magereza ya bongo hayafai kuishi binadamu ndio maana mmezuiliwa kuingia, wanaficha ili dunia isione kinachoendelea humo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2006

    Michuzi naomba utuwekee picha ya KINJE-KITILE NGOMBARE MWIRU,nasikia ni mmoja wa vijana anayesumbua sana watu hapo dar. Na pia nasikia anamiliki disco ambalo watoto wa vigogo wenzake wanakwenda kwa kulipa kiingilio cha hali ya juu,nasikia hilo disco ni kama uwanja wa mpira wa karume. Sakafu zina vumbi kama nini.(Na pia hile tabia yake ya kutishia watu pisto kaacha na kuingiza madawa ya kulevya nchini)

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2006

    I am kwakweli very impressed with JK's speed as a president. He is doing what hasnt been done and he is going where no body dared. I pray for him that the almight rescue him from bad hands.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2006

    issue hii ni sensitive. Kuna majambazi ambao si tu wanaiba bali pia wanaua watu hata baada ya kuwaibia, hawajui hata 'ethics za robbery', sidhani kama serikali itumie pesa ya nchi kuwajengea mahali pazuri pa kuishi wakati wa vifungo vyao watu kama hao.

    ReplyDelete
  5. Zemarcopolo umesema kweli, siku nyingine watumie hata simu za mkononi kupiga picha maeneo hayo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2006

    Askari wenyewe hawajui haki za binadamu maana yake ni nini. Kama wangejua dunia nzima ingejua nini kinachoendelea humo ndani. Si tunaona Guantanamo kila siku? si tunaona Al-ghaib kila siku? kwa nini isiwe Ukonga na Segerea?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2006

    Wajameni, kwa mujibu wa habari iliyochapishwa nipashe hivi leo, mfungwa mmoja anagharimu serikali shilingi 2500 kwa siku, hebu zidisha mara 30,, hata kima cha chini ya mfanyakazi wa serikali hakifikii. Sasa sipingi hilo suala ni kwamba, hawa wafungwa wanazalisha kitu gani? tumeshuhudia wengi wao hasa pale ukonga wakiishia kujenga nyumba za wakubwa. wanalishwa na serikali, wanajenga nyuumba za wakubwa. Kwa nini wasizalishe kile wanachokula? kuna mapori, kuna ufugaji? wakubwa wamekalia kujinufaisha wao tu bila ya kubuni mikakati ya kupunguza mzigo wa walipa kodi katika kulisha wahalifu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2006

    Anonymous hapo juu, hicho kiwango cha mfungwa mmoja anatumia TShs 2,500 kwa siku utakuta ndio kiwango kinachoonyeshwa kwenye vitabu vya mahesabu wakati Magareza na Wizara husika zikiwa zinaandaa bajeti zake.

    Kuna uwezekano mkubwa kwamba gharama ya mfungwa mmoja ni chini ya TShs 500 kwa siku, hiyo ikijumuisha mlo, malazi, maji, umeme, mavazi nk! Hawahitaji usafiri maana hakuna wanakoenda!

    ReplyDelete
  9. Nakuunga mkono anyonymous uliyesema kua kiwango halisi wanachotumia kwa siku ni 500.

    Hizo 2000 tumuulize chiligati na Banzi zinakwendaga wapi?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 05, 2006

    hii rangi inaonekana jinsi ilivyo mbichi.....itakuwa imepakwa jana yake!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2006

    Anyony na fikrathabiti,
    Hiyo ndiyo kweli yenyewe, mtu aliyeko mtaani pamoja na milo mitatu na gharama zinginezo anatumia chini ya 1000 iweje hawa wafungwa watumie zaidi kwa kipi hasa? Tunajua wanakula mlo mmoja wa ugali na maharage yasoungwa ambao kwa hakika hata kugharimu sh 200 (mia mbili) ni mukhari, na asubuhi uji uso sukari. Tuelezwe mchanganuo wa hizo pesa sio hesabu za juu juu tu!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2006

    Askari wenyewe hawajui haki za binadamu maana yake ni nini. Kama wangejua dunia nzima ingejua nini kinachoendelea humo ndani. Si tunaona Guantanamo kila siku? si tunaona Al-ghaib kila siku? kwa nini isiwe Ukonga na Segerea?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2006

    Michuzi wewe ni kiboko kama hamkuruhusiwa kuingia kaka hii picha uliinasaje. Utatuwa kwa maraha keep it up na ubarikiwe sana

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 06, 2006

    we hawakurusiwa kuingia ndani huoni picha aliyopiga hii ni nje, kweli aliye na macho haambiwi ona

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 08, 2006

    michu sijui kama wewe ni kachero au mpiga picha wa gazeti la serekali.hebu tueleze mbona waziri pesa mbili mramba anabebeshwa lawama za POMBE magufuli?waziri aliyekuwa anaonyesha cheche zake nakuonyesha uzalendo wa hali ya juu kabisa wakati wa awamu ya uwazi na ukweli.yeye ndiyo wakuulizwa yakuwa kwanini alitu ahidi kuwa kabla ya rais mkapa kumaliza uongozi wake mtanzania ataweza kutembea kwa taxi kutoka bukoba hadi lindi.wakati siyo kweli.akazuia maboti kupelekwa mwanza kwa shinikizo yakuwa madaraja na barabara zitavunjika.mbona hizo barabara na madaraja za kenya haziku vunjika.kumbe alikuwa anatu danganya.sasa leo imegundulika kuwa hata hiyo barabara ya lindi amempa kazi M A KHARAFI isiyekuwa na ujuzi wa kujenga barabara hata siku moja.ilikuwaje tunashaka alikatiwa ndio maana akatoa hiyo kazi.leo waziri mramba analaumiwa.mshikeni huyu pombe atueleze ukweli.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 10, 2006

    Kiwango cha gharama ya kumtunza mfungwa ni sawa na allowance ya mwanafunzi chuo kikuu (Kula, kusafiri na kuhakisha anapata mahitaji mengineyo) na hawaipati mpaka wagome!!!!!!! Hii ni mpya!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 10, 2006

    Ushauri mzuri wa wanachuo kikuu, fanyeni makosa ili mfungwe jela kwa sababu wafungwa expenditure yako inawazidi wanapata huduma bila matatizo

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 13, 2006

    UZURI WA GEREZA NI LAZIMA UENDANE NA MAISHA YA RAIA WA KAWAIDA!MIE NAONA BADO WAMEJITAHIDI!RAIA WENGINE URAIANI HAWANA HATA DAWA,CHAKULA,MALAZI,ULINZI MADHUBUTI NYIE MNAPIGIA KELELE MAGEREZA!KUYABORESHA MAGEREZA KABLA YA URAIANI KUNATAFSIRI NINI?YAANI UHARIFU UONGEZEKE ILI KUISHI MAISHA YENYE NAFUU YA UHAKIKA WA CHAKULA,MALAZI NA ULINZI!WE UMESIKIA HATA SIKU MOJA HAO JAMAA WAMEVAMIWA NA MAJAMBAZI?SI WANALINDWA?MAISHA YA RAIA WENGINE YAKIBORESHWA NDIO"LABDA"MAGEREZ YAFIKIRIWE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...