jk alipotembelea soko la nafaka la tandale

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2006

    Michuzi samahani kwa kuandika hii habari hapa,kuna habari nimeisoma kwenye nipashe la leo asubuhi kwenye mdaharishi wao.I nasema kwocha msaidizi wa chelsea amekuja nchini kuja kuongea na Jamaa wa TFF...Kwenye timu ya chelsea hakuna mtu kama huyo ambaye anajiita Jeff Bookman. Hawa jamaa watakuwa matapeli na wanakuja nchini kwetu kutapeli naomba uwezu kuliwasilisha hili jambo kwa mwandishi aliyeandika habari Majuto Omary. Na kwa ushaidi mzuri jina lake hata kwenye website ya chelsea halipo na mimi pia nimfanyakazi katika hotel moja ambayo wachezaji na viongozi mara nyingi wanafikia hapa chelsea sijawahi kumsikia huyu mtu na wala hayupo chelsea...Naomba uweze kumfahamisha huyu mwandishi wa hii habari kama utakuwa unamjua

    Kocha wa Chelsea kuteta na Stars leo

    2006-05-03 09:03:35
    By Majuto Omary


    Kocha msaidizi wa mabingwa wa soka wa England, Chelsea, Jeff Bookman aliwasili nchini juzi na leo atazungumza na uongozi wa Shirikisho la Kandanda la Tanzania, TFF, na wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars.

    Bookman amewasili nchini akiongozana na kocha wa timu ya watoto ya Tottenham Hotspurs, Ose Aibangee kwa mwaliko wa kampuni yenye lengo la kusaka wachezaji wenye vipaji hapa nchini, Global Scouting Bureau (T) Limited, GSB.

    Makamu wa Rais wa GSB, Jack Pemba alisema jana kuwa makocha hao watawasilisha programu ya miaka mitano iliyoandaliwa na kampuni yao kwa TFF yenye lengo la kuiwezesha Tanzania kushiriki katika mashindano ya Mataifa ya Afrika ya mwaka 2008 na vile vile Kombe la Dunia.

    Pemba alisema kuwa mbali ya programu hiyo, makocha hao watazungumza na wachezaji wa timu ya taifa jinsi ya kuwa na wachezaji wa kulipwa na mambo mengine mengi ya kiuchezaji.

    Alisema kuwa pia watazungumza na TFF kuhusu jinsi ya uanzishwaji wa mipango endelevu ya timu za watoto, elimu kwa makocha na mambo mengine mengi muhimu kwa maendeleo ya soka la Tanzania katika mkutano huo uliopangwa kuanza saa 6:00 mchana.

    Msemaji wa TFF, Florian Kaijage amethibitisha hayo.

    Alifafanua kuwa makocha hao wana uhusiano mzuri na kampuni yao na ndiyo maana Bookman ameamua kuachana na sherehe za ubingwa wa timu yake na kuja nchini kutoa mada za maendeleo ya soka.

    Kwa mujibu wa Pemba, GBS itaendesha mpango wa kusaka wachezaji chipukizi na kuwatafutia masoko nje ya nchi, mbali ya kuunganishia wachezaji watakaokuwa na mpango wa kwenda kucheza soka la kulipwa.

    Alisema kuwa Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, lakini hawajijui na kujikuta wanaishia kucheza hapa hapa nchini.

    ’Lengo langu ni kuendeleza soka la hapa nchini, na kazi ambayo nimeifanya kwa muda nchini Marekani na Uingereza na wachezaji kibao wamefanikiwa,’ alisema Pemba.

    Kampuni hiyo inatarajia kukusanya jumla ya wachezaji 440 ambao watatafutiwa masoko nje ya nchi katika mpango wake maalum ambao utakwenda sambamba na kuwaendeleza kielimu.


    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2006

    hIYO HAPO CHINI NDO LIST YA MANAGEMENT YA CHELSEA MPAKA JANA WAKATI ANACHEZA NA BLACKBURN...Na hii ndo imekuwa list ya management kwa season nzima ya league hajaondoka mtu wala kuongezeka

    The Management

    Jose Mourinho (Manager and First Team Coach)

    Baltemar Brito (Assistant Manager)

    Steve Clarke (Assistant Manager)

    Silvino Louro (Goalkeeping Coach)

    Andre Villas (Assistant Coach/Scout)

    Rui Faria (Fitness Coach)

    Ade Mafe (Assistant Fitness Coach)

    Mick McGiven (Reserve Team Coach)

    Brendan Rodgers (Youth Team Coach)



    Medical Department

    Bryan English (Chief medical officer)

    Dean Kenneally (First Team physio)

    Mike Banks (Reserve Team physio)

    Alex Nieper (Reserve Team Doctor)

    Ian McCurdie (Rehabilitation Doctor)

    Thierry Laurent (Rehabilitation)

    Rob Brinded (Rehabilitation)

    Billy McCulloch (Masseur)

    Stuart Sullivan (Masseur)

    Mauro Doimi (Masseur)

    Pedro Phillipou (Masseur)

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2006

    wee chizi nini Utaandikaje habari za kocha wa Chelsea ktk mambo ya JK NA NJAA BONGO??

    Regards
    Chupaki

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2006

    Wewe ni mpumbavu sana,soma vizuri post ya kwanza imeandikwa nini kwanza,jamaa kaanza kwa kuomba samahani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2006

    nyie ndo mnaodanganywa tz? huyu mtu ameomba samahani hapo juu kwanza nashukur sana na napenda sana kukupongeza ndugu yangu uliyeweza kuwafumbuaa watz maana tumezidi sie kudandia kila kitu ndo maana hata mikataba tunayoletewa tusaini tunasaini tu hatusomi yalio ndani au hata tukisoma tunafumbia macho ni ujinga tuu.

    safi sana kijana umefanya kazi nzuri

    Kikwete naona ana bidii yahali ya juu sana kufanya anayofanya lakini mbona kila siku dar tuu aende kule kijijini kwetu uhambule,kila siku tandale,manzese.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2006

    Anons wa saa 6:37 na 6:43,
    Yaani kuna watu kwa kujifanya wanabusara acheni tu inakera sana. Mtu anakurupuka tu na kuanza kumwita mtu chizi wakati vitu alivyoondika ni vizito mno. Hiyo habari ya huyo ndugu ni nzito mno ingeweza hata kuingilia hotuba ya Kikwete ya Mei Mosi achilia mbali kuingia kwenye habari ya Kikwete kutembelea Tandale. Ni ajabu kuona mtu anamwita chizi mtu ambaye anatufumbua macho watanzania tusifanywe wajinga. Samahani Bwana Michuzi, lakini kwa sababu unaweza usipite hapa tena mpaka baada ya siku tano naipost hiyo habari huko juu ili uweze kumpata huyo Majuto Omary. Ndio raha ya blogu: kupashana habari siyo kutukana

    ReplyDelete
  7. kwa taarifa yako napita humu kila siku mara tatu, kama mlo. nashukuru kaka kwa kututonya, naifanyia kazi mada yako, na asante sana. wito ni kwamba mtu asiogop kusema lolote na popote humu bloguni, kwani kuna wakati mada inakuwa tofauti na mawazo ama nia ya kusema kwa wakati uliopo bloguni. hivyo hamna noma, sioni kama jamaa kakosea...vile vile nakaribisha mtu kunitumia ujumbe, hasa wa picha yake, kusabahi ndugu na jamaa. tuma kwa kupitia issamichuzi@gmail.com, nitaibandika humu chap chap.

    ReplyDelete
  8. Huyu ni kocha wa Chelsea FC Academy sio ile ya Premier League

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2006

    Mwaipopo umenichekesha sana ..........that is fun !

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2006

    Michuzi vipi hali ya chakula nyumbani. Manake hapa U.S.A tumepata email on the behalf of Balozi tuchange pesa kwa ajili ya kusaidia NJAA NYUMBANI. Pesa zitakabithiwa President Kikwete atakapokuja hapa later this month.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2006

    WE CHANGA HELA(KAMA UNAJALI KWENU)KWANI WALIOKWAMBIA HUKUWAULIZA HADI UMUONEE MICHUZI KWA KUWA KAJITOLEA KUKUGEA HABARI ZA KWENU BERE?AKIKWAMBIA UKOO WENU PIA UNA NJAA NDIO UTACHANGA!?TOA NDUGU,TOA NDUGU X2 ULICHONACHO WEWE....ANAKUONA MPAKA MOYONI MWAKO!WEKA MASWALI KIKWETE AKIJA UMUULIZE!WAAMBIE NA WALE WANAOTAKA TANZANIA IWE NZURI KAMA MAREKANI HUO NDIO MUDA MUAFAKA WA KUTOA HOJA HIYO KWA PRESIDAA!SIO KUJAZA KERO ZAO KWENYE BLOGU YA MICHUZI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...