...hata hivyo ziara iliisha vizuri na wazee waliweza jionea jinsi hoteli hiyo ya kitalii ilivyopendeza. hapa ni ghorofa ya saba kwenye prezidensho swit

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2006

    daktari wa mkapa anafanya kazi gani kama mkapa anaendelea tu kuwa mnene namna hii?au mkapa ndio atoi ushirikiano kwa daktari!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2006

    hiki ndio kile chumba rais akigombana na mkewe anakuja kulala. jamjuah

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2006

    hapo kikwete anatamani kumsukuma mkapa dirishani lol.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2006

    Jk kuna sehemu nyingi bado zinatakiwa kuangaliwa vijana wanalia ajira kuna ofisi tena za serikali na mashirika ya umma. kama watendaji wake wamesoma nafikiri hawakuelimika. Fikiria shirika kama tanesco, naomaba uwaulize Engineer wa mwisho aliajiliwa lini. Je umeme hauuziki. Ni proposal ngapi za kuendeleza tanesco wamefanya. naomba mashirika kama hayo ilituendane na kasi yako wazee wapumzike kwanza watafutwe vijana ambao wana ambisheni ya kushindana na ulimwengu waongoze mashirika hayo. Kuongoza shirika ni utaalamu siyo siasa jamani we need creative people. Watu wawe wanatoa summary ya mwaka amefanya nini kwa mwaka mzima na ametumia nini. Vinginevyo hatutafika

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2006

    Kwa hiyo Jk asichungulie sana dirishani badala yake awachungulie mashirika na watendaji au vipi?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2006

    Naunga mkono hilo la kwamba achungulie mashirika ya umma na ofisi za serikali.Yaani wakuu katika taasisi hizo hawaendi na wakati kabisa, nafasi za ajira za miaka ya 70 na 80 ni hizo hizo, wakuu hao wanahofu kuajiri vijana kwa kuwa watachukua nafasi zao, lakini kwanini hawabuni nafasi mpya za kazi na kupanua huduma za mashirika? Hivi kweli leo hii, mtu amejenga nyumba, fundi umeme unatafuta mwenyewe, kwa nini TANESCO isiwe inatoa huduma hii, mtu unaenda kuchukua fundi tanesco na kulipa shirika.. badala ya kusubiri ufungiwe na fundi wa mtaani halafu TANESCO wanapokuja kukagua wanakueleza kuwa nyaya darini zimetandazwa hovyo, unaingia gharama upya? taasisi kama RTD/TVT ndo kabisa wamelala, hata tovuti hakuna, habari ukisikia redioni ni za nje tu, hivi habari za wananchi hakuna? Kwa nini hakuna ubunifu jamani? naamini kuwa katika maendeleo haya ya sayansi na teknolojia fursa za ajira zinakuwa nyingi zaidi na si finyu kama ambavyo wakuu katika taasisi hizi walivyo na hofu! kitendo hiki kinakwamisha huduma kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa jumla! JK katika kasi yako ondoa hao wabinafsi wenye hofu kwa ajili ya matumbo yao!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2006

    Tatizo la nchi yetu bado uchumi unategemea siasa mno. Suala la JK kushughulikia mashirika ndugu hizo ni ndoto. Tumezidi kubebana mno bila kuangalia ability na capacity ya mtu unayembeba. Usiasa siasa umezidi sana Tz, hatuangalii uzalishaji wala nini zaidi ya siasa. Kuna lobbing nyingi mno kwenye mashirika yetu, we shirika kama TANESCO bado linategemea ruzuku kutoka serikalini wakati linakamua wateja wake ile mbaya na linajiendesha kibiashara. Mie nadhani tuliwatimua wakoloni mapema mno na tukajidai tunaweza kujiendesha wenyewe.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2006

    Hili swala na wafanyakazi toka miaka ya 1967, ataleta maendeleo gani .....kama mwetu alivyo sema hapo juu, wachague watu wapya wwith new ideas......Circut ya 1967 sio kama ya 2000.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2006

    grill nakubaliana na wewe, ila ktk jambo la wakoloni hapana.ila cha muhimu ni kuacha siasa nyingi,tunaitaji vitendo na changamoto sio sifa na kujipendekeza.
    sijapata sikia nchi inayomsifia raisi wake kama bongo,kwanini?
    tumsaidie lakini sio kumsifia, sifa ni kitu kibaya,bado ana miaka kumi mbele,
    anafanya vizuri ndio,tunajua tumpe changa moto na sapoti.
    mliopo huko ughaibuni nitajieni ni nchi inayofanya hivyo.
    wansi tutakapokuwa na demokrasia ya kweli kuanzia vyombo vya habari ,wabongo tutaona mbele.
    kuhusu wakoloni ni kwamba hakuna anayependa kutawaliwa hata kwa siku moja.jj

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2006

    Bwana Mzee wa juu siyo kumsifia jk ni kumpa moyo na kukubaliana naye kwa yale anayoyafanya. Wote hatuwezi kuonekana kama tunamsaidia. Kumsaidia nipale anapokuwa na kizingiti tukapiga kelele kwamba kweli ondoa na kikaondoka, hiyo ndo kusaidia. Usitegemee kuzalia leo ukatambaa, halafu ukakimbia. Ukipata mtu anayekuwezesha angalau kusema kidogo baadaye sauti itasikika. Juzi umesikia takrima imeondoka, Tikila kashinda kale ka kesi ka mwaka 1993. Talatibu mzee kasauti sasa kanaanza kutoka. Turudi kwenye mada kumsaidia JK ni pamoja na Uwajibikaji katika mashirika ya uma. Tumelala mno wazee wetu wameishazoea kwenda ofisini kusaini makabrasha na kurudi nyumbani. Namna hii ukiona ni kijana unafanya hivi jua unajimaliza mwenyewe, hivyo imefika wakati kufanya mabadiliko makubwa kabika mashirika yetu. Kama walivyosema hapo juu hiyo siyo siasa. Sasa hivi shirika kama Escom South Afrika(Hii ni kampuni kama TANESCO tanzania) imeisha kuwa Multi-National. Kitengo tu cha Luku ndani ya Escom ni kampuni tosha yenye waandisi wa kila aina, mameneja na wakurugenzi. Pia ina watu wanakaa vyuo vikuu wanafanya tafiti kuhusu matatizo ya mita zao, pamoja na jinsi ya kuziuza Tanzania. je Tanesco ya Tanzania na mashirika mengine ya serikali ni lipi limeweza kuwa na kampuni ndani ya kampuni na ikakua?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 08, 2006

    Hivi Tanzania huyo wa kufikiria kuendesha shirika kwa ajili ya kuzalisha profit baadae yupo wapi? Huo wakurugenzi na wenyeviti wana umri gani ili wahangaike kufikiria future. Wao wanaangalia leo watakulaje wewe unazungumzia shirika ndani ya shirika for the benefit of whom? Uongozi kwenye mashirika mengi Tz ni uozo mtupu hakuna anayefikiria kuzalisha zaidi ya kujaza matumbo yao. Ndio maana wataalamu wengi wameishia ugaibuni hata kwa kufanya kazi za kubeba Mabox. Kazi Tz inauzi we acha tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...