nipo na mabosi wangu wa deiliniuzi tukitoka nyumba ya sanaa kwenye hafla. toka kulia ni mhariri mtendaji seth kamuhanda (sasa ni mwandishi hotuba wa rais), mkumbwa ali (kaimu mhariri mtendaji sasa) na nyuma ni mwandishi mwandamizi na bingwa wa habari za kichunguzi, charles kizigha.

ndugu zangu kina ndesanjo, jeff msangi, makene, mark msaki, da mija, mwaipopo, mk, na wengineo naona mnaogopa hata kutoa maoni, ingawa najua mwanitembelea. najua mnakerwa baadhi ya wana blogu wenzetu ambao hawana lugha aali, kiasi cha kufanya maoni ya maana toka kwa watu kama nyie yakosekane.

kuna ndugu yangu (jina kapuni) kasema hiyo inatokana na wivu wa baadhi ya watu ambao blogu zao zimevunda kwamba kwa nini mie nitembelewe na watu wengi kiasi hiki; kwani mie nani?

sina ubavu wa kukubali hayo ya huyo ama kuyakataa, kwani kama alivyoimba bitchuka, duniani kuna mambo.

waraka huu ni kuwaomba msiogope kuwa nami kwani wote jahazi hili tumelijenga wenyewe, hivyo endapo wimbi na papa visitutenge bali vitupe nguvu na kuzidi kuwasiliana hata waseme nini.

naomba kuwasilisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2006

    Michuzi wenye wivu wajinyonge,kwanza kwenye kila website ya kibongo niingiayo nakuta kuna link ambayo inakuleta kwenye hii website...Hii yote ni kwasababu ya kazi nzuri ufanyayo ya kutuwekea masnepu ambayo yanaeleza nyumbani kuna nini...Kama hao jamaa zako wana wivu waache na achana nao...Kama glob zao hazitembelewi basi haina maana kwamba wakuonee wivu kisa wewe unavuta watu wote...Watu wanakuja kwako kutokana na kazi nzuri ufanyayo na pia asiyekubali kushindwa si mshindani.Na mimi nahisi hao wenye lugha chafu ni hao hao jamaa zako hasa mwaipopo na msaki

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2006

    Kikulacho Ki nguoni mwako, hii methali ina maana sana.

    ReplyDelete
  3. Michuzi nadhani utakuwa unakumbuka msemo wa kiswahili usemao: "Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa kilio!"
    Kila jema lapaswa kujengewa mhimili na kulihifadhi bila kujali vikwazo vinavyoweza kumkuta mtu anayeweza kuona umuhimu wa kuhifadhi jambo jema! Si wakati wote macho yetu huona, lakini si wakati wote tunakuwa vipofu. Jamii yetu katika Magazeti Tando bado ni changa sana na siku zote tupo katika harakati za kuitanua iongezeke na kuwa kama mchanga wa ufukwe wa Koko pale Dar es Salaam. Bado hajujatosha kujaza timu yetu na tungependa tuongezeke zaidi na zaidi. Lakini kabla hatujajaza upwa wa bahari tunatakiwa kujijengea namna ya kujiendeleza kuliko kujibomoa, Je tunaweza kufanya hivi? Jibu rahisi ni kuwa tunaweza na ndio maana hata sasa tunapongeza jitihada za Azimio la Dodoma lililopitishwa hivi karibuni na wengi wetu kuliunga mkono!

    Hatujavunjika moyo kabisa na kauli hasi za baadhi ya wachangiaji lakini sasa zinavuka mipaka! Sikubaliani na udhaifu wa hoja kuwa binadamu tumeumbwa tofauti na kuiacha imeze ukweli wa kuwa hakuna asiyethamini utu wake? Kama tumeumbwa tofauti iweje huyu atumie njia za kujificha katika kumtukana mwenzake ambaye hakuwahi kumfahamu, au hakuwahi kuwa naye katika mashindano ya kutukanana na kuvuana misingi ya haiba ya utu?
    Kunahitajika ruwaza mpya iweze kubaini kuwa tuna watoto ambao sasa wanasoma magazeti tando ya baba zao au nao kutafuta maarifa yasiyosiganifu ili kukuza uelewa wao. Yaani hata hawa hatuwathamini kabisa? Ni lini tutatambua kuwa yale unayopenda kutendewa ndiyo watakiwa kuyafanya kwa mwenzako?

    Nilikushukuru juzi kama ambavyo nimewahi kufanya baada ya kutuwekea hotuba za Rais wetu, niliiisoma yote kila neno na kuweka maoni yangu bila hofu. Nilifanya vile nikitambua kuwa hapo ni uwanja ambao sitatukanwa, sitabezwa wala kudhalilishwa kabisa! Je hotuba ile ni hirizi kwa wanaotoa matusi na je kwa nini magazeti tando yenye habari kavu hayana matusi ya aina yoyote? Kuna jibu jepesi naweza kulipata hapa, aina ya maudhui, maudhui mepesi ama lugha nyingine maudhui chapwa! Jamii yetu imependa mambo mepesi mepesi tangu zamani, inathamini kuwa mambo magumu ni ya tabaka fulani tu na fikra hizi na nyingine zimechangia kutufikisha hapa tulipo katika Tanzania na Afrika! Vijana wa X-Plastaz wameimba wimbo mpya waitwa NINI DHAMBI KWA MWENYE DHIKI? Wote hatujawa matajiri wa urazini na hatutaweza kuwa hata sasa, kwa nini tukipambane kuchota maarifa na kugawiana taarifa chanya za kutunufaisha sisi kama umma na badala yake tukimbilie kukwamishana, kutishana na kuogopeshana!

    Azimio la Dodoma lilijadili suala muhimu la kuhamasisha jinsia ya Kike kufungua Magazeti Tando. Hadi sasa ni watatu watanzania waliodumu sana na mmoja amekuja hivi juzi ana makala moja tu! Sasa hawa wanapofika kuchangia na kisha kukabiliwa na matusi ya kuvuliwa nguo unatarajia nini maumivu ya kutumia akili na nguvu zako kununua jeraha? Sidhani kama jeraha hili linaweza kutibika haraka lakini pia unadhani akina dada na mama zetu wengine wanaweza kujjitokeza kufungua magazeti tando na kutuongezea maji katika kisima cha fikra tunachokikimbilia kunywa baada ya kuona hali hii iliyopo sasa?

    Michuzi niliposoma hoja hii, niliinama chini kilio nilikiacha moyoni lakini nilishajiambia kutokata tamaa kutoa nafasi ya maoni yangu pale ninapoona jambo fulani linaweza kupoteza dira ya makusudio ya wengi. Sitaogopa kabisa kufanya hivi maana naamini kuwa natenda nafasi yangu na sitahukumiwa kwa kukaa kimya, lakini tena unapotimiza wajibu wako na kutoonekana faida yake ni lini mwisho wa wewe kuhitimisha kuwa umetenda na hivyo kuchukua mhimili mwingine? Hapa ndipo nafikia ile methali niliyoitumia wakati naanza kuchangia hoja, tunajifunza nini kuhusiana na mchezo wa karata hasa pale mchezaji mmoja akikakataa kucheza karata yake? Je Profesa Kezilahabi hakuwahi kuandika kuwa "Sisi kwa sisi tukilana je lazima safari iendelee?" Kwa nini tusiamini kuwa tabia hii inatukera wewe unayetukana na mimi ninayetukanwa! Kwa nini basi tusikubali kusema mabadiliko yanawezekana na kujenga jamii safi inayothaminiana na kupendana!
    Nikamilishe waungwana kwa kusema "inawezekana cheza karata yako!"
    Niombe radhi kwa niliowakwaza na mchango wangu huu.

    Komredi Makene.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2006

    Makene ndio maana wenzio wanakutukana, unajifanya mjuaji sana. Kumbe hakuna lolote la maana unalolijua. Pole sana

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2006

    huyu mtu wa musoma wa nini?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2006

    jamaa tujifunza kuvumiliana,matusi ni aina mojawapo ya kuwasilisha ujumbe.tukisema freedom of speech hiki ndicho tunachomaanisha.tukimuona mwanablog mwenzetu anawakilisha hisia zake kwa kutukana basi tumueleweshe kwa hoja ambazo zitamfanya akubaliane nasi sio tu kumwambia ACHA MATUSI.

    ReplyDelete
  7. Michuzi,

    Kutembelea hatuwezi kuacha na tutaendelea kutoa maoni yetu siku zote.

    Usipofika ktk hii tovuti utakwenda wapi? Hapa ndio kikomo chake hivyo daima ni lazima kuweza kutembelea.

    Tunashukuru kwa kila kitu na mchango wako unaonekana kwa jamii.

    Tusikate tamaa kwani safari ni ndefu, na wale wote wenye mafanikio duniani ni wale wanao pigana kimaisha ata kama ni magumu kwa namna gani.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2006

    huyu makene bora ajinyonge tu, tena kwake kwaenda kilio,sio shujaa kabisa,
    anajaza blog huyu.khaaaaaaaa anakera sasa we unaandika yote hayo? huchoki? unafikiri nani atasoma? khaaaa andika kidogo tu bwana,
    nyie ndio mkikaribishwa kwenye pati mnakula mpaka kupasuka kaa manenge na mandawa.
    samahani kaka ila tabia yako inakera!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2006

    Wa-Tanzania bado tuna safari ndefu!

    ReplyDelete
  10. M.I-Michuzi,mzee kazi unaifanya - tena nzuri sana. Pamoja na kuwa si kila siku mtu unakuwa na hoja... kwa baadhi yetu, siku haipiti bila kukupitia mara mbili mbili (Asubuhi na jioni - kama dawa); hivyo mzee wee endelea na kazi nzuri unayoifanya.
    Kuhusu matusi... laiti kungekuwa na namna ya kuzuia watu kusaini kama "Anonymous"! Wakati ambapo tatizo ni watu wenyewe, nadhani uwezekano wa kusaini kwa kujificha ficha - kuna changia kwa kiasi kwa watu kujisikia kama vile hawezi kujulikana - kama mtu mwamba kwa nini asisaini kwa jina lake?
    Ama kwani kuna ugumu gani kutoa hoja bila kutukana? Au matusi ndio njia mpya ya kuongeza uzito wa hoja? Kama mtu hutapenda kuambiwa (kuandikiwa) unachomwambia mwenzako - kaa kimya! Ukimya wako unaweza kuwa na faida mara millioni.
    Muhidin, kwa tulio wengi; blogu yako ni kama dawa! Picha unazoziweka, zinaturudisha nyumbani - na kuzungumza kwa uwazi zaidi kuliko mtu angekaa na kujaribu kutuelezea. Anayekererwa na mafanikio yako - alie tu!
    Ned

    ReplyDelete
  11. komredi makene, mk na ned nawasalimu kwa jina la YESU. hao wasiotutakia mema WASHINDWEE! mie nawaambia hapa piga ua, aluta kontinua!!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2006

    Ameeeeeeeeeeeeeeen

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 08, 2006

    mzee michuzi, pole sana kwa yanayokukuta ndo mambo ya dunia. una uzoefu wa kutosha nategemea utawakabili.

    ReplyDelete
  14. Wewe ndugu wa mwisho umeongea maneno mazuri, Lakini naomba usitumie majina ya watu kufikisha ujumbe wako.

    Nashukuru,
    Copyright © 2006 MK, The Real MK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...