mh. amina chifupa akiondoka baada ya kuhudhuhuria sherehe za kukabidhiwa nyumba ya nancy sumari leo huko tabata chang'gombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2006

    Jamani hii ninakubali kweli bongo kutoka ni mtu yeyote, hupate channel tu...Yaani huyu demu alikuwa anauza maziwa pale kwao kwenye nyumba za ottu..Kutoka ushindi mpaka dodoma.Nampa hongera sana...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2006

    Good job Mh. Chifupa....maisha always you have to start from some where. If you are dreaMING...KEEP ON DREAM. .

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2006

    yaani hilo CRUISER na uchumi wetu wala haviendani. Hivi unaweza kuniambia kwanba akikaa humo na usiunajua tambo za kina mama/dada anaweza akatukumbuka kweli? yaani huo ndio wasiwasi wangu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2006

    Bwana Said, hii ni Lexus 470 Special edition...kuna tofauti kubwa sana kati ya Lexus na Cruiser.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2006

    Imeandikwa Land Cruiser lakini, au hujaona?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2006

    AAW ina stand for what?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2006

    hata mimi nashindwa kutafuta kirefu cha hiyo AAW,

    wewe anony hapo juu unajiuliza swali ambalo lina jibu na kwamba hata amina asipokukumbuka hatakuwa wa kwanza ndio utamaduni wetu,lakini anatakiwa kumshukuru sana mpakanjia hata akimwacha leo ana kitu cha kujivunia ambapo pia nina uhakika kumwacha ni ngumu ndio wakati wa kula matunda ila mshikaji mpakanjia una akili(msemo wetu wabongo mtu akifanikiwa), nyie wote mnaopiga kelele mtapiga tuuu wenzenu washachukua channel ndio hivyo
    tena risk katika maisha kufa au kopona ili ufanikiwe ndio aliyoyafanya mpakanjia, hata nyie mngekuwa nayo mngekuwa hivyo hivyo walivyo,makekele yenu kwenye blog ya michuzi hayafanyi lolote ni kujipa mioyo tu ya kiuongo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2006

    jamani naombeni mnieleweshe historia ya huyu mama maanake mimi nimekuja kumfahamu kwenye hii blogu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2006

    Hiyo aaw ni namba mpya za bongo sema haijaonekana namba yote kwenye number plate

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2006

    Naona trade mark ya Lexus na jina la Land Cruiser. Wabongo...Mtafungwa fanyeni masihara na majina ya watu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 03, 2006

    aliyeandika hii msg hapa juu namjua hata kama kasema yeye anony...

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2006

    ndugu anonymous amina chifupa sio mama bali ni msichana aliyemaliza form six mwaka 2001 pale makongo sekondari.kwa bahati mbaya alipata divisheni zero.kwa vile ana kipaji cha kuongeaongea akapata kazi clouds fm kama mtangazaji.baadae mimi nikaondoka bongo.nikapata habari kuwa kaolewa na bw.medi(cheki kwenye hii blog) ambaye ni mfanyabiashara.katika uchaguzi uliopita dada huyu alitumia haki yake ya kikatiba kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM na akafanikiwa.kwa hiyo sasa hivi ni mbunge.according to me katika nyanja hii ya siasa dada huyu hana future yoyote(maelezo zaidi yakihitajika nitatoa).hata hivyo nadhani watanzania ni vyema tumshukuru kwa mchango wake,hata kama tunahisi kuwa ni kidogo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2006

    ndugu anony ahsante sana kwa kunielewesha. na unaposema hana future yeyote unaamanisha nini? ni kwamba yeye kazi yake kutanua tu au?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2006

    Wewe anonymous hapo juu unajua maana ya mama ? kwa nini unasema Amina sio mama wakati hana mtoto .

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2006

    Hii gari ni LEXUS na siyo LANDCRUISER (LAND CRUISER 2006 MODEL hazina headlights zenye design kama kwenye hiyo picha).

    La muhimu kufahamu ni kwamba mtengenezaji wa magari yote mawili ni TOYOTA. Ukichunguza utaona hilo jina la LAND CRUISER limebandikwa kwenye GUARD GRILL ambayo nadhani ni maalum kwa LAND CRUISER lakini inaweza kutumika kwa LEXUS kwa vile magari haya mawili yanafanana sana.

    Hili ni gari la bei mbaya sana!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2006

    Inategemea na mahali ulipo.
    Still gari hilo liko kwenye kundi la Ladcruiser.
    CYGNUS,LEXUS nk

    vilevile kuna Alteza Japan ukienda Europe ni Lexus ,Windom ni Lexus , Harrier kwetu ni Lexus

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 04, 2006

    Hiyo michanganyiko yote ni kwetu kule 3rd World, Lexus na Land Cruiser katika gari moja mbona kwao hawafanyi hivyo? au bora liende tuu..Rejected cars!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 05, 2006

    Hili gari ni LEXUS LX 470 na siyo LEXUS LS 470.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 05, 2006

    Waheshimiwa,
    Mkienda Dubai kuna watu kazi yao ni kugeuza Landcruiser kuwa "Lexus" na hiyo mnayoiona hapo ni kazi ya mikono yao. Hayo niliyashuhudia mwenyewe

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 05, 2006

    anony uliyenitangulia hapo kweli umegonga Ikulu, mambo yote yanafanyika dubai. Nasikia kutoka japan wafanyabiashara wananunua magari yaliyo katika yadi kwa ajli ya kutupwa.. scrappers. halafu yanafunguliwa upya... yanaingizwa kwenye kontena, kwa hiyo unakuta yanabebwa kama vipuri.. mambo yote yanafanyika dubai, sasa kazi iko kubwa kweli kweli vipuri vinapoingiliana, nafikiri inaweza kuwa hayo ya mheshimiwa hapo juu... gari ikitoka kule ni mpya na bei yake ni nafuu kuliko unaponunua kutoka kule japani. sasa nani anajali? dunia ya tatu kuna kufuatia ubora? nani kakwambia kuwa maskini anajali sheria au anahoji? yeye ni kuangalia na kutia moto huyo kuondoka, hana muda wa kuhoji kwa kuwa lengo lake ni 'kuwakoga' watu kumbe anajikoga mwenyewe! kwa kweli dunia ya tatu kwa fikra ya sasa safari yetu bado ni ndefu sana!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 05, 2006

    ninaposema kuwa hana future katika fani hii ya siasa namaanisha kuwa observation niliyoifanya nimeona kuwa suala la Amina chifupa(AC) kupata ubunge limechukuliwa na jamii ya wasomi kama insult kwa sababu bibie huyu kiwango chake cha elimu ni form 4(form 6 alifeli).demokrasia siku hizi tanzania imebadilishwa kuwa pesakrasia yaani mtu anaweza kununua mpaka haki,hiki ndicho kilichompa AC ubunge.sasa kutokufanikiwa kwake kutasababishwa na vitu vitatu 1.wanasiasa wengi wa sasa ni wasomi wa level ya juu,angalia baraza la mawiziri la kikwete jinsi lilivyojaa maprofesa na ma ph dokta,AC atatumia brains zipi to come on top of them? 2. sasa hivi kuna akinadada na akina mama kibao ambao wana combination of both pesa na elimu ambao hiyo nafasi wataigombania katika uchaguzi ujao.hata hivyo hawa inabidi wamshukuru AC kwa kuwaonyesha kuwa inawezekana 3.AC hajaonyesha dalili zozote za kujiendeleza kielimu kwa kipindi cha miaka 5 tangu amalize form 6.alichofanya ni kutafuta cheti cha VETA cha kiaina ili aweze kuuficha ukweli kuwa elimu yake ni ya kidato cha 4.......hata hivyo iwapo AC ataruhusu watu wenye mawazo endelevu wamshauri anaweza kufanya wonders!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 05, 2006

    Anony,
    Sina mengi ya kusema kuhusu uliyosema hapo juu kuhusu AC. Lakini kuhusu hilo baraza la Kikwete Mmmmh, limejaa madaktari feki, Nchimbi, Chegeni, Nagu, Kamala n.k sasa AC atashindwaje kuwa na elimu japo ya degree ya kwanza akiamua kama wako watu wana Doctrate za Mrema type?

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 05, 2006

    Hivi pesa ya petroli analipiwa na Serikali?
    Maana hilo Motor linatumia Petroli na ukubwa wa injini ni cc5000.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 05, 2006

    mrema hana doctorate...AC tatizo ni kwamba ana cheti cha form four tu.hata hivyo hapo nimesema kuwa iwapo atapata watu wa kumshauri kujiendeleza then anaweza kufanya wonders,yeye mwenyewe AC hana iniciative ya kujiendeleza kielimu.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 06, 2006

    AAW sio nambari mpya za bongo, ila kwa sasa magari ya wabunge yanawekwa hizo alama ambazo zinawakilisha wizara zao.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 06, 2006

    Nimekubariana na aliyesema kuwa hana future katika siasa nafikiri nimeona discussion nyingi kuhusu gari. Hii ni tosha kabisa siyo kawaida watu kubishia gari. Nafikiri kuna tatizo hapa. Na tatizo watu wanafikiria katika kumukomboa mtanzania huitaji kuonyesha ufahari mkubwa kama huo. Watanzania watakasirika, bado ni masikini wa kupitia madirishani, kwenye daladala(ubungo). Na hawatachukua peasa. Nafikiri huyu dada kila akifanyacho kwanza aombe ushauri. Atafika mbali. Lakini pamoja na kutokua na Elimu namkubari uwezo anao tena wa kuelekeza watu, wenye vyeti feki vya udaktari wanajulikana muda ukifika Wataumbuka.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 06, 2006

    Mmebakia kumuandama dada wa watu kuhusu elimu, nyie mnaojifanya mmesoma na hivyo vibasic degree vyenu mmefanya nini cha maana? Acheni dada wa watu ale maisha kwani ameweza kuchanganya karata zake vizuri. Wengi mnashindwa hata kurudi nyumbani kwa sababu mnaogopa utata utaojitokeza umekaa nje miaka zaidi ya kumi halafu unarudi mikono mitupu. HONGERA SANA MHESHIMIWA MBUNGE AC, TUPO NYUMA YAKO

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 07, 2006

    Mheshimiwa Anonymous hapo juu, hacha maneno yako bwana. Utakuwaje nyuma ya mheshimiwa Mbunge AC? Kwanini usiwe naye bega kwa bega!

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 08, 2006

    Anony unayetuambia hizo namba zinawakilisha wizara za wabunge, wabunge wana wizara zipi? Muwe mnauliza kama hamjui kuliko kuanza kusema vitu utafikiri una uhakika. Hizo namba kwenye picha zimekatwa, zinaanzia juu, ambako ni T...AAW, hapo katikati kuna tarakimu tatu, mfano 123

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 10, 2006

    Benny780912,
    Hili ni gari binafsi, Nusu ya malipo ni kodi ya walalahoi na nusu wanakopeshwa hawa waheshimiwa sana.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 10, 2006

    maisha ni kuwini,kama mtu anaona Amina anamkera akazane huko kusoma!kama maisha yanapanda elimu itafuata tu!peta Amina usisikilize ujinga we kula nchi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...