mchungaji mtikila na viongozi wenzie wa upinzani akiongea na waandishi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2006

    kushoto kwa mtikila ni prof.shayo wa UDSM.naye pia aligombea urais.agenda yake kubwa ilikuwa ni kuomba ruzuku zirudishwe ili kuwawezesha wasio na fungu pia kushiriki katika uchaguzi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2006

    hili ndilo shujaa la haki za binadamu na za kikatiba.Usifanye mchezo bwana, Iringa ina impact katika siasa za Tanazania tangu wakati wa akina Chifu Mkwawa.Hongera sana mchungaji Mtikila,tutaonana katika uchaguzi wa 2010.Sasa angalia la wagombea wenza na kuungwa mkono katika pande zote mbili maana litachafua hili tuliloshinda.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2006

    acha moyo wa ukabila wewe tanzania ni nchi moja....mambo ya iringa etc yataharibu umoja wetu.huyu ni mtanzania hodari.hii inatosha sio mambo ya kuingiza ukabila hapa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2006

    Mtikila kilichobaki sasa jitahidi uwaunganishe wapinzani muwe na sauti moja. Achane Ubinafsi wapinzani Tz umimi utatumaliza milele.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2006

    Mtikila ameonyesha njia.Yapo mengi ambayo bado yamekaa kombo na ni jukumu letu sote kuhakikisha tunayaweka sawa.Aluta continua!

    ReplyDelete
  6. kwa taarifa yenu, serikali inakata rufaa kupinga hukumu ya kukomeshwa kwa 'takrima'

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2006

    2010 lazima tukagombee kwa sababu hakutakuwa na gharama za takrima, hivyo ni uwezo wako wa kuongea ndio utakao matter. Kwenye chama wakileta mambo yao ya umekifanyia nini chama unawamwaga na kuwa mgombea binafsi. SAA YA UKOMBOZI NI SASA WADANGANYIKA

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 08, 2006

    Micguzi, Siamini wanataka kufanya hivyo au ndio wanataka kuhalalisha gharama za kukata rufaa ambazo zitaonyeshwa ni mara tano ya gharama halisi? Hivi hawa CCM wanaitakia nini nchi yetu? Kama takrima ni nzuri kiasi hicho mbona kwenye uchaguzi wa CCM 2002 waliipiga marufuku. Watu wengine hata haya hawana. Pambafuu kabisa.

    ReplyDelete
  9. Mimi hapa nina furahi kwa suala la takrima tu lakini ktk swala la mgombea binafsi naona wamechemsha.

    Wamechemsha kwa sababu:

    a: Watapata wapi Sera za maana, Sababu sio wote watakao jua sheria.

    b: Watapata wapi pesa za kuendesha kampeni na ktk uchaguzi au ndio hasara kwa wananchi na pesa zetu za kodi ndio watapewa wao.

    c: Matajiri wengi kama akina Mengi, Wahindi, Waharabu watatumia pesa zao ktk kugombea nafasi mbali mbali na siasa huru itakuwa hakuna.

    d: Kama mgombea binafsi, atafuata Sera gani na sisi au Taifa tutafuata Sera gani kama wakishinda?

    e: Ukiangalia Mataifa mengi ya Afrika yenye machafuko, Vurugu yanatokana na kuwa na vyama vingi au makundi mengi sana ndani ya nchi au watu wengi kuwa ktk Siasa sasa ongezeko la wagombea binafsi ni kama kukaribisha yote hayo.

    f: Kwa wakati huu tu mambo sio mazuri sana hapo Zanzibar wakati kuna vyama vichache, je ongezeko la wagombea binafsi na wafuasi wao sio kuongeza matatizo sehemu kama Zanzibar au Tanzania kwa ujumla.

    g: Hii System ya wagombea binafsi sio nzuri kwa Tanzania sababu Tanzania ni nchi changa na hatuja komaa kisiasa labda hapo baadae sana tena sana. System hizi ni sawa kwa nchi zilizo endelea.

    Tunabidi tuangalie ni wapi tunaelekea watanzania na tuweze kutetea yaliyo mazuri kwa wote tusije tukaleta machafuko kwa sababu za wagombea binafsi.

    Nasubiri kwa hamu kwa Serikali kukata rufaa kuhusu wagombea binafsi maana kwa kuangalia mbali tu naona moto unatufuata.

    Haya yalikuwa ni mawazo yangu binafsi na sio lazima yawe sahii kwa wasomaji wengine.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 10, 2006

    kama selikali itakata rufaa kwa takrima basi mimi nitaamua kuomba hifadhi ya ukimbizi kwenye nchi za watu na nitaomba watanzania wote waombe ukimbizi wabaki hao wenye serikali wajitawale wenyewe benki, TRA, Forodha, Bunge vyote wachukue.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 11, 2006

    MK,
    Ni kweli hayo ni mawazo yako lakini ni mawazo finyu mno. Ninyi ndio mnaodanganywa eti vyama vingi vitaleta vita kama vya Rwanda. Ni nchi gani ina machafuko kwa sababu ya kuwa na wagombea binafsi?
    Kuhusu pesa za kampeni nani kasema watapewa na serikali? Mtu akiamua kugombea atajua atatoa wapi pesa. Hilo la sera hapo napo huna hoja. Ni wapi inaposema mtu huyohuyo akiwa ndani ya chama anakuwa na sera na akiwa nje hana sera? CCM ina sera zimetufikisha wapi? Kwani wewe hujui kuwa sasa hivi uongozi ni pesa? Unapata uongozi kadri unavyoweza kuhonga wapiga kura za maoni? Kama ni Wahindi na matajiri mbona sasa hivi ndio viongozi?
    Swala la mgombea binafsi ni muhimu kwa ajili ya watu wenye uwezo na sifa lakini hawaoni chama cha kujiunga nacho. Huwezi kuwalazimisha watu waingie kwenye chama hata kama maleno yake hawakubaliani nayo. Ndio hayo ya sasa watu wanakimbilia CCM si kwa sababu wanataka bali wapate ulaji.
    Kama ni machafuko yanaletwa kibri cha kujifanya CCM iko juu ya sheria na hivyo kukiuka maamuzi yanya mihimili mingine ya dola.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 11, 2006

    MK,
    Ni kweli hayo ni mawazo yako lakini ni mawazo finyu mno. Ninyi ndio mnaodanganywa eti vyama vingi vitaleta vita kama vya Rwanda. Ni nchi gani ina machafuko kwa sababu ya kuwa na wagombea binafsi?
    Kuhusu pesa za kampeni nani kasema watapewa na serikali? Mtu akiamua kugombea atajua atatoa wapi pesa. Hilo la sera hapo napo huna hoja. Ni wapi inaposema mtu huyohuyo akiwa ndani ya chama anakuwa na sera na akiwa nje hana sera? CCM ina sera zimetufikisha wapi? Kwani wewe hujui kuwa sasa hivi uongozi ni pesa? Unapata uongozi kadri unavyoweza kuhonga wapiga kura za maoni? Kama ni Wahindi na matajiri mbona sasa hivi ndio viongozi?
    Swala la mgombea binafsi ni muhimu kwa ajili ya watu wenye uwezo na sifa lakini hawaoni chama cha kujiunga nacho. Huwezi kuwalazimisha watu waingie kwenye chama hata kama maleno yake hawakubaliani nayo. Ndio hayo ya sasa watu wanakimbilia CCM si kwa sababu wanataka bali wapate ulaji.
    Kama ni machafuko yanaletwa kibri cha kujifanya CCM iko juu ya sheria na hivyo kukiuka maamuzi yanya mihimili mingine ya dola.

    ReplyDelete
  13. Naheshimu mawazo yako, Hayo yalikuwa mawazo yangu tu na sio lazima yaendane na ya kwako.

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 11, 2006

    Mie nasubiri tu serikali ikikata rufaa nitaukana UTz na kuomba uraia huku nilipo ya nini kuwa raia wa nchi inayongozwa na watu wasiojali raia wake.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 12, 2006

    Nilikuwa sifahamu kama kinyume cha finyu ni bora, mie na Udigo wangu nilikuwa nafahamu kuwa kinyume cha finyu ni pana. Na hapa ndipo matumizi ya neno finyu yanapokosa/pata ustaarabu. Asante sana Zemarcoplo

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 12, 2006

    Ok siyo mchezo usitaarabu mk

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 16, 2006

    Pamoja na mk kuwa mstaaarabu naomba next time abadilishe jina lake make inaonekana kila sehemu wanamkimbiza anapochangia anachemsha. Naomba ambadili jina hili azaliwe upya. samahani mk huo ni ushauri na mawazo binafsi hivyo yasikusumbue sana. Yafikirie tu wewe jifue badili jina na uzaliwe upya.

    ReplyDelete
  18. Hayo ni mawazo yako, Na kila mwanadamu ana mawazo yake na pia sio lazima kuyafuata.

    Sijui ni lipi lililo kufanya kuongoa hayo na kama ni mawazo mazuri au mabaya (fikra nzuri au mbaya) lakini nina kuheshimu kwa yote.

    Ni wapi umeona kila ninapo changia nina chemsha?

    Ni mawazo yako ndio unaona nina chemsha! Kwanini na wewe usiweke jina lako wazi na kuweza kuona unavyo changia!

    Binadamu tunatoana kasoro lakini atuangalii nafsi zetu kwa undani zaidi, Na sijui ni vitu (mawazo) gani yanayo tupeleka kuwaza hayo maana haunijui na mimi sikujui na ni lipi kujifanya unanijua?

    Muheshimiwa mimi siwezi kubadili jina kwa sababu ya kwako na hizi sababu sijui ni kutokana na roho nzuri au roho mbaya uliyo nayo ktk nafsi yako iliyo kufanya kuongea hayo.

    Katika Internet au blog ni wachache ndio tunajuana hivyo basi tuweze kuheshimiana kwa dhati kama ninavyo waheshimu watu wote ukiwamo wewe, kama kuna sababu nyingine zilizo kufanya uandike hayo naomba ziweke wazi maana utawafanya watu wajiulize una waza nini? au ni sababu gani zilizo kufanya uongee hayo? Roho nzuri au Roho mbaya? Unaona wivu au Hauoni wivu?

    Mungu akubaliki na awabaliki wote.

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 16, 2006

    Ila kweli Anony hapo juu kafuatilia comments zako Mk sehemu nyingi unabore. Kwa nini WaTz hamfurahii kuambiwa ukweli Pole sana Bro, lakini ukweli ndio huo aliosema jamaa hapo juu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 16, 2006

    Mimi namshauri Mk asibadili jina ila tu zile mada ambazo zipo nje ya uwezo wake asichangie. Sio lazima uchangie kila kitu. Kila mtu ana eneo lake analolijulia zaidi. Huwezi kuwa mtaalamu wa kila kitu bwana wee Mk uwe tu unavizia zile mada nyepesi nyepesi.

    ReplyDelete
  21. Nashukuru ndugu zangu kwa maoni yenu yote mnayo yatoa kuhusu nafsi yangu. Mna haki ya kusema chochote kile sababu ni haki yenu.

    Kwa kweli ni vigumu kujuana kila mmoja wetu kupitia blog au kupitia Internet.

    Mnaweza kusema yote ktk maisha lakini ukweli utabaki ya kwamba ni vigumu kunijua nafsi yangu kwa undani.

    Kuhusu kuchangia mada mimi nina uwezo kuchangia mada yoyote ile maana nina uhakika nina uwezo wa kutoa maoni ktk kila sekta yoyote ile iwe siasa, jamii, Computers, Biashara, n.k , na pia ktk dunia hii tunayo ishi inaitwa dunia huru ambayo hakuna kiumbe chochote kile zaidi ya MUNGU kinacho weza kuniwekea limit za kuchangia mahali popote pale ata kama mkitumia u-dikiteta.

    Naomba mniambie ni comments gani zangu ambazo zina bore? Na kama zina bore ktk nafsi zenu sio kuniondolea mimi haki yangu kuchangia kile ninacho ona ni sahihi sababu hii ni dunia huru na wote tunaishi ktk mataifa huru iwe Tanzania, UK, US au popote kule mlipo.

    Naomba muendelee kuwa huru na muweke majina yenu wazi na msiogope kuweka wazi pale kila mnapo sema mabaya kuhusu nafsi yangu.

    Yoyote anae chukizwa na mimi iwe kutokana na Roho nzuri au Roho mbaya, Wivu au sio wivu napenda kutoa taharifa kwenda kwenu mimi nitaendelea kuwa hapa hapa na kuendelea kutoa maoni nikiwa huru ktk kila sekta, na nina uhakika MUNGU atawasaidia kuwaondolea mawazo yenu yote mliyo nayo.

    Mwisho, Mimi ni MK na nitaendelea kuwa MK daima na kamwe siwezi kubadili jina kwa chuki zenu binafsi. Ni vizuri mkiendelea kufanya kazi zenu na kujali maisha yenu au familia zenu na kuniacha nafsi yangu.

    Wote mnao sema vibaya kuhusu nafsi yangu nawaomba mbonyeze hapa.

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

    Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa, Mungu awabariki nafsi zenu.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 17, 2006

    Watu wawe na chuki binafsi na wewe Mk wanakujua kwani. Watu nadhani walichoandika hapo juu labda ni kutokana na contribution zako kwenye hii site. Wewe usimind wala nini we endelea kuchangia kama kawaida asiyependa asisome maoni yako. Binadamu hawa ukiendelea kujibizana nao ndio wanafurahi na wataendelea kukuchanganya zaidi.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 19, 2006

    Yes samahani sana mk, mimi di anony nilioanzisha mjadala huu wakati mwingi huwa nampima mtu baada ya kuona contribution zake nafatilia kujua kama najua kweli anachokiandika. Mzee nimekubali baada ya kupiga ka wimbo. Nimefatilia sana reaction zako nimegundua kuwa ni mtu aliye elimika kabisa. Nafikiri uko stage fulani katika kuelewa mambo, uchokozi wangu huo ni wakawaida. Naweza nikaona uko sahihi lakini nikataka kujua kama unachosema unakijua kweli. Nakufanyia utafiti nimekubali unajua mambo mengi na ni mstaarabu kweli. Sasa ili kujua kwamba ndio mimi nitakapo kuwa naandika kwa kitu ulicho andiaka. nitakuwa naongeza mzeemk, kumanisha heshima niliyokupa kuwa una busara. Usichoke make kuandika ndio fani yangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...