mlio ughaibuni hapa ni ni mtaa gani. jengo linaitwa zahra towers

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Michuzi kwa jinsi mambo yanavyo kwenda haraka haraka, ngoja nirudi nyumbani maana nisije siku nikapotea wakati wa kurudi si unaona mabadiliko hayo!! Safi sana.

    Nashukuru,
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2006

    Hapo Makunganya Street, ukienda mbele kuna round about, kulia Maxoms Bureau de change!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2006

    Mtaa wa Indira Gandhi

    ReplyDelete
  4. We Ken (MK - nimekugundua) - Kalang'abaho... mambo Dar yenda yakiongezeka kwa kasi sana. Mwenzako nikienda"ga" huko ni kutokwa na macho tu... sio kama sijaona majengo makubwa, lakini ni ile hali ya kutokuamini mabadiliko yanayotokea Dar. Kuna nyumba kama 2 - 3 maeneo ya Kariakoo - ambazo mwaka jana nilipokwenda zilikuwepo... NIliporudi mwezi huu wa March... tayari yeshakuwa "leveledL na badala yake wababe wanaweka "high-rise". KWa sehemu ni jambo la kujivunia, kwa sehemu ni kuanza kufikiria wakina mzee "Jongo" - wakazi wa asili wa maeneo hayo - na hatima yao.
    Cha kutia moyo ni kuwa hata hawa wenzetu nao walianza hivyo hivyo - hatimaye hata mtu wa chini alipata makazi ya maana (bei inashuka with an increased supply) - Labda ndipo tuendapo... good stuff
    Ned

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2006

    Uzuri wa majengo kama haya ni vivutio kwa wawakezaji. maanake wawekezaji kutoka nje huwaga wanapenda ofisi zao ziwe kwenye majengo ya kisasa. halafu bomoa bomoa bado inaendela. Michuzi, nasikia pia kuna mall kubwa na business center zinajengwa hapo mlimani city. naomba nieleza.
    James

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2006

    Ni kweli itavutia wawekezaji, Ila tukumbuke pia kwamba mji haukuwa designed kukidhi majengo ya jinsi hiyo. Maji, umeme, drainage systems na vitu kama hivyo ni jambo la kufikiria pia kabla hatujaongeza tu majengo katikati ya mji. Je kwani ni lazima kujenga katikati ya mji? Kwa nini tusione mbali na kuanza kujenga nje ya mji ili kupanua mji? hii itapunguza sana misongamano isiyo na sababu pale mjini.
    Kwa wale waishio ughaibuni watakubaliana nami kwamba mtu si lazima uende Manhattan ili kupata mahitaji muhimu kwa vile unaweza ukayapata popote pale.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2006

    Michuzi naomba utuwekee picha ya hayo majengo mapya ya BOT na hilo la mafuta house sisi wengine tunasikia tu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2006

    Anan nakuelewa, sio lazima ujenge katikati ya mji ndiyo maana sasa hivi watu bongo wanaanza kujenga maofisi ya kisasa sehemu kama ubungo (ubungo plaza), mlimani (mlimani city project), kijitonyama (millenium towers) etc.lakini kama kuna majengo katikati ya mji (hasa majengo ya NHC) ambayo yamechakaa, basi wacha wayabomoe wanaendelee kuporomosha ya kisasa. halafu nasikia pia wanataka kuanzisha rapid bus transit system ili kundoa msongamano wa daladala hasa vituo vikuu kama posta, kariakoo etc.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 06, 2006

    Brother Michuzi sasa tunaomba ututafutie mambo ya kazi, maana hii blog sisi tulio ungaibuni inatufanya turudi nyumbani. Shukrani !

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 06, 2006

    Hivi mtu unaweza kurudi nyumbani simply kwa sababu ya jengo zuri ? Please give me a break ....Watu mnachanganya mambo sana tunapozungumzia maendeleo hatuzungumzii majengo mazuri. Kwa nini majengo yote yanajengwa katika mji mmmoja tuu ? kwa nini hakuna uwiano wa maendeleo katika miji Lindi , singida, Tabora....n.k

    Michuzi nakuomba sana utuwekee picha za Lindi na mtwara , especialy hotel yetu ya kimataifa ya litingi ..pia kama ukipata picha za kitangali, lukuledi , newala na mchinga ningefurahi sana .

    Michuzi pia naomba sana sana uweke picha ya Mbunge wetu mpendwa wa lindi mjini Mohamed abdulaziz maarufu kwa jina la "SILIPI DENI"

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 06, 2006

    Wewe anon kutoka lindi, haya majengo sisi wengine hatukuyaacha na yavutia. tunaelewa kwamba mikoa mingine haijapiga hatua, lakini kwa mtu kama mimi ambaye sijafika bongo for 15 years lazima nishangae kwa sababu jengo zuri nilioloacha ni extelecom na bima. lazima pia uelewe hata wawekezaji wanavutiwa na majengo kama haya.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 06, 2006

    wewe kwa nini huendi kwenu miaka 15 hiyo ni kufuru!!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2006

    hayo ni maendeleo,lakini hatuna budi kufanya research kabla ya kuporomosha hayo majengo

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2006

    Lazima tuangalie huu utitiri wa majengo makubwa yanasaidiaje uchumi wa mwananchi wa kawaida. Kama tutakuwa na majengo makubwa hata mpaka Lindi na Nachingwea lakini contribution yake kwenye pato la mtanzania ni kama hakuna yatakuwa hayana maana. Duh Anony hapo juu inakuwaje mkuu miaka 15 hujaenda kwenu, tatizo ni kuondoka kwa KUZAMIA au huna nauli ndugu. Mimi nina wasiwasi uliondoka kwa kuzamia hivyo ukirudi kwenu itakuwa tabu kuja tena huku una pasport ya tz kweli wewe maajabu. Kama tatizo ni nauli anika account yako hapa tutakuchangia uende utakuja kuta ndugu zako wote hawapo.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 07, 2006

    Mzee grill unanimaliza. Jamaa kweli inabidi asaidiwe kwa sababu miaka 15 ni mingi mno.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 08, 2006

    mbele ya mnugu anarudije nyumbani huyu kabanwa hapo hata kupumua hapumui ndo maaana anasema kabisa kwa ufahari amekaa miaka kumi tano hata aibu hasikii.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 09, 2006

    Michuzi hebu tujibie swali ulilouliza manake hapa tuna majibu mawili MTAA WA INDIRA GANDHI au MTAA WA MAKUNGANYA. ipi sahihi sasa?

    ReplyDelete
  18. hapa ni kona ya makunganya na zanaki

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 13, 2006

    Asante michuzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...